Mboga za majani zinauzwa zikiwa bado na dawa ,ni hatari kwa afya ya binadamu .

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,851
15,265
Wakulima wetu wameingiwa na tamaa ya pesa, na haswa wakulima wa mbogamboga wamekuwa hawajali afya ya binadamu tena.

Siku hizi kunatokea kwa magonjwa mbalimbali kwenye mazao mfano ugonjwa wa kimamba ambao huaribu mimea na kuifanya kuwa njano, na hata wadudu mbalimbali,

jambo hili limekuwa likiwapasua kichwa wakulima na hivyo hupiga dawa mara mara hata kama imebaki siku mbili kuvuna yeye hajali kuhusu afya ya mlaji ila anachojali yeye ni pesa yake irudi.
Hivyo mlaji au mnunuzi hununua mboga hizo bila kujua kama siku mbili au tatu nyuma zilipigwa dawa yenye sumu.

Dawa za kukuza na kunenepesha mazao nalo pia ni tatizo lingine kwa mlaji kwani mazao hayo yanalazimishwa kukuzwa kwa haraka haraka kwa kutumia mbolea fulani au madawa.

Kama ukiwa karibu na Mkulima au kama wewe ni mkulima utagundua ukweli wa haya

Mambo hayo yote tajwa hapo juu yamekuwa yakiharibu afya ya binadamu au kumuua taratibu na magonjwa mbalimbali kama vile cancer, bila kujua chanzo haswa,kumbe ni aina ya mazao ya siku hizi hayo anayotumia bila kujua.

Elimu na ufuatiliaji zaidi kwa wakulima inatakiwa kuokoa afya zetu.
 
umeonhea vyema kabisa sasahivi hili ni janga unapika mboga inanuka dawa kabisa, nafikiri mabwana afya wanakazi ya kufanya hapa tunauwawa jamani
 
Usemalo lina ukweli, siku hizi hata mboga nyingine ambazo sio chungu unashangaa huu uchungu kwenye mboga inakuwaje??
 
Ukienda sokoni hakikisha unanunua mboga ambazo zimeliwa na na wadudu! Tafsiri yake hazina au zina dawa chache!

Mboga kijani kibichi haina hata tundu moja la kuliwa na mdudu iogope hiyo, imepuliziwa dawa ya kutosha!
 
Back
Top Bottom