Mbona Freemason kitengo cha Ulaya hakipendelei kafara kama kitengo cha Afrika

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,191
13,614
Mzuka wanajamvi!

Hatujawahi kusikia watoto au ndugu wa Bill Gates, Jeff Bezos, Mak zugeberg na wengine matajiri ulaya wakipoteza maisha kizembezembe.

Je, Freemason kwa kutoa kafara ni wabaguzi wameegemea tu huku kwetu Africa? Ama Africa kafara zetu zinathamani sana?

Yani unakuta mmatumbi anatozwa kafara hata kwa utajiri wa million hamsin tu 25,000 USD can you imagine? Halafu masharti kibao.

Mimi nachoona hii dhana ya ufree Mason ni uongo na potofu. Kwa kifupi haipo.

Ni kufanya kazi tu kwa Weledi na bidii. Utajiri ni bahati lakini kuishi maisha mazuri na bora ni maamuzi.

Tusishawishike kuwatoa kafara ndugu na wapendwa wetu kwa kumbatia imani potofu.
 
Hamna yeyote anae ijua Freemason,HAKUNA. Freemason ni secret society,Ukishaelewa maana ya neno SECRET ndio utakubaliana namm kuwa HAKUNA yeyote ataeweza kuja hapa kusema lolote wala chochote.

everything will remain as a secret. Kanuni na vigezo kuzingatiwa.
 
Wajenzi huru.
Hivi baada ya Andy Chande kufariki mikoba nani kaishika ?
Halafu kwa hapa Tanzania wajenzi huru maarufu ni kina nani so far.!?
Freemason Haina upuuzi kama huu tunaoambiwa Africa, ile Ni taasisi ya siri imara sana na Kongwe
 
Na hao ndio wanajua Mungu/Nguvu kuu ya dunia hii kwa uhalisia wake...sisi wanasukumizia ukristo na uislam sababu wanajua ni dini feki.
Hamna yeyote anae ijua Freemason,HAKUNA. Freemason ni secret society,Ukishaelewa maana ya neno SECRET ndio utakubaliana namm kuwa HAKUNA yeyote ataeweza kuja hapa kusema lolote wala chochote.

everything will remain as a secret. Kanuni na vigezo kuzingatiwa.
 
Kwani Afrika tuna dogo!.. huku hata muuza maandazi tu akitoboa utaambiwa ni freemason!.. kafara za kuua zinaaminika Sana huku kwetu maana ndio uchawi ulipolalia..😂
 
Kufanya mema yanayoendena na asili/nature na mazingira yanayonizunguka ndio dini yangu mkuu.

NB: ninaamini kuna Mungu/ Nguvu Kuu inayo endesha dunia hii.
 
Back
Top Bottom