Mbio za uongozi CCM: Sumaye amuengua Nagu, Mama Salma Hana mpinzani Lindi, UWT Dar moto......

Jana nimesoma magazeti mawili yamenifurahisha sana
sana labda kabla ya kuendelea nauliza hii nec ni nini hasa...naona according to magazeti ya jana
nahisi kuna ukoo fulani uko ndani ya nec...

Mtanzania
salma kikwete apita lindi nec bila kupingwa

mwananchi

riziwan kikwete apita bagamoyo bila kupingwa nec:

sasa hii ndio ilionimaliza kabisa nikumalizie akitangaza matokeo ya bagamoyo
mwenyekiti wa wa wilaya ya ccm bagamoyo mh "yussuf kikwete"" uwiiiiiiii
alitangaza mshindi ni riziwan kikwete baada ya aliekuwa akishindana nae kujitoa

nasubiri ukoo wa kawawa, na wengineo naona uko ndani kuna mambo mazuri sio hivi hivi
aiwezekani baba mama mtoto wanganganie sehemu moja nahisi kaama kuna viti maalum
sitoshangaa kusikia yule craizy wetu m...kikwete nae amechaguliw akuingia kama vit maaalum
 
These guys hawajifunzi kutoka kwa rafiki zao ambao koo zao zote zimengamia:

Hosni mubarak

sadam husein

Muamar Gadaf.

Pole yao
 
Sasa kama watanzania wote wako CHADEMA.Waliobaki ni ni viongozi wao na Familia zao.unategemea viongozi watawatoa wapi? lazima itakuwa humohumo wajomba, wakwe, mashemeji mahaouse girl, mkaza mjomba, watoto wakufikia na shehe wa ukoo umo umo.Chaajabu nashangaa kuna watu wachache wapo kama mazuzu na wamebaki ccm na hawajashtuka wanafata mkumbo tuu.
 
Sasa kama watanzania wote wako CHADEMA.Waliobaki ni ni viongozi wao na Familia zao.unategemea viongozi watawatoa wapi? lazima itakuwa humohumo wajomba, wakwe, mashemeji mahaouse girl, mkaza mjomba, watoto wakufikia na shehe wa ukoo umo umo.Chaajabu nashangaa kuna watu wachache wapo kama mazuzu na wamebaki ccm na hawajashtuka wanafata mkumbo tuu.
 
CCM imekuwa na tabia ya kukishutumu Chadema kwamba ni chama cha ukoo. Lakini katika hili, bila shaka CCM imeizidi Chadema, hasa katika awamu ya nne. Tumeona jinsi gani watoto wa wakubwa wanapewa vyeo serikalini, chama, na taasisi za umma. Lakini hii ya mtoto wa Rais, Mke wa Rais wa nchi kuwa wajumbe wa chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya Chama na Serikali yake NEC – ni kuvunja rekodi. Ridhiwani kapita NEC Bagamoyo, na Mama Salma kapita NEC Lindi, na wote bila ya kupingwa. Hapa demokrasia ilikandamizwa, na tulidhania utaratibu mpya wa kuchagua wajumbe wa NEC ungeboresha demokrasia ndani ya chama kumbe ni mbinu za watawala kupeana madaraka kama njugu.

Haiingii akilini eti Baba ni Mwenyekiti wa CCM, hivyo mwenyekiti wa vikao vya NEC, Mke mjumbe wa kikao chenye maamuz ya juu kabisa juu ya mustakabali wa nchi, mtoto mjumbe wa kikao vile vile. Nadhani kwa kituko hiki, Chadema haina haja tena ya kujibishana na CCM kuhusu chama kuwa cha ukoo. Asante CCM kwa kuzidi kujimaliza yenyewe kwa mwendo wa konokono.

 
Hiyo ndiyo demokrasia. Viopngozi wanapatikana kwa uchaguzi unaoheshimu katiba ya chama. Watu hawabaguliwi kwa majina ya baba zao.
By the way, wangeshindwa pia kungekuwa na headings za kukejeli. Ya moto inauma ya baridi inauma.
 
siamini kwamba ni sawasawa kwa mke wa raisi na mwenyekiti wa chama kujiingiza kwenye siasa. Kama mke wa raisi ni kiongozi wa juu katika utawala wa nchi. Wajibu wake ni kumsuport raisi na mwenyekiti. Kitendo chake ni sawa na mkuu wa mkoa kugombea udiwani wa kata anayoishi.

usafi na uchafu na udhaifu wa salma niulizeni mimi niliekaa nae pale mnarani kwa babu kushoto(marehemu moledina) na pia nikasoma nae liseco kisha nachingwea ttc namjua hasa! Hawezi kukosa mpinzani lakini loo!! Kweli pesa zinavunja milima.
 
Mke wa Rais, Salma Kikwete amerudisha fomu ya kuwania ujumbe wa Nec Taifa kupitia Wilaya ya Lindi Mjini.
Katibu wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini Mohamed Kateva, alisema jana kwamba Salma ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo katika wilaya yake.


Kateva alisema mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Agosti 28, mwaka huu na mpaka tarehe hiyo hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Hivi Mwenyekiti wa vikao vya NEC ni nani? Huko kwenye vikao watatizamanaje na M/kiti?
 
Jamani tulikuwa na Rais Nyerere, akaja Mkapa wote walitulia na kuhesimu Ikulu. Watoto wao wanaishi maisha ya kawaida sana. Ila nashangaa huyu rais Kikwete. Anatutawala kibabe na kihimla. Jakaya Kikwete anatumia vyombo vya dola kuikandamiza nchi. Raia wanauwawa bila sababu maalum.

Polisi wake wamegeuka kuwa majambazi, wanapora mali za raia, bandarini na hata kwenye majumba yao.Wanateka watu, wanawabambikizia kesi, wanaomba rushwa mchana. Kikwete ameamua kukaa kimya Polisi chini ya uongozi wa shemeji yake Said Mwema, wakiendeleza haya maovu. Mbaya zaidi Familia yake nzima inashikilia madaraka kwa mwendo wa kutisha. Haya siyo majungu ni kweli. Oneni wanavyojigawia vyeo

Mwenyekiti CCM: Jakaya Mrisho Kikwete (Pita Bila Kupingwa)
Mjumbe CCM-NEC: Salma Kikwete (Pita Bila Kpingwa)
Mjumbe CCM-NEC: Ridhiwani Kikwete (Pita Bila Kupingwa)
Mwenyekiti Vijana Chipukizi CCM: Khalfani Kikwete (Pita Bila Kupingwa)
Kamanda CCM, IT-Operesheni: Miraji Kikwete (pita Bila kupingwa)
Katibu Mkuu CCM, Yusuf Makamba (Mstaafu aliyepitisha tochi Kwa Manaye)
Naibu Waziri Mjumbe CCM-NEC: January Makamba (Pita Bila Kupingwa)
Mkuu Wa Polisi-CCM : Said Mwema (Shemeji Yake)
 
Hilo ndo tatizo la kutumia kichwa kufugia nywele.Mtu Kama anauwezo wa kugombea asifanye hivyo kwa sababu Baba yake Rais wa nchi Kweli uwezo wako ndipo ulipofikia hapo.Ndesamburo mbunge,Lucy owenya mtoto wake nae mbunge,Grace kiwelu mkwe wake nae mbunge wewe huoni hiyo.Usije ukawaza kupata cheo chochote kwa akili ulizokuwa nazo am out.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom