Mbona bei ya chipsi yai haipungui licha ya mayai kushuka bei?

Shinnok

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
236
562
Hawa jamaa wauza chipsi-yai walikuwa wanatuongezea bei kila kukicha viazi vikipanda bei au mayai yakipanda bei.

Wametutoa kwenye 250 chipsi yai mpaka 1500. Baada ya hapo bei ikawa inapanda kadiri mayai yanavyopanda bei mpaka kufikia bei ya 2500.

Cha ajabu mayai yameshuka sana bei siku hizi; trei ni Tsh 4000 tu, ikizidi sana 4500 au 5000 kutoka 9500 mpaka 11000 kwa trei.

Yai moja moja kwa sasa linauzwa 250 mpaka 200. Cha ajabu jamaa hawajashusha bei yao
hapa wanatuibia.
 
Back
Top Bottom