Mbio za baiskeli Dar mpaka Butiama siku 12?

Kwa wazoefu na watu wanaofanya mazoezi ya baiskeli inawezekana kabisa.

Tulikua tunaendesha baiskeli kutokea Shelui - Igunga miaka hiyo bara bara mbovu, baiskeli nzito na tulikua na umri mdogo (miaka 14). Hapo ni umbali wa Takriban KM 36. Ukienda na kurudi inamaana 72 KM. Ila ndio ukirudi ulimi na kinywa vimekauka unatoka utelezi tu.
Mwili wote hauwezi hata kunyanyua kidole.
 
Kwa hao wa baiskeli ni sawa kwani, niliwafuatilia sana, na kwa masaa kama 10, waliyokuwa wanatumia kwa siku ni sawa.wastani wa km 12, kwa saa, tena ni ndogo sana.
hakuna lolote...walipanda magari mpaka Musoma mjini...pale wakaendesha baiskeli mpaka Butiama
 
Kwa wazoefu na watu wanaofanya mazoezi ya baiskeli inawezekana kabisa.

Tulikua tunaendesha baiskeli kutokea Shelui - Igunga miaka hiyo bara bara mbovu, baiskeli nzito na tulikua na umri mdogo (miaka 14). Hspo ni umbali wa Takriban KM 36. Ukienda na kurudi inamaana 72 KM. Ila ndio ukirudi ulimi na kinywa vimekauka unatoka utelezi tu.
Mwili wote hauwezi hata kunyanyua kidole.
Aliyeelewa hiyo sentesi anifafanulie plz
 
Aliyeelewa hiyo sentesi anifafanulie plz

Kwa sasa jikite kwanza kwenye uwezekano wa kufika huo umbali kwa Baiskeli.

Hapo nilimaanisha koo limekauka, ulimi mkavu. Mate yamekauka. Kumbuka unatandikwa jua siku nzima, hambebi maji ya kunywa wala nini. Ukitaka kutma mate ndio hiyo nakwambia ni vitu vinanata tu kwenye ulimi.
 
hakuna lolote...walipanda magari mpaka Musoma mjini...pale wakaendesha baiskeli mpaka Butiama
Sio kweli!!toka wanaanza kila siku walikuwa wanaonyesha kupitia itv, jioni sehemu wanapolala.kwani kuna mtangazaji wa itv na yeye alikuwa miongoni mwao, ndio alikuwa ak ripoti
 
Back
Top Bottom