Mbio za uongozi CCM: Sumaye amuengua Nagu, Mama Salma Hana mpinzani Lindi, UWT Dar moto...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za uongozi CCM: Sumaye amuengua Nagu, Mama Salma Hana mpinzani Lindi, UWT Dar moto......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 5, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Wakuu hebu jisomeeni muone CCM walivyoanza kuparangana wenyewe kwa wenyewe.

  Waandishi Wetu

  MBIO za uchaguzi ndani ya CCM zimefikia patamu, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk Mary Nagu kuenguliwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hanang', huku Mke wa Rais, Salma Kikwete akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo Lindi Mjini.

  Mkoani Dar es Salaam, mbio hizo zimeonekana kuwaweka pabaya Mwenyekiti wa UWT wa mkoa huo Zarina Madabida na Katibu wake, Tatu Maliaga baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa, John Guninita kueleza kuwa viongozi hao watafikishwa kwenye kamati ya maadili kueleza kwa nini wamesitisha uchaguzi wilayani Kinondoni.

  Habari kutoka Hanang' zimeeleza kuwa Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya hiyo imemwengua Dk Nagu na kuwabakiza wagombe wawili, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Leonsi Marmo.

  Taarifa kutoka kwenye kikao hicho kilichofanyika juzi katika Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo na kuhudhuriwa na wajumbe 12 zimeeleza kuwa Dk Nagu ameenguliwa kutokana na maelezo kuwa kanuni hazimruhusu kugombea.
  Chanzo cha habari kimeeleza kuwa kanuni iliyomwondoa Dk Nagu kwenye kinyang’anyiro hicho ni ile inayowataka viongozi wenye kazi za kila siku; ubunge na uwaziri kutogombea.

  Imeelezwa kuwa jitihada za wajumbe watano waliojipambanua katika kikao hicho kumtetea Dk Nagu ziligonga mwamba, baada ya wenzao saba kuunga mkono uamuzi huo.

  Kuenguliwa kwa Dk Nagu kunatokana na sababu za kuwa na kazi za muda wote kumeibua hofu kuhusu hatima ya viongozi wengine waliochukua fomu ambao kwa mujibu wa kanuni iliyomwondoa Dk Nagu nao hawakupaswa kugombea.

  Hao ni pamoja na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Emmanuel Nchimbi.

  Wengine ni Wabunge Deo Filikunjombe (Ludewa), Mussa Azzan Zungu (Ilala), Dk Hamis Kigwangalla (Nzega) na Andrew Chenge (Bariadi Magharibi).

  Salma akosa mpinzani Lindi

  Katika hatua nyingine Mke wa Rais, Salma Kikwete amerudisha fomu ya kuwania ujumbe wa Nec Taifa kupitia Wilaya ya Lindi Mjini.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini Mohamed Kateva, alisema jana kwamba Salma ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo katika wilaya yake.

  Kateva alisema mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Agosti 28, mwaka huu na mpaka tarehe hiyo hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo.

  Madabida kiti moto

  Katika Mkoa wa Dar es Salaam, Madabiba na Maliaga watahojiwa kwa kukiuka uamuzi ya Halmashauri Kuu ya Mkoa.
  Viongozi hao wanadaiwa kusimamisha uchaguzi wa UWT Wilaya ya Kinondoni ambao ulipangwa kufanyika Agosti 31, mwaka huu.
  Guninita alisema jana kuwa kikao hicho cha Nec mkoa kiliagiza uchaguzi wa jumuiya zote ufanyike kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 2, mwaka huu lakini UWT Wilaya ya Kinondoni haikufanya uchaguzi huo.

  Alisema katika kikao chake cha Agosti 29, mwaka huu Nec Mkoa kilipitisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika wilaya zote tatu na kuagiza uchaguzi ufanyike.

  “Mwenyekiti wa UWT na katibu wake kwa sababu zao binafsi walisimamisha uchaguzi na kwa mujibu wa katiba yetu hili ni kosa,” alisema Guninita.

  Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo Madabida alisema: “Nipo kikaoni. Lakini ndani ya chama chetu cha CCM hakuna mtu anayeweza kuusimamisha uchaguzi peke yake.”

  MY Take: Wabunge wengine wote kuenguliwa kama Nagu????????????
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Mke wa Rais, Salma Kikwete amerudisha fomu ya kuwania ujumbe wa Nec Taifa kupitia Wilaya ya Lindi Mjini.
  Katibu wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini Mohamed Kateva, alisema jana kwamba Salma ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo katika wilaya yake.


  Kateva alisema mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Agosti 28, mwaka huu na mpaka tarehe hiyo hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo.
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  wabunge wengine wasipoenguliwa pia kuwania ujumbe NEC mawilayani na uenyekiti wa mikoa kwa walioomba, nitaamini Sumaye kaanza rafu za urais 2015
   
 4. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Salma Kikwete hajakosa mpinzani sema watu ima wamehongwa au wameogopa ikulu. Salma ana nini cha mno zaidi ya kuwa mke wa rais kuweza kuwazidi wenzake? Ana elimu gani au usafi upi vya kupigiwa mfano kuwashinda wengine? Kwa vile CCM ni chama cha kifalme ambapo ufalme wa sasa ni wa Kikwete, Salma lazima apite. Hata kama Salma angempendekeza mbwa wake angeshinda kutokana na tabia ya woga na kujipendekeza vya wana CCM. Mara hii mmesahau zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM ambazo Nyerere alizikosoa?Huu ni ushahidi kuwa CCM haiko kwa ajili ya wananchi bali kikundi kidogo cha walaji wenye madaraka na tamaa ya madaraka. Ningekuwa Jakaya nisingemruhusu first lady kujiingiza kwenye siasa zisizo saizi yake. Ila tamaa haina macho wala hisia zaidi ya majuto.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,068
  Trophy Points: 280
  haya bwana, ndo mambo ya magamba hayo
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hizo ni taratibu za kawaida ndani ya chama. Hakuna mwenye hati miliki ya uongozi.
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  maneno yako makali lakini yana ukweli sana tu
   
 8. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Si kwamba Salma amekosa mpinzani-wanaopaswa kumpinga wameogopa ikulu. Zaidi ya kuwa mke wa rais Salma ana sifa gani ya kukosa mpinzani? Ana elimu au ujuzi gani? Kwa vile CCM ni chama cha kifalme lazima mke au mwana wa mfalme apite. Hii inachangiwa na tabia ya woga na kujipendekeza vya CCM. Ningekuwa Jakaya nisingemruhusu first lady kujiingiza kwenye siasa za aibu ambazo hazilingani na hadhi yake. Kwa vile tamaa haina macho wala mawazo zaidi ya majuto hili limewekekana hata kama ni aibu tupu. Lini atafanya kazi za umma na za chama? Anyway, kwa vile siku za CCM zimekwisha, acha watuonyesha ubovu na uovu wao zaidi.
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Bujibuji mie nahisi kuna namna Hanang sio bure
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sumaye ni bora kuliko Nagu ambaye alishindwa hata kujitetea juu ya tuhuma za kughushi udaktari. Kwa vile yote ni magamba hakuna cha maana zaidi ya kuomba wazidi kumalizana ili ukombozi uwadie.
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  you are talking! Freedom is coming tomorrow
   
 12. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Siamini kwamba ni sawasawa kwa mke wa Raisi na Mwenyekiti wa chama kujiingiza kwenye siasa. Kama mke wa Raisi ni kiongozi wa juu katika utawala wa nchi. Wajibu wake ni KUMSUPORT Raisi na mwenyekiti. Kitendo chake ni sawa na Mkuu wa mkoa kugombea udiwani wa kata anayoishi.
   
 13. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii kanuni inawabana mawaziri/naibu mawaziri na wakuu wa mikoa/wilaya ... wabunge ni ruksa kugombea.
   
 14. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ama kweli hiki chama cha magamba sasa ni cha kifalme. Nasikia huko Pwani rizi1 nae amepita bila kupingwa. Watanzania tunaona yote haya. Fainali 2015.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  ....Wakibadilishe jina tu na kukiita chama cha vikwete. Ana wadhifa mkubwa kama first lady lakini haukumtosha mpaka naye ajiingize kwenye siasa!!! Tamaa hizi mbaya sana!!!
   
 16. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Masultani hao !
   
 17. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Huyu mama na siasa wapi na wapi? Kuwa mke wa mwanasiasa hakumfanyi mtu kugeuka mwanasiasa. Nani amesahau alivyokuwa anatetemeka akisoma risala zake siku za mwanzo? JK aking'oka na yeye kwisha.
   
 18. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania kila kitu kinawezekana.
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Hivi Mama Maria alikuwa naye M NEC ? Na Mama Mkapa je alikuwa nani ? Ama kweli CCM ina mambo mengi baada ya hapo watasema Chadema ya ukoo ?
   
 20. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Au tunaigiza marekani? Lakini mama Hillary alikuja kugombea kiti cha siasa baada ya mumewe kuondoka madarakani. Au hii ni ya Uganda nini? Mmmh yangu macho tu.
   
Loading...