Mbio Za Urais Wa Zanzibar 2010: Kanisa Katoliki Laanza Kumnadi Waziri Khatibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio Za Urais Wa Zanzibar 2010: Kanisa Katoliki Laanza Kumnadi Waziri Khatibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 19, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  KIONGOZI wa Dini Padri Lucian Malamsha wa Kanisa Katoliki Zanzibar amemfananisha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano) Mohamme Seif Khatib na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Padri huyo amesema Khatib ndiye kiongozi hasa anayefuata muongozo na nyayo za baba wa taifa, Mwalimu Nyerere katika utumishi wake wa kulitumikia taifa la Tanzania.

  Tamko hilo amelitoa jana katika mkutano wa hadhara alipokuwa akihutubia wananchi katika hafla ya kukabidhi nguzo za umeme zinazotarajiwa kutumika kusambaza huduma hiyo katika vijiji vya wilaya ya kati katika Jimbo la Uzi Kisiwani Unguja.

  Padri Malamsha alisema Waziri Khatib ametoa mchango mkubwa katika kutumikia taifa la Tanzania na ni miongoni mwa viongozi wachache walioonesha uadilifu wa kujiepusha na vitendo vya ufisadi katika jamii na hasa wakati huu ambao viongozi wengi wamekubwa na kashfa hiyo.

  Alisema kwamba viongozi wengi wamekuwa wakitoa ahadi, lakini baadaye hushindwa kuzitekeleza, kitendo ambacho hakileti sura nzuri na kusema kitendo cha kukabidhi nguvu za umeme ni ukombozi mkubwa katika kuwasogezea maendeleo wananchi katika vijiji hivyo.

  Padri huyo alimsifia Waziri Khatib ambapo alisema ameanza kumfahamu miaka mingi tokea alipokuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM taifa na ni miongoni mwa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kulitumikia taifa na kudumisha muungano wa tanganyika na zanzibar.

  “Ndugu wananchi mliokusanyika hapa mnamuona mheshimiwa khatib hata umbo lake linafanana la Mwalimu Nyerere, amekuwa hanenepi kutokana na harakati nyingi alizonazo kutumikia wananchi”, alisema Padri huyo.

  Kiongozi huyo wa dini alisema hivi sasa Tanzania kuna viongozi wengi lakini ni wachache ambao wamekuwa wakifuata misingi ya baba wa taifa ya kuwa karibu na wananchi na kujua matatizo yao jamo ambalo limesababisha wananchi wengi kukosa imani na serikali yao kutokana na na tabia za viongozi hao.

  Aliema kwamba Waziri Khatib pamoja na kukabidhiwa wizara nzito ya muungano lakini ameweza kuiongoza kutokana na kufuata misingi ya uongozi ya baba wa taifa na kuweka mbele maslahi ya taifa tofauti na wenzake.

  “Kutokana na uwezo wake wa kudumisha Muungano ndio maana wananchi kutoka Bara leo hii wanaishi bila matatizo yoyote Zanzibar na wale wa Zanzibar wanaishi Bara kwa utulivu kabisa”, alisema Padri.

  Askofu huyo alisisitiza “Nakuombeni wananchi zingatieni ule msemo wa Kiswahili, Usiache mbachao kwa msala upitao na Zimwi likijualo halikuli likakwisha kwa hivyo wenyewe mna hiari yetu tena hapo”, alisema na kuibua shangwe za wananchi hao.

  Kwa upande wake akitoa shukurani zake kwa wananchi hao, Waziri Khatib amesema mradi huo wa umeme utasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo iwapo wananchi watatumia nishati hiyo kwa kubuni miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

  Alisema mradi huo utawasaidia wananchi wote bila ya kubagua kwani kitu kizuri ni kuishi kwa mashirikiano bila ya kujali itikadi za kisiasa wala kidini huku akiwataka wananchi hao kufahamu kwamba msingi mkuu wa taifa hili ukiwa ni usawa katika kupata haki.

  Katika hatua nyengine Waziri Khatib aliwataka wananchi kukamilika masharti ya sifa wajitokeza kujiandikisha katika zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura linaloendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.

  Pia aliwataka wafuasi wa CCM na CUF waache tafauti zao na washirikiane katika miradi ya maendeleo kwa vile maendeleo hayawezi kupatikana bila ya kuwepo mashirikiano ya pamoja ya wananchi katika maeneno husika.

  Waziri Khatib alikabidhi nguzo 100 za umeme na kukagua vituo vya afya katika vijiji vya Ghana, Mpapa ambayo imekuwa ikijengwa kutokana na mchango mkubwa wa viongozi wa jimbo hilo.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Naona Khatib "Msakatonge",kaanza mbio zake kwa mguu wa kushoto..a wrong move...nafikiri padri Malamsha anamfahamu tokea akiwa umoja wa vijana wa CCM, lakin ni Khatib...tunamjuwa zaidi kuliko yy Malamsha...si tu kuanzia umoja wa vijana bali hata namna ya kufika hapo na kupanda ngazi...kama Khatib anatafuta ushawishi wa kanisa kufanikisha malengo yake ya kisiasa, ni wazi kuwa anaielekeza CCM zanzibar...iwapo itamchagua kugombea...kushindwa kwa kishindo hata kama wataiba vipi...kumfananisha Khatib na Nyerere ni hatua ya kwanza ya kanisa katoliki kuelekea ya pili ya kumtangaza kuwa "chaguo la Mungu", sasa tumeona vipi waraka wa kanisa unavyoanza kufanya kazi yake. Ushauri wangu wa bure kwa Khatib "Msaka Tonge", siku zote rais wa zanzibar anatoka BLW...kama anataka historia ibadilike...aache kuendekeza siasa za kubebwa bebwa na SMT kupitia chama chao cha kanisa katoliki...wazanzibari are no longer fools like he thinks they are...
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mbona Waziri Khatib kaianza safari yake kwa namna ya kushangaza.....Sidhani kama Askofu Malamsha katumwa kumtambulisha Khatib kama nae yumo katika kinyang'anyiro cha Urais hapo Mwakani.Tuchukulie Maneno hayo Askofu kayazungumza tu bila kuwasiliana na Waziri,ambaye anafahamu fika kuhusishwa kwa kanisa katika kumtangaza ni kumchimbia kaburi.....Askofu akazidi kumdidimiza Khatib kwa kumfananisha na Mwalimu...Mwalimu sio maarufu maeneo mengi ya Unguja na Pemba.Askofu Malamsha kutoka Rombo anadai anamfahamu Mzee Khatib vizuri...Ninamshangaa sana, katika anaowahutubia wapo waliocheza na kwenda shule na Khatib sio Askofu (Malamsha) ambaye ni muhamiaji huko.

  Pamoja na Waziri Mohammed Seif Khatib kuna wana-ccm wengine kumi wanaonekana mara kwa mara Unguja/Pemba na kuzungumzwa kwamba wanajitayarisha kwa Uchaguzi huo wa Mwakani,Orodha ya WanaCCM wanaozungumzwa huko visiwani ni:

  1; Shamshi Vuai Nahodha - Waziri Kiongozi Zanzibar.
  2; Dr Ali Mohammed Sheni - Makamu wa Rais - Tanzania.
  3; Ali Abeid Karume - Balozi wa Tanzania Nchini Italia.
  4; Dr Hussein Ali Mwinyi - Waziri wa Ulinzi - Tanzania.
  5; Mohammed Aboud - Waziri wa Afrika Mashariki.
  6; Dr Mohammed Gharib Bilali - Waziri Kiongozi Mstaafu.
  7; (Balozi) Seif Idd - Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje - Tanzania
  8; Justice Hamid Mahmoud -Judge Mkuu Zanzibar.
  9; Ali Juma Shamhuna - Naibu Waziri Kiongozi Zanzibar.
  10;Haroun Ali Suleiman -Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,009
  Trophy Points: 280
  Junius,Mwawado,

  ..ukisoma habari hiyo utaona mahali wameandika kwamba wananchi walishangilia kauli za Askofu Malamsha. hiyo inadhihirisha kwamba Askofu alikuwa anzungumza ktk eneo ambalo Waziri Khatibu anakubalika.

  ..wakati umefika Watanzania tuache kutumbukiza Udini na siasa hata mahali pasipostahili.

  ..kitu cha msingi na umuhimu zaidi ni kwamba wananchi wa jimbo la Uzi wamepatiwa nguzo za umeme na Kanisa Katoliki.
   
 5. M

  MLEKWA Senior Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa tukubali ukweli kuwa Mohammed Seif Khatib hana base Zanzibar kama alivyo Makamo wa Urais wa Tanzania aligombea Ubunge Pemba na kuukosa kwa hiyo ukweli wenye base ya Urais wa Zanzibar ni hawa Hapa nawaweka kutokana na nguvu ya camp zao.

  1. DR Bilal power full camp inayoongozwa na wafanya biashara wale wale aliokuwa kwenye camp ya Komandoo, hii ni camp iliyo na upinzani na Karume Camp na inaonekana inataka kurudi kwa nguvu mpya kuingausha Karume Camp
  2. Shamsi Vuai Nahodha ( anategemea turufu ya Rais Karume )
  3. Shamhuna , anategemea nguvu ya kwao ila ukweli nafasi yake ni ndogo ni corrupt Leader
  4. Dr Shein ni poweful figure ikiwa ataamua kugombea kwani ni mtu pekee atakae weza kuwaweka CCM/CUF pamoja ila inaonekana bado ni mzito kutangaza jina lake na heshima aliyonayo kwenye Halamashauri kuu Tanzania bara huu ndio ukweli hata wazee wa Pemba wameenda kumuomba agombee kwa vile Miaka 40 ya Mapinduzi hakujawahi kuwa na RAIS MPEMBA.
  Ali Karume nafasi yake na DR Hussein Mwinyi watu wa Zanzibar hawataki tena kusikia watoto wa viongozi ndio wanakua warithi wa madaraka hii Amani Karume wengi wanaijutia huu ndio ukweli, Hussein Mwinyi ataweza labda baada ya Miaka kumi.

  Mohammed Aboud pia ni jina linaloingizwa kwenye list ya Urais wa Zanzibar ila na yeye hajulikani Zanzibar zaidi anategemea Kikwete Camp.

  Dr Omar Shajak ni Kijana pekee wa Kipemba ambae wasomi wengi wanamuona ndio anaweza kuonekana ni damu mpya ya kizazi kipya cha CCM na pia ana turufu ya kuonekana ni Mpemba pia ana umaarufu hasa kwa historia yake ya kutoka katika UMOJA WA VIJANA WA CCM na pia historia yake ya Wazazi wake ni Wana Afro Shirazi kindaki ndaki kina PILI Khamis wa Kengeja Pemba, ila hana makundi hili linaweza kuwa tatizo kwake.

  Mohammed Seif Khatib ni (gate Keeper) anaamini yeye ndio mlinzi wa muungano ila ukweli ni kuwa hakubaliki kabisa ZNZ na sasa hivi CCM itafanya makosa makubwa kumueka mgombea asieuzika kushindana na CHAMA CHA CUF kilichoota mizizi Zanzibar kwani mumeona na 1995/ 2000 /2005 ukweli kama kungekuwa na fair election ZanzibarSalmin/ Karume asingeuzika au kushinda ila ni faulo ndio inayoshinda uchaguzi , Jakaya Kikwete anahitaji kuweka Lagacy yake sio kama BEN kuuwacha mzozo wa kisiasa wa Zanzibar bila suluhisho ni makosa makubwa na hii ni nafasi muhimu kwake JK yoyote atakaepewa support ya Halamashauri kuu ya Bara lazima akubali ile nipe nikupe akubali kugawana madaraka na CUF kupunguza mgogoro wa Visiwani ndio apewe kura za Tanzania bara kwani ni aibu kwa Tanznaia kila siku kuambiwa Tanzania ni kisiwa cha amani lakini kila siku watu wanapigwa bakora Zanzibar nimeona Jina la JK kwenye hii blog kuwa huenda akawa ni nominee wa MOhammed Ibrahim Foundation wa kula dola milioni tano mwaka 2010 ila Zanzibar ndio itakayomkosesha kikwete nafasi hii see this blog.

  http://dirayetu.blogspot.com/2009/10/president-kikwete-will-be-nominee-for.html
   
 6. u

  under_age JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  misaada inayotolewa kwenye viriri vya siasa kwenye kipindi hiki cha karibu na uchaguzi huwa sina imani nayo, ikitolewa na askofu au imamu wa msikiti,it doesnt make any difference. wanatufanya sisi raia ni wapumbavu. wakitaka kura zao ndio wanakuja na vijinguzo vya umeme. natamani taifa letu lingekuwa na ujasiri wa kukataa misaada kutoka kwa wanasiasa katika kipindi cha kampeni.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kumbuka hapo ni jimboni kwake Khatib..yaani Mkuu...ni sawa na ww mtu mbali aje akutambulishe mwanao wa kumzaa, utamuonaje, si anawazimu tu. Nasisitiza Khatib kaanzia mguu wa kushoto...na mbio zake ndo zimeisha hapo watu wa zanzibar hawana dogo na keshawatibua hapo, hasa mambo yao ukianza kuingiza imani nyingine ya dini...(sileti udini nasema hali halisi ya visiwani)
   
 8. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kazi ya siasa na kudanganya wananchi sasa ndio imeanza kupamba moto
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,009
  Trophy Points: 280
  Junius,

  ..naona kama haya mambo ya dini ni yako wewe binafsi.

  ..wananchi wa jimboni kwa Khatib ambako Askofu alihutubia hawakuonyesha kuwa na tatizo na maneno yaliyotamkwa na wala imani ya Askofu Malamsha.

  ..tena imeripotiwa kabisa kwamba wananchi walishangilia hotuba ya Askofu Malamsha.

  ..jambo la msingi na la kutiliwa mkazo siyo hotuba au imani ya Askofu Malamsha, bali ni suala la maendeleo ambapo wananchi wamepatiwa msaada wa nguzo za umeme.

  ..wakati mwingine nadhani huu udini ni mambo ya kujiendekeza tu.
   
 10. a

  akili Member

  #10
  Oct 19, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanshafulia hivyo. Wazanzibari safari hii hawawezi kamwe kumchagua kiongozi anayepiga vita Uislamu na anayekuwa kafiri kushinda makafiri. Hamna hilo. Sahauni kabisa nyie manasara!!!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kanisa katoliki linataka kumpigia debe Khatibu kama mwandishi unavyosema. Maoni ya Padri ni maoni yake binafsi, kwa maana hiyo basi kila mtu ataamua yale anayofikiri ni sahihi kufanya kwake.Kama wangelitoa waraka ningeelewa kuwa huo ni msimamo wa kanisa katoliki.
   
 12. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mi naona hawa viongozi we2 wa dini wakae mbali sana na Siasa na Wanasiasa kwani hivi ni vi2 viwili ambavyo ukivichanga tu Amani itavutugiga mara moja.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kila Padre au Askofu sio MSEMAJI wa Kanisa Katoliki. Tunapotoshana tu hapa.
   
 14. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280

  tunasubiri tuambiwe ni chaguo la mungu ,

  labda wahyi haujafika bado ( astaghfirullah )
   
 15. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  Hakika Huyu Padre amechemsha. Kwanza Zanzibar hatumtaki mtu kama Nyerere. Aliyoyafanya huku bara tunaona matokeo yake hivi sasa.Umaskini na udini umetawala sasa huyu anataka kuleta ukatoliki huko Znz.

  Kifupi Khatib hana bao Zanzibar. Hata mwendawazimu hamchagui na hata wakatoliki wakimchagua hapati hata 2% ndani ya CCM.
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  hapa hakuna kitu wote wasindikizaji tu.

  hapo namuona labda Dr Mohd Ghalib Bilal anaweza kufurukuta. wengine wote bomu
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli Zanzibar mmewahi kuwa na uchaguzi wenu halisi wa Rais?
   
 18. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyu Padri Malamsha huwa anatumwa na nani? Nakumbuka katika uchaguzi wa 2005 aliwahi kutoa hotuba akidai kuwa iwapo CCM itashindwa Zanzibar maisha ya wakristo wa huko yatakuwa hatarini. Akaomba serikali ijitahidi jambo kama hilo (la kushindwa CCM) lisitokee!
   
 19. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Aliyeandika story hii hajui jinsi Kanisa katoliki linavyofanya kazi. Kanisa lina chombo chake yaani TEC na matamko rasmi yote upitia katika chombo hiki. Akikurupuka Padri mmoja kama alivyofanya Padri Mapunda 2005 kwa kusema "J.K ni chaguo la Mungu" haina maana kwamba kanisa katoliki limesema hivyo. Na hili la Zanzibar ni hivyo hivyo. Mwandishi alitaka kuuza story kwa kuliingiza kanisa katika ushabiki wa kisiasa Zanzibar.
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ati Kanisa Katoliki.........huko ndani...Padre Malamsha???:confused:
   
Loading...