MBONA KAMA MO DEWJI ANATAFUTIWA SABABU?mtakimbiza matajiri nyie acheni ujinga

N

nzagambadume

JF-Expert Member
2,071
2,000
Nakumbuka kikwete alivyokuwa kila mara anasema anataka kuzalisha mabilionaires na marais wengi hufurahia mabilionea wanavyoongezeka lakini hapa kwetu ni kinyume utawala huu wa awamu ya tano,jamani mengi keshakufa,manji na matajiri kibao wa kihindi wamehamishia mitaji zambia na kenya sasa inaonekana ni zamu ya huyu kijana kuungua moto maana hiki kipeperushi cha musiba na kama kipaza sauti tu.halafu mbona this time wanaogopa sana uchaguzi wa 2020?kuna yanayofukuta sisi hatuyajui?
Matajiri wenyewe wa sasa ni kina bashite wanaomiliki ma hotel,ma apartments na magari ya kifahari au ndo mnataka warithi kina MO?msituletee ya zimabwe tafadhali,hali mtaani ni mbaya sana,msituchoshe.
Dah sipati picha Yanga watakavyoshangilia masaibu yanayokuja.
 
darcity

darcity

JF-Expert Member
4,859
2,000
Hivi nani anasoma hili gazeti? Na analipa wafanyakazi wake vipi/kwa faida ipi? au ndio yuko na waandishi wake wawili watatu wanatengeneza habari za kubuni na tetesi za vijiweni kisha kuchafua watu waliotumikia taifa kwa heshima
 
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
6,641
2,000
Picha haitoshi ,maudhui ni muhimu yawekwe wazi tuyachambue na kuyapima
 
issac77

issac77

JF-Expert Member
2,534
2,000
Hivi nani anasoma hili gazeti? Na analipa wafanyakazi wake vipi/kwa faida ipi? au ndio yuko na waandishi wake wawili watatu wanatengeneza habari za kubuni na tetesi za vijiweni kisha kuchafua watu waliotumikia taifa kwa heshima
mkuu heading za hili gazeti haziandikwi andikwi tu... kuna mikono ya watu wazito hapo! ukiona umeandikwa hapo tena #frontpage jua kuna jambo linakunyemelea!
 
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
12,344
2,000
mkuu heading za hili gazeti haziandikwi andikwi tu... kuna mikono ya watu wazito hapo! ukiona umeandikwa hapo tena #frontpage jua kuna jambo linakunyemelea!
Hivi jamani huyu mtu kwanini asipingwe ?! Ni Mungu ?!.

Kuna shida gani waTz wengine nao wakichangia mawazo yao ktk ujenzi wa taifa hili ?!.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
T

Taso

JF-Expert Member
2,091
2,000
Rostam na Manji na Mo na mdosi yeyote hawawezi kukimbia Tanzania kwa sababu hakuna sehemu duniani wataenda kupiga hela na kulambwa lambwa miguu kama hapa kwao Tanzania. Kitakachowashinda Tanzania (kodi, madeni, siasa) ugenini Zambia ni kigumu mara mia. Ni kama Diamond alivyotishia kuhamia Kenya, siku ya tatu Kenya wakamnanga alipe kodi zao na aache matusi hata Kenya. Karudi kwao tuko nae kwa Mtogole na Madale na Uwanja wa Fisi.

Worth repeating: hakuna sehemu duniani Mhindi ataenda kusujudiwa kama Tanzania, hawaondoki ng'o. Na wakiondoka good riddance, watazaliwa wengine, wata fill the void.
 
Louis II

Louis II

JF-Expert Member
2,728

Mmmh Aisee
 
Louis II

Louis II

JF-Expert Member
2,728
2,000
Nakumbuka kikwete alivyokuwa kila mara anasema anataka kuzalisha mabilionaires na marais wengi hufurahia mabilionea wanavyoongezeka lakini hapa kwetu ni kinyume utawala huu wa awamu ya tano,jamani mengi keshakufa,manji na matajiri kibao wa kihindi wamehamishia mitaji zambia na kenya sasa inaonekana ni zamu ya huyu kijana kuungua moto maana hiki kipeperushi cha musiba na kama kipaza sauti tu.halafu mbona this time wanaogopa sana uchaguzi wa 2020?kuna yanayofukuta sisi hatuyajui?
Matajiri wenyewe wa sasa ni kina bashite wanaomiliki ma hotel,ma apartments na magari ya kifahari au ndo mnataka warithi kina MO?msituletee ya zimabwe tafadhali,hali mtaani ni mbaya sana,msituchoshe.
Dah sipati picha Yanga watakavyoshangilia masaibu yanayokuja.
View attachment 1109390
MO ameingia anga za Msiba
 
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
5,510
2,000
Jamani kuna vita ya matajiri??
Watu wamefunga biashara wengine wamehama nchi.
Kwa nini kuwr na roho mbaya na matajiri??
Si tulikubali biashara huria, tumelogwa na nani kubomoa uchumi!!
Acheni kina Mo wafanye biashara iko nini bandugu??
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
34,714
2,000
msiwe na presha,matajiri wa kisukuma mbona tupo wengi sana?,tutaziba nafasi ya hawa wahindi bila tabu,kama Mo anamsaidia mnyaturu mwenzie Lisu,Musiba ana haki ya kuweka wazi,hatupendi mambo ya chinichini,mfano juzi Nyarandu alinaswa akila rushwa kule singida vijijini,akifikiri serikali haioni,serikali ako na mkono mrefu
 
aisee hali ni tete,jana nilikuwa sehemu naangalia mechi ya arsenal dah hadi huruma wadau wanalamba bia kama pipi,bia ya 1500 dakika 90...aisee haya ni majaabu wasukuma wamevuruga kwelikweli
 
I

Ijura

JF-Expert Member
360
500
msiwe na presha,matajiri wa kisukuma mbona tupo wengi sana?,tutaziba nafasi ya hawa wahindi bila tabu,kama Mo anamsaidia mnyaturu mwenzie Lisu,Musiba ana haki ya kuweka wazi,hatupendi mambo ya chinichini,mfano juzi Nyarandu alinaswa akila rushwa kule singida vijijini,akifikiri serikali haioni,serikali ako na mkono mrefu
Upumbavu mtupu
 
Forum statistics

Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom