Mbio za Ikulu zapamba moto; Kikwete kupangua makatibu wakuu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Mwandishi Wetu

Toleo la 269
21 Nov 2012




  • CHADEMA wataka mdahaloo Kinana, Dk. Slaa
  • Zitto ashauri CCM inavyoweza kujisafisha
  • Kikwete kupangua makatibu wakuu


WAKATI mawaziri wakiingia katika mchezo wa siasa kwa kuzunguka mikoani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kukabili kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza mabadiliko ya makatibu wakuu wa baadhi ya wizara, Raia Mwema, limeelezwa.

Hayo yanatokea huku CHADEMA, kupitia kwa Kabwe Zitto, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, wakiamini kwamba CCM sasa inafuata nyayo zao katika kuendesha siasa nchini na hayo ni mafanikio makubwa kwao.

Vinginevyo taarifa ambazo Raia Mwema limepata zinasema uamuzi wa Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya makatibu wakuu wa wizara unatarajiwa kufanyika ikiwa ni miezi sita sasa imepita tangu kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri na unaolenga kuongeza nguvu katika mkakati wa CCM kujisafisha mbele ya macho ya umma.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari serikalini, kati ya sababu za mabadiliko hayo ni kubainika kwa tofauti kubwa ya kiutendaji kati ya mawaziri na baadhi ya makatibu wakuu wa wizara wanazoongoza, ikielezwa kuwa, baadhi ya makatibu wakuu wamo kwenye mitandao ya ufisadi katika baadhi ya mashirika yaliyo chini ya wizara zao.

Vyanzo hi vyo vya habari vinasema tayari safu ya makatibu wakuu wapya imeandaliwa na kwamba Rais Kikwete anaweza kutangaza mabadiliko hayo ya makatibu wakuu wa wizara kati ya wiki ijayo na mwanzoni mwaka 2013.

Habari za karibuni kabisa zinasema wizara zinazoweza kukumbwa na mabadilkiko ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi, inayoongozwa na Katibu Mkuu Omari Chambo.

Kuna mambo yanaendelea katkika wizara hiyo ikiwamo na hatua ya Waziri, Dk. Harrison Mwakyembe kuendesha uchunguzi katika Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam kwa kutumia timu maalumu baada ya kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe.

Mbali na uchunguzi huo kufanyika na Dk. Mwakyembe kukabidhiwa ripoti huku akiahidi kuwachukulia hatua wahusika, Waziri huyo pia ameteua wajumbe wapya wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), akiwaondoa wale wa zamani, sambamba na kupendekeza jina la mwenyekiti mpya wa bodi hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye "mamlaka" ya uteuzi.

Lakini pengine lilitokea karibuni zaidi katika wizara hiyo na serikalini kwa ujumla ni kuibuka kwa kampuni ya Uchina ya China Merchant Holdings ambayo ililetwa kuwekeza katika Bandari ya Dar es Salaam na aliyekuwa waziri Omari Nundu, ikapigwa chini kuwa haifai kutokana na mkataba wake wa utata lakini wiki hii ikaibukia Bagamoyo itakakohusika na ujenzi wa bandari kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).

Wizara nyingine ambayo inatarajiwa kupata katibu mkuu mpya ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inayoongozwa na Waziri Dk. Hussein Mwinyi, wizara ambayo iliwahi kutikiswa na madaktari waliowahi kugoma ili pamoja na mambo mengine, kutaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni kuachia ngazi.

"Katika baadhi ya wizara makatibu wakuu wataachwa lakini kunaweza pia kukawa na mabadiliko katika wakuu wa mamlaka au taasisi zinazosimamia sekta ndogo. Kwa mfano, Wizara ya Nishati viongozi watabaki lakini ni lazima kutakuwa na mabadiliko makubwa katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

"Katika Wizara ya Elimu ya Juu kutakuwa na mabadiliko katika Bodi ya Mikopo. Tayari hili umeliona katika Wizara ya Uchukuzi ingawa huko pia kutakuwa na mabadiliko ya katibu mkuu," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Rais Kikwete amejipanga kutangaza mabadiliko hayo ya makatibu wakuu wa wizara mapema zaidi ili kuwapa nafasi viongozi wapya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa bajeti ya sasa lakini pia kuwapa nafasi ya kushiriki katika maandalizi ya bajeti ijayo ya serikali.

Itakumbukwa kuwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, mwezi Mei mwaka huu, Rais aliteuwa mawaziri hao ikiwa tayari kwa sehemu kubwa bajeti za wizara zao zimekwishakuandaliwa na wenzao waliowatangulia.

Kauli ya Kabwe Zitto

Lakini kwa upande wao, CHADEMA, kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto wanasemaje kuhusu hatua hizi za CCM na Serikali?

"Tunaona juhudi za CCM kutaka kujiweka sawa kisiasa. Hata hivyo ni dhahiri kwamba wanafuata nyayo zetu. CHADEMA inaongoza wao wanafuata. Nimemsikia Katibu Mkuu wao anazungumzia kuhusu viwanda Arusha na mambo mengine, lakini ni CCM ndiyo imeua mji wa Arusha kwa kuua viwanda.

"Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma imetoa mapendekezo mengi kuhusu kwa mfano, kiwanda cha General Tyre, lakini Serikali imekaa kimya. Kama wameshindwa kutekeleza maazimio ya Bunge, juhudi za Kinana hazitafua dafu.

"Makundi ndani ya CCM hayataruhusu sekretariati mpya kufanya kazi. Sisi CHADEMA tunataka siasa za masuala yanayohusu nchi. Kinana anaweza kujitahidi kufanikisha hilo lakini njia pekee ya CCM kurudi kwenye mstari ni kupoteza utawala.

Wamechoka mno kujibadilisha.

"Ningefurahi kuona midahalo kati ya Kinana na Slaa (Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA) kuhusu Taifa letu. Nitafurahi kuona shida za wananchi na hasa ukosefu wa kazi, umasikini, elimu na afya zinajadiliwa.

"Ningependa kuona masuala ya namna ya kuvuna kwa ubora utajiri wa rasilimali zetu yakipewa kipaumbele. Ningependa kuona aina mpya za siasa. Siasa za kujenga matumaini kuwa tunaweza kuwa Taifa lisilo na ufisadi. Tunaweza kuwa Taifa imara na bora Afrika," alisema Zitto Kabwe, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mawaziri kupiga siasa

Licha ya mawaziri kutakiwa kusimamia shughuli za kisera katika wizara zao, sasa CCM kimewaongozea jukumu jingine la kupanda katika majukwaa ya kisiasa kueleza namna wanavyotekeleza ilani ya chama hicho.

Taarifa zinasema tayari Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ametangulia mkoani Rukwa ambako kutakuwa na mkutano wa CCM na yeye atazungumzia ujenzi wa barabara za mkoani humo, huku Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda akitangulia mkoani Arusha ambako katika jukwaa la CCM atatakiwa kueleza hatima ya ubinafsishaji usio kuwa na matunda wa baadhi ya viwanda vilivyokuwa bora mkoani Arusha, na nchini, hususan kiwanda cha matairi cha General Tyre Ltd anachokizungumzia Zitto.

Dk. Kigoda ndiye aliyeongoza sera ya ubinafsishaji kwa ngazi ya wizara, ubinafsishaji ambao kwa sehemu kubwa umetawaliwa na malalamiko.

Mkoani Geita, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele atapanda katika jukwaa la CCM kwenye mkutano wa hadhara, kujibu kero za wachimbaji wadogo wa madini mkoani humo, wakati Waziri wa Uchukuzi Dk. Mwakyembe atapanda jukwaani Mtwara pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza.

Mawaziri hao watapanda katika majukwaa ya mikutano ya CCM ikiwa ni awamu ya pili ya uendeshaji huo wa siasa nchini. Awamu ya kwanza ilifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Kigoma, mawaziri kadhaa walipanda jukwaani kujieleza.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekwishazungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hizo za mawaziri katika mikutano ya CCM na kueleza kuwa nafasi ya mawaziri ni lazima itoe "mchango wa kisiasa" kwa upande wa CCM.

Na juzi, Jumatatu usiku, akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Jenerali On Monday kinachoongozwa na Jenerali Ulimwengu katika stesheni ya televisheni ya Channel Ten, Kinana alisema wamejipanga kurejesha haiba ya chama chao na ziara hizo za mikoani wanazopanga kufanya zinalenga kuleta uhai mpya ndani ya chama.

"Tunataka twende hadi katika ngazi ya matawi. Mimi nitakwenda Mtwara na Rukwa na kisha Arusha, kazi moja tutakayoifanya ni kwenda kwenye matawi yetu, huko ndiko wanachama wetu na umma uliko. Tunataka kukijenga upya chama na kuondoa hii taswira kwamba hiki ni chama cha rushwa," alisema Kinana.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kupongezana mwishoni mwa wiki, Makamu wa Bara, Philip Mangula alisema chama chao kimejipa miezi sita kuanzia sasa kusafisha safu zake hasa za walioingia katika safu mbalimbali za uongozi wa chama hicho kwa rushwa.

Baadhi ya waliozungumza na Raia Mwema wamekuwa wakisema kwamba japo sekretariati iliyowaleta kina Kinana madarakani inaonyesha matumaini mapya, bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

"Doa kubwa la CCM ni kuonekana kukumbatia rushwa. Wanaotafuta kuchaguliwa wanatoa rushwa. Wanaotaka kuchagua nao wanataka rushwa. Hachaguliwi mtu bila rushwa, na mtu hachagui bila rushwa na hapo ndipo kazi ngumu ilipo," anasema mmoja wa wanasiasa wakongwe na mwanachama wa zamani wa Tanganyika African Union (TANU) chama kilichozaa CCM.











 
bado hajamaliza hilo zoezi?As if mtu amenunua betri feki za 200/= hakomi zitoa kila mar ana kutupa mwisho wa tukio anakau kakosa vipande ya matangazo ktk radio yake.

Mwenye akili anaona probability ya kupata kiongozi bora ndnai aya CCM ni finyu sana.Ni kama kupepeta pumba kutafuta mabaki ya mchele.
 
Mdahalo mwingine wa manaibu katibu Zito na mwigulu nchemba.tena wote ni wachumi na mmoja alishawahi kuitupa bajeti ya mwenzake.waanze kwanza hawa.
 
Hakuna jipya ccm, iwekwe kando kwanza wajipange upya. Hawawezi kujipanga hawa wakiwa madarakani.
 
Hakuna jipya ccm, iwekwe kando kwanza wajipange upya. Hawawezi kujipanga hawa wakiwa madarakani.
 
Back
Top Bottom