Elections 2010 Mbio Za Urais: Prof. Lipumba Anakuja, Na Chupa Ya Maji Mkononi!

Ha ha haaa! Maggid bwana!

Sasa unataka kutuambia nini? Kampeni za sasa za Lipumba naziona zaidi kama za kuaga katika ulingo wa siasa kuliko kuomba kura ili ashinde.

Acheni kumpigia kampeni JK kwa mlango wa nyuma. Mwaka huu hatudanganyiki.
 
Mjengwa unazigawanya kura za Kikwete maana masheik waliokacha shule walisema, "hawa wote ni wenzetu na ni bora tumpigie yule mwenye uhakika zaidi!! tafakari! mwenzenu kivipi?"

MH! NADHANI HII JM ITAKUFA BAADA YA OCT 31-KAMA HIZI NDIYO STYLE ZENYEWE. MASHEIKHE WAMEKACHA SHULE? ARE U CRAZY, WAPI YAMEANZIA HAYA! WADHANI DR. WA ROMA ANAWEZA KUMFIKIA JAPO STUDENT WA MADINA? KAMA NCHI HAINA MAENDELEO SI NYIE MA-DR WA ROMA NDIYO MNAOSABABISHA HAYA, NYIE NDIYO MA-DIRECTORS, KAMISHNAS, PSs, MINISTERS, DG, MD, CEOs-HEBU TUAMBIENI MNATAKA RAIS ASHIKE VYEO VYOTE HIVI-CHAPENI KAZI JAMANI, ACHENI KUTUMIA MUDA NA KOMPYUTA ZA SERIKALI KUBISHANA UJUBA TU HUMU HALI YA KUWA MAISHA YA WATANZANIA MNAYAFISIDI NYIE!
 
Mjengwa.
umejenga hoja kwa Lipumba na jamaa zake lakini umeacha namna walivyoshiriki kuibaka demokrasia ktk uchaguzi mkuu wa CUF. Pia nashangaa unavyompromoti mtu ambaye miaka yooote anagombea tu wala hana dalili ya kushinda. Pia tafakari kuhusu yeye kama Lipumba angelikuwa fair kwa kukubali safari hii kuiunga mkono CHADEMA maana wao walimuunga mkono past chaguzis.

Pia historia ya CUF imejaa uzandiki na hila. naamini wakumbuka walichomfanya muasisi wa chama hicho na mpaka wakamtoa nje kabisa. je hayo siyo historia ya kumpima Lipumba? Ktk mawazo yangu neno LIPUMBA maana yake ni Pumba kuuuubwa isiyo na maana yeyote
hapa umenena mkuu nilisahau hii point hata mimi chaguzi mbili nimepigia CUF, 2000 na 2005!
 
Lipumba ni mtu mwenye akili sana na anajua mambo ya uchumi kiundani kuliko wagombea wengine wote. Vile vile ni mtu mwungwana sana. Ingawa mwaka 1995 kura yangu nilimpa mrema, nilijishauri mara mbili mbili kati ya ushujaa wa Mrema na akili za Lipumba ni kipi kipata kura yangu. Bahati mbaya ushujaa wa Mrema ukaonekana kuwa ni wa muhimu sana kwangu kutokana na system mbovu iliyojengeka nchini, ambayo inahitaji kubomolewa na mtu mwenye ushujaa. Mwaka 2000 na 2005 sikupiga kura, ila mwaka huu nitapiga tena. Sijaona kama Lipumba anao huo ushujaa wa kupambana na mtu au kikundi chochote bila kuogopa; kufanya mabadiliko nchini ni jambo linalohitaji ushujaa sana zaidi ya akili kwani kuna resistance kubwa sana kutoka kwa watu waliozowea status quo.
 
acha kashfa za kijinga mbwiga wewe! nani alokwambia mashekh wamekacha shule?? soma historia na uache kuropoka,mlofilisika kisiasa mtatuingiza katika udini badala ya kutuambia mtatufanyia nini watz!! hufai
 
tatizo la wachaga wa chadema,hamuoni namna chaga yenu ilivyoilawiti demokrasia kwa kumtoa ouf of competition mzitto kabwe mbele ya mbowe, na ni wangapi walioikimbia chadema kwa uzandiki wa ukabila na ufisadi wa ruzuku ya chama na mpaka wengine mkawafyeka kama akina chacha wangwe ( kamanda wa kweli???) tazama ukweli katika rangize halisi,ondoeni ukampuni wa chaga kiwe chama cha siasa NA MUACHE UDINI WENU NA KAMPENI ZA MAKANISANI NDO MJE KUOMBA KULA KAMA TUTAWAPA
 
Huyu ni mpiganaji wa kweli,tatizo la hawa chaga development manifesto ni kelele tu katika vijiwe vya kahawa kama hapa geita ambapo padre wao alikuja jana na badala ya kutueleza atatufanyia nini watanzania,yeye ametua na kahelcopter kake hapa kutueleza ratiba zake za mikutano yake ya tabora na bukombe!! Sio ukichaa huu???yani kampeni zinatakiwa kufanyikia tabora na bukombe halafu ratiba unakuja kuitangazia geita!!!! Hahahaaaaaaaaaa
 
tatizo la wachaga wa chadema,hamuoni namna chaga yenu ilivyoilawiti demokrasia kwa kumtoa ouf of competition mzitto kabwe mbele ya mbowe, na ni wangapi walioikimbia chadema kwa uzandiki wa ukabila na ufisadi wa ruzuku ya chama na mpaka wengine mkawafyeka kama akina chacha wangwe ( kamanda wa kweli???) tazama ukweli katika rangize halisi,ondoeni ukampuni wa chaga kiwe chama cha siasa NA MUACHE UDINI WENU NA KAMPENI ZA MAKANISANI NDO MJE KUOMBA KULA KAMA TUTAWAPA

Ndugu sio lazima ukatoa maoni hapa

inakera sasa kwani mkishaona mnaelemewa mnatafuta wakumlaumu,,kwani Chadema kina Wachagga wangapi? huwezi jenga hoja bila kuwahusisha hao wachagga,,Endelezeni hizo siasa zenu za uendawazimu kwa kuendekeza Njaa tu
 
Na Maggid Mjengwa,

MBIO za Urais zimeshika kasi. Media imekazana kuandika habari za JK na Slaa. Habari za CCM na CHADEMA. Kuna aliye kwenye mbio wanamsahau, kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Ni Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF).
Katika wote wanaoshiriki mbio za Urais, Prof. Lipumba ndio mwenye uzoefu zaidi wa njia wanayokimbilia. Alianza mwaka 1995, ni kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi.
Alishiriki mdahalo wa kwanza wa wagombea urais. Ingawa, aliibuka wa pili kwenye mdahalo ule uliomwacha Ben Mkapa akiongoza na Mrema akiambulia nafasi ya tatu na John Cheyo akikamata mkia, bado Mashirika ya habari ya kigeni yalimpa Prof. Lipumba alama za juu zaidi.
Lipumba ni mpiganaji mahiri. Mwaka 1995 aliingia kwenye mbio za Urais kama ' Profesa'. Hilo lilikuwa kosa, akalirudia tena mwaka 2000. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Profesa Ibrahim Lipumba alionekana zaidi kama ' Ibrahim Lipumba'. Profesa aliamua kushuka chini.
Nakumbuka kukutana nae kwa mara ya kwanza mwezi kama huu, Oktoba 2005. Ni pale Isimila Hotel, Iringa. Ni Hotel ya kawaida kabisa. Rafiki yangu Saed Kubenea alikuwa kwenye msafara wa Lipumba na ndiye aliyefanya maandalizi ya mimi kukutana na Lipumba.
Ilikuwa siku ya Alhamisi, nilifika pale Isimila Hotel kunako saa tatu asubuhi. Aliponiona, Profesa Lipumba alinijia akiwa mwingi wa tabasamu. " Kumbe, ndiye wewe Maggid!" Alitamka huku akionyesha furaha. Mkono wa kushoto alikamata jarida la Rai na chupa ya ‘Maji Afrika'. Saed Kubenea alisimama kando kupisha mazungumzo yetu.
Nilimwona Profesa Lipumba kuwa ni mtu wa kawaida sana. Kuna wakati kwenye mazungumzo yetu tukiwa tumesimama alikuwa akipukuta vumbi kwenye suruali yake kwa kutumia gazeti la Rai. Lipumba anaongea kwa mpangilio na kwa kutulia. Kushiriki kwake katika uchaguzi wa 1995 na 2000 kumempa uzoefu zaidi katika kinyang'anyiro hiki. Lipumba ana uwezo na kipaji cha kufafanua mambo magumu yakaeleweka kwa mtu wa kawaida. Kuna wakati nilimsikia akitoa mfano wa ajira elfu moja zenye uhakika kwa vijana zinavyoweza kuathiri maisha ya mama mwuza vitumbua. Profesa Lipumba alitamka; " Ndugu zangu, bila ya vijana hawa kuwa na ajira na kipato , mama huyu atashinda na vitumbua vyake vikimtazama !."
Hakika, Lipumba ana uwezo pia wa kutengeneza sentesi fupi na zenye kishindo; Msikilize anaposema; "Wananchi nikopesheni kura zenu, nitawalipa maendeleo!" Hizi ni baadhi tu ya nguvu za Ibrahimu Lipumba katika rethorik, sanaa ya kuzungumza.

Ndio, Profesa Lipumba hata hii leo , bado yumo kwenye mbio za kusaka kura kwa wapiga kura wapatao milioni 19. Na Profesa Lipumba safari hii anaonekana kutumia mbinu za kijeshi zaidi. Anakwenda kwanza kule ambapo anaamini kuna matumaini ya kupata ushindi, matumaini ya kuvuna kura.
Itakumbukwa, Lipumba alianza kampeni zake kwenye ‘ngome' ya CUF. Ni mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara. Huko Profesa ‘alipiga kambi'. Kama safari hii atatoka patupu hata kwenye ngome yake, basi, Profesa atalazimika kutafakari upya kama aendelee kuwapo kwenye uongozi wa juu wa CUF au awapishe wengine.
Baada ya kule Kusini, tulimwona Profesa akichagua maeneo ya kwenda. Na kila alikokwenda kulikuwa ni kule ambako CUF imeonekana kuungwa mkono.
Staili yake ya kampeni imebadilika pia. Profesa Lipumba wa leo, anavutia zaidi wasikilizaji na watazamaji. Lipumba haonekani sana juu majukwaani. Ameshuka chini, anaongea na wapiga kura akiwa karibu nao sana. Kila mahali anapofika, anaunganisha masuala makubwa na yale ya mahali hapo. Ameacha staili ya kutumia muda mwingi kukishutumu Chama Cha Mapinduzi. Profesa anasisitiza zaidi nini atakifanya, yeye na chama chake. Kile ambacho CCM wameshindwa kukifanya.
Kabla ya mikutano ya hadhara, Profesa anafanya jitihada za kuikaribia jamii ya mahali hapo. Mathalan, atakwenda hospitali kuwaona majeruhi wa vurugu za vijana wa CCM na CHADEMA. ( Mara) . Akiwa hospitalini ataongea kuhusu umuhimu wa kushindana kwa hoja na si kupigana. Si profesa yule wa CUF ya ' Jino kwa Jino'. Na hatusikii siku hizi habari za ' Blue Guards'. Kama kutakuwa na habari za kontena lililosheheni visu kukamatwa na CUF ndio wakawa watuhumiwa, basi, habari hiyo itatiliwa mashaka na wengi.

Profesa Lipumba atakwenda sokoni . Huko ataongea na wananchi, atauliza bei ya vyakula. Kule Musoma tukamwona Profesa akipima nguo kwa fundi cherehani, alitaka fundi huyo amshonee suti yake. Pale Bunda Lipumba akamtembelea nyumbani kwake Mzee Raphael, mwanachama wa CUF wa miaka mingi. Kule Geita tumemwona Lipumba akizungumza na wachimbaji madini wadogowadogo akiwa kwenye machimbo hayo.

Ndio, tumemwona Lipumba akibeba mawe kuweka chini ya tairi na hata kusukuma gari kule Kondoa . Ni wakati msafara wake ulipokwama njiani. Tumemwona Lipumba akishiriki shughuli ya mazishi kule Mafia na Kagera. Kwamba kila anapokwenda kukampeni, Profesa Lipumba anatafuta habari kuhusiana na mahali hapo, ikiwamo na habari mbaya kama misiba. Kwenye misiba kuna wapiga kura.

Hii nayo ni staili ya kampeni anayoionyesha Lipumba katika uchaguzi huu. Kushuka chini kwa watu. Mgombea usijikite tu kwenye kukusanya watu, unapaswa pia kuonekana iliko mikusanyiko ya watu. Nimepata kumwambia raia mmoja wa kigeni aliyeshangazwa na ratiba ya JK Mkoani Iringa, ratiba ambayo ilikuwa nyuma ya wakati kwa saa kadhaa. Nilimwambia; " In Africa, Presidential is Communal". Kwamba ' Afrika Urais ni jamii'. Mgombea urais ukiacha kusimama njiani kuongea na wanakijiji wanaokuomba ufanye hivyo. Sababu? Eti unawahi ratiba, basi, na kura zao kwako umeziacha pale pale.

Tukirudi kwa Profesa Lipumba, bila shaka, Lipumba anajivunia pia nguvu za chama chake, CUF. Chama hiki kiliundwa Mei 28, 1992. Ni chimbuko la kuunganishwa kwa Chama cha kutetea haki za Wananchi (Civic Movement) kwa upande wa bara na chama cha KAMAHURU cha Zanzibar.
CUF inatokana na vuguvugu la mageuzi nchini. Ingawa NCCR-mageuzi kilikuwa ni cha kwanza cha upinzani, CUF kilikuwa chama cha pili kusajiliwa katika mfumo wa vyama vingi baada ya CCM. Hii ilitokana na sura yake ya muungano kuonekana dhahiri. Hii ni moja ya nguvu kubwa za CUF. Hakuna anayejisumbua kuweka hadharani, ukweli kuwa, kwa sasa, CUF ni chama pekee cha siasa, chenye uhakika wa kuwa na wawakilishi bungeni kutoka Unguja, Pemba na Bara.
Udhaifu wa CUF: Kama ilivyo kwa vyama vingine vya upinzani kama CHADEMA, bado hakijawafikia wapiga kura wengi vijijini, hususan bara. CUF ni chama pekee cha upinzani kilichokuwa na wabunge wengi katika bunge lililopita. Hivyo basi, kilipata ruzuku zaidi. Bado ni ajabu kuwa CUF imeshindwa kutumia ruzuku hizo kujitangaza na kujiimarisha zaidi bara.
Hata hivyo, nguvu za CUF Zanzibar ni fursa kwa chama hicho kujiimarisha bara. Idadi kubwa ya wabunge wa CUF inaamanisha kiasi kikubwa cha ruzuku watachokipata. Ruzuku ikitumiwa vizuri inaweza kukikuza chama hata bara.
Tishio. Tuhuma za kuwa CUF kinakumbatia uislamu ni tishio kwa chama hicho. CUF imegubikwa na wingu la mashaka ya baadhi ya Watanzania juu ya chama hicho na uislamu. Kimsingi tuhuma hizi dhidi ya CUF ni propaganda za kisiasa kutoka kwa wapinzani wa chama hicho. Hazina ukweli. Wanaokipiga vita chama hicho, hususan bara, wamefaulu kuipaka CUF rangi ya udini. Ni jukumu la CUF wakiongozwa na Mwenyekiti wao ( Taifa) , Profesa Lipumba, kujitetea na kujibu hoja hizi kwa vitendo, hivyo wakaeleweka na wapiga.


mjengwa
Duh, Kumbe Lipumba anafaa sana kufungua NGO yake ya Usamalia, siasa za Bongo haziwezi..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom