Mbio za Watuhumiwa "UFISADI" Kwenda Mahakamani Zimeishia Wapi?

RA hawezi vya mahakama yake ni ugaidi tu wa kuhujumu roho za wafichuzi wake kisiri,ila siku zake zinahesabika kuingia 18 ya mkondo wa sheria kwa ufisadi.
 
Nijuavyo mimi RM alifungua kesi dhidi ya RA kwa kukashifiwa, ila sikumbuki alidai kiasi gani (nadhani kitu kama 10bn/-). Lakini RA naye alimfungulia RM kesi siku chache baada ya RA kufungua yake. Mpaka sasa naona ni ngoma droo. Tusubiri kesi hizo zipangiwe majaji ngoma ianze. Ila nadhani RA kafungua hiyo kwa kudhani kwamba RM atakubali yaishe, kumbe hajui mwenzake ana ushahidi wa 'kufa mtu' wa ufisadi wa huyu Muajemi, wakati yeye vielelezo vyake alivyovipeleka Takukuru nasikia ni feki. Hebu tusubiri.
 
Inavyofahamika, kesi za madai haziwezi kwenda kasi. Kwanza inashangaza mnasahau chronolgy of events (mtiririko wa time) wa mambo yalivyo-take place na kitu gani kilichotendeka. Nitawakumbusheni:

1. Baada ya RM kutoa tuhuma dihidi ya 'mapapa' (kwanza tuhuma dhidi ya baadhi yao, hususan RA zilishatolewa na Dr Slaa kule Mwembe Yanga mwaka 2007) -- RA naye akatoa tuhuma dhidi ya RM -- zile za "papa nyangumi."

2. Kilichofuatia ni kwamba RA hakwenda mahakamani kwa maana inayoeleweka. Alikwenda tu kutoa ushahidi na vielelezo kwa TAKUKURU.

3. Baada ya hapo RM alikwenda mahakamani kufungua kesi dhidi ya RA kwa
kumkashifu, akipinga tuhuma za RA moja baada ya nyingine.

4. Ikapita mda mrefu ambapo hatimaye RA, bila shaka baada ya kugundua kuwa kupeleka vielelezo, ushahidi TAKUKURU siyo "kufungua kesi", naye rasmi alifungua kesi dhidi ya RM ya kukashifiwa kutokana na zile tuhuma za awali za RM za "mafisadi papa."

Aidha inashangaza mtoa thread hii kuhoji et kipi kinachoendelea kuhusu kesi aliyofungua RA dhidi ya RM, wakati kufunguliwa kwa kesi hiyo kulikuja mwisho kabisa. Kwa nini asihoji kipi kinaendelea katika kesi iliyotangulia mwanzo kabisa ya RM dhidi ya RA?

Au tusema mtoa thread katumwa?
 
Kumbe alifungua kesi ya madai na mtu anapinga hapa jamani .Upenzi mwingine bwana .Yes nataka kujua kama kuna move zozote hata kama ni madai ama jinai .Ningalipenda sasa kujua kama kasi ile ya vyombo vya habari bado RA anayo .
 
mkapa.jpg
Mhhh
 
Zimeishia pale pale kama za wale waliowataja zilipoishia...kwa maneno mengine, majina yametajwa na kitakachofuatia hakuna. CCM na Kikwete watachaguliwa tena kwa asilimia kubwa tu. Anayebisha na asubiri aone....hamna haja ya kuandikia mate wakati wino upo. 2010 sio mbali...

Nyani Ngabu, i have quoted your 2007 post, times are saying exactly what you predicted. Kweli waafrika ndivyo tulivyo.
 
Mbio za sakafuni huishia ukingoni! sasa mbio za ufisadi zimeishia kwenye siasa na maandalizi ya october 2010
 
Back
Top Bottom