Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,241
Hivi kweli hizi mbio na matamshi makali makali kwenye vyombo vya habari kwa hao watuhimiwa kuwa wangewafikisha watoa tuhuma mahakamani zimeishia wapi... au hisia zetu kuwa hiyo ilikuwa mikwara mbuzi zimekuwa kweli?...
Posted Date: 11/17/2007
Mbio za watuhumiwa wa ufisadi kwenda mahakamani, zimeishia wapi?
Na Ramadhan Semtawa
KUITWA fisadi kama si fisadi huwa inaumiza roho kweli, kiasi ambacho, kama ni tuhuma za uongo, mtu huweza kupata kesi kwa kuua anayemtuhumu.
Hii inaumiza zaidi kwa mtu aliyepewa dhamana ya kuongoza idara yoyote katika ofisi ya umma, ambayo huendeshwa kwa kodi inayotozwa kwa sehemu kubwa kutoka kwa wavuja jasho wa nchi hii yaani wakulima na wafanyakazi.
Nasema kodi za wakulima na wafanyakazi, ndiyo! najua matajiri wengi ambao ni wafanyabiashara katika nchi hii hawalipi kodi na hawa ni wahujumu wakubwa wa uchumi wa nchi, lakini hii si mada yangu.
Hapa najadili na kuangalia heshima ya madaraka ya umma katika siku hizi na zama zile wakati wa serikali ya chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho hadi leo bado kinabaki kuwa msingi wa maadili ya uongozi wa umma.
Heshima ya madaraka ya umma imesisitizwa sana katika moja ya ahadi kumi za Mwana TANU, kwamba "Cheo ni Dhamana", kwa mantiki hiyo, aliyepewa dhamana hiyo hakutakiwa kuitumia kwa maslahi binafsi.
Iliwezesha kuwepo heshima ya madaraka ya umma na kuzingatiwa kwa maadili ya kazi, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ufisadi.
Ufisadi katika awamu ya kwanza chini ya serikali ya TANU, ulipigwa vita kwa nguvu zote, hivyo mtu aliyetuhumiwa au kubainika na rushwa au kuhujumu uchumi alijihisi kama mhaini na aliomba ardhi ipasuke.
Nchi hii ilikwenda vizuri, waliokuwa wakifanya ufisadi ambao ni pamoja na kuhujumu uchumi, walihofu kweli na kila mmoja alikuwa akitaka kulinda heshima yake katika jamii na nafasi ya madaraka aliyonayo.
Hii imenisukuma kujadili hawa ambao walitajwa na wapinzani kwamba ni mafisadi, baadhi yao walikaa kimya lakini wengine wakatamka kwenda mahakamani kujisafisha.
Binafsi, nilijawa na hamu kuona wapi watuhumihawa hawa wangefungua kesi zao na lini hasa ili kujisafisha na tuhuma hizi.
Kwa maana, hawa ni watu ambao heshima zao katika nchi zimechafuka, Watanzania wengi wanawaona ni watu waliohujumu uchumi tu kutokana na tuhuma hizo za ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma.
Kibaya zaidi hata watoto au ndugu zao ambao wana upeo, hawawezi kujisikia vizuri katika mkusanyiko na wenzao wanaposikia baba zao wanaitwa mafisadi na pia si heshima kwa mtu anayeongoza ofisi ya serikali kuitwa fisadi.
Hii ni dhambi na aibu kubwa , kutuhumiwa kufanya ufisadi kwa nchi masikini kama Tanzania ni dhambi kubwa ambayo lazima mtu athibitishie umma undani wa tuhuma kwa kutumia vyombo vya sheria.
Kwa maana tuhuma za kuhujumu uchumi kwa kutumia madaraka ya umma katika nchi kama hii yenye watoto wanaokufa kwa malaria kila kukicha na akina mama na dada zetu wanaojifungulia vichakani vijijini, ni dhambi kubwa.
Hii inatosha kwa mtuhumiwa wa ufisadi kwenda haraka mahakamani ili umma ujue kama kweli ni fisadi au si fisadi.
Ndiyo maana niliposikia akina Gray Mgonja Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Patric Rutabanzibwa, Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Nazir Karamagi, Waziri wa Nishati na Madini, wanakwenda mahakamani nilifurahi.
Hii inatokana na tuhuma zinazowakabili kuwa kubwa ambazo mtazamo wangu ni za kuhujumu uchumi wa nchi kwani mamilioni wanayodaiwa kuhusika nayo katika upotevu au mikataba isiyokuwa na maslahi kwa nchi, ni mengi.
Kibaya zaidi, watu hawa ni bora wangekaa kimya kama baadhi ya wenzao lakini walijigamba kwenda mahakamani matokeo yake hadi leo hii haijulikani mbio zao zimeishia wapi?
Hii inatoa taswira mbaya kwa umma, umma unajenga hisia kwamba hizi tuhuma za ufisadi dhidi ya hawa wana wa nchi wanaotajwa, ni za kweli hivyo kuamsha hasira zao.
Umma huu umechoka, tayari umepigwa na umasikini huku maisha yakzidi kuwa magumu siku hadi siku, thamani ya fedha ikizidi kuporomoka ikilinganishwa na mfumuko wa bei za bidhaa.
Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kundi kubwa la wananchi wakiwa katika hali ngumu, huku wakijenga hisia kwamba kundi dogo linanufaika kwa kuibia na kuhujumu uchumi wa nchi kwa kutumia madaraka ya umma.
Lazima watawala walioshika madaraka ya dola na watendaji wote wa ngazi tofauti katika mhimili yote ya dola ambayo inaendeshwa kwa kodi za umma, wajitambue, wajenge heshima ya ofisi za umma kwa kuhakikisha hazitumiki kinyume na ahadi ya 'Cheo ni Dhamana'!
Kwa maana kama hawa waliotuhumiwa na kuahidi kwenda mahakamani wangekuwa wamejengeka katika maadili ya uongozi na kutambua zile ahadi kumi za mwana TANU, basi tayari wangekuwa wamekwenda mahakamani.
Lakini masikini looh! nchi ina watu ambao wanaonekana kuwa wana 'system' lakini ni hawa ambao leo hii wanathibitisha kwamba walipinga Azimio la Arusha ndiyo wengine wanatuhumiwa kuitumia ofisi za umma kuhujumu uchumi wa nchi.
Umefika wakati, lazima tuwe na taifa la viongozi wa serikali ambao wakitaka kuhongwa watalia kwa kutoa machozi, taifa ambalo kila mtu katika nafasi yake atafanyakazi akijua anafanya kwa ajili ya nafsi yake.
Tubadili fikra na mtazamo kwamba, madaraka ya umma ni sehemu ya kuhujumu uchumi wa nchi kwa kujilimbikizia utajiri badala ya kutumikia nchi na kufuata maadili katika kusimamia dhamana hiyo.
Naamini haya ni mambo ambayo watuhumiwa hawa wa ufisadi waliotaka kwenda mahakamani walipaswa kukaa na kutafakari kwa kina, lakini hawakufanya au wanatumia unyonge wa Watanzania na kuona hakuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Hawa wameutangazia umma wa Watanzania kwamba watakwenda mahakamani kujisafisha na tuhuma za ufisadi, sasa wanapaswa kukumbuka 'Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Vitendo'.
Je, mbio na azma hii imeishia wapi, je wamebaini kwamba wakienda mahakamani mengi yataibuka na kuzidi kuumbuka?
Sasa kama ni hivi, basi waitishe tena mikutano na waandishi wa habari kama mwanzo, kisha wautangazie umma kwamba wameachana na mpango wao wa kwenda mahakamani na watoe sababu.
Hii si hiari yao ni lazima kwa maana mabosi wao ni wananchi ambao ndiyo wanaoendesha serikali kwa kulipa kodi ambazo pia zinawalipa wao mishahara.
Kwenda mahakamani au kutokwenda halikupaswa kuwa jambo la hiari, lakini wanaweza kufanya hivi kutokana na upole huo wa Watanzania.
Lakini ukweli ni kwamba, matukio kama haya yangekuwa katika nchi ambazo wananchi wamejenga utamaduni wa kupinga uchafu wa viongozi wa serikali kwa njia za maandamano na migomo, hawa tayari wangekuwa wameng'olewa katika nafasi hizo.
Leo hii hawa wanaringia udhaifu huu, lakini umma huu siku moja utalipuka, moto wake utachoma na kuwasambaratisha wote wanaoihujumu nchi.
Tanzania ya mwaka 1970 si kama ya leo, ya leo haiwezi kuwa kama ya kesho au kesho kutwa, mabadiliko yanakuja taratibu, fikra za utaifa na uzalendo zinazoambatana na ujasiri wa umma kufanya maamuzi, zinakuwa siku hadi siku.
Wapo vijana wenye fikra za kimapinduzi wanazidi kuamka, wako ndani na nje ya nchi hii, wanajua mbivu na mbichi, hawawezi kukubali kuona nchi inatafunwa.
Sasa ni vema watuhumiwa wa ufisadi ambao wameazimia kwenda mahakamani wakafanya hivyo wenyewe kama walivyoutangazia umma , kwani kutokufanya hivyo ni kuzidi kucheza na akili za Watanzania na kuichafua serikali, mbio zao zimeishia wapi?
Source: Gazeti la Mwananchi.
SteveD.