Mbio za mwenge 2011

Wabogojo

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
354
87
Wapendwa wanaJF, kuna habari kuwa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2011 hazitakuwepo. Naombwa kujuzwa: Je tetesi hizi ni za kweli na kama ni kweli ni kwa sababu zipi za msingi ikiwa WATANZANIA tunakwenda kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wetu?
 
The difference is the same! Either zipo au hazipo haiwezi kusaidia kupunguza kuanguka kwa uchumi wa nchi!
 
Zitakuwepo, inasemekana zimechelewesha ili wakati wa kuzimwa mwenge iwe siku ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru!
 
Nami nimesikia tetesi hizo, inasemekana ni kutokana na ukata mkubwa unaoikabili serikali, maana mbio za mwenge zinaiingiza serikali gharama kubwa sana. Na huenda serikali imeanza kuelewa kwamba mbio hizo hazina tija kwa taifa
 
Zitakuwepo, inasemekana zimechelewesha ili wakati wa kuzimwa mwenge iwe siku ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru!
Hii itakuwa kali...Yaani mwenge uzimwe siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru!
 
Wapendwa wanaJF, kuna habari kuwa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2011 hazitakuwepo. Naombwa kujuzwa: Je tetesi hizi ni za kweli na kama ni kweli ni kwa sababu zipi za msingi ikiwa WATANZANIA tunakwenda kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wetu?

Zitakuwepo ila si kama ilivyozoeleka....Mwaka huu mbio hizo zitafanyika katika makao makuu ya mikoa tu na hazitafanyika wilayani kama ilivyo ada,mwakani utafanyika utaratibu ule ule wa miaka ya nyuma.....
 
Wapendwa wanaJF, kuna habari kuwa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2011 hazitakuwepo. Naombwa kujuzwa: Je tetesi hizi ni za kweli na kama ni kweli ni kwa sababu zipi za msingi ikiwa WATANZANIA tunakwenda kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wetu?
Nina mshukuru Mungu kama huo mwenge umefutwa na hizo mbio zake kwani hauna tija kwa sisi watanzania,Tujiuliza unapopita na kutumulika nini kinatokea kama sio laana ya kuongezeka kwa mafisadi nguli.
 
ukifuatilia ilani ya uchaguzi iliyokuwa ikinadiwa na mgombea uraisi wa CHADEMA alisema atapopewa ridhaa ya kuwa raisi atahakikisha mwenge wa uhuru unahifadhiwa kwenye jumba la makumbusho ya taifa ili kupunguza gharama kwa taifa. sasa ukiona mwenge haupo tena ujue ilani ya CHADEMA inatekelezwa kwani ndio inayotekelezeka. kwa taarifa nilizo nazo mwenge utapita kwenye makao makuu ya mkoa na sii kwenye wilaya ili kupunguza gharama zisizo za lazima. pia watapunguza msafara wa watu waliopo.
 
Wapendwa wanaJF, kuna habari kuwa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2011 hazitakuwepo. Naombwa kujuzwa: Je tetesi hizi ni za kweli na kama ni kweli ni kwa sababu zipi za msingi ikiwa WATANZANIA tunakwenda kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru wetu?
Nina mshukuru Mungu kama huo mwenge umefutwa na hizo mbio zake kwani hauna tija kwa sisi watanzania,Tujiuliza unapopita na kutumulika nini kinatokea kama sio laana ya kuongezeka kwa mafisadi nguli.
 
Mwenge wa uhuru?! Kwani mwenge ndio ulileta uhuru? Ni kupoteza hela tu,si bora hizo hela zake wangekuwa wanunua ambulance hata kumi kila mwaka!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom