Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Nimezoea kuona mbio za mwenge ambazo zimesheheni shamra shamra, vifijo, sanaa na ujumbe kufikishwa kwa wananchi katika uzito unaostahili.
Mbio za Mwenge za safari hii zimengia Zanzibar kimya kimya na uwepo kwa mbio hizo umepoteza haiba, na hamu hata huwezi kuufuatilia.
Mara ya kwanza kusikia habari zake kuwa umeingia Visiwani ni kupitia ZBCTV wakati Kiongozi wa mbio hizo Nd. George Watson alipotoa misaada ya "vitanda vya kamba (Mayowe)" maarufu vya kukoshea maiti, kwa Wizara ya Afya, Pemba, kwa ajili ya wagonjwa!
Mbio hizo za Mwenge sasa ziko Unguja ambazo pia zimekosa mvuto na umaarufu na kugeuka kuwa mbio za wanasiasa na askari wateule wachache wa FFU.
Msafara wa jeneza (msiba)unaonekana kukusanya watu wengi kuliko ushiriki wa watu kwenye mbio za Mwenge ( furaha).Kulikoni? Tujiulize, Bado una tija, kuhitajika na thamani kwa wananchi? Kipi kifanyike kurudisha ari, mshawasha wa kuupokea na kuuengaenga kama zamani. Au hili linatokea visiwani tu kwenye watu waliokwisha kata tamaa?