Mbinu za vurugu kwa jina la chama kingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu za vurugu kwa jina la chama kingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Mar 20, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama tawala hakiwezi kuepuka lawama za mbinu chafu za kufanya vurugu kwa kutumia watu watakaoonekana ni wa chama tofauti.
  1. Tangu mwanzo wamekuwa wakihubiri kuwa vyama vya upinzani ni vya vurugu
  2. Kila eneo wanaloogopa kushindwa vurugu hutumika
  3. Igunga walichoma nyumba na kuandika kikaratasi kinachosema ni CHADEMA.
  4. Hata gari la waandishi watu wanaweza kuona wazi kuwa sio rahisi watu na akili zao wawapige waandishi wakati hakuna waandishi waliwaandika vibaya.

  Kutokana na sababu chache hapo juu na nyingi nyingine nitakazozitoa baadae, Inaonekana wazi kuwa Chama tawala zinatumia mbinu zilizokuwa zinatumiwa urusi. Unachoma nyumba yako ili mtu ajue ni adui yako. Hizi ni mbinu chafu.
  Nawaomba viongozi wa upinzani wakemee wazi vijana wao ili mbinu hii isifanikiwe.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Hao vijana wanaotumika ni wa magamba,wanawavalisha nguo za pipoz ila huku arumeru 2metapakaa kuwatokomeza
   
 3. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka tatizo ni kauli mbiu yenu, vijana hawaielewi, kuna mtu nilimuuliza maana ya PEOPLES POWER akasema ni kutumia nguvu kuiondoa serikali iliyopo madarakani, pia alama ya V ukiangalia kwenye TV yanayoendelea arabuni ni Fujo, kutega mabomu n.k
   
 4. Fungameza

  Fungameza Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  {Inaonekana wazi kuwa Chama tawala zinatumia mbinu zilizokuwa zinatumiwa urusi. Unachoma nyumba yako ili mtu ajue ni adui yako. Hizi ni mbinu chafu.}

  Ushahidi upo? Kama upo mbona wanaotendewa hawaendi kwenye vyombo vya sheria?
  :hand: Tehe teh teh teh
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani cha msingi ni kuhamasisha pande zote kuendeleza kampeni za ustaarabu badala ya kujenga mazingira ya kuonesha kwamba chama fuani ni chanzo cha vurugu au chama fulani kinaonewa.
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 6. K

  KABUKANOGE Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kama wangekuwa wapinzani hakika lingepigwa gari la mgombea ubunge au la makada wegine, ila kwa kuwa limepigwa la waandishi wa habari it is possible wakawa magamba na waandishi inabidi muwe makini kwani mtaumia na hakuna anae weza kupiga mawe mgombea wake, so hujuma zote na mipango michafu zitaishia kwa waandishi wa habari
   
 7. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanajulikana kwa mbinu chafu, tutayasikia mengi zaidi katika wiki ya mwisho ya kampeni
   
 8. d

  davidie JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  akitoke mtu akakuambia maana ya ccm ni chama cha majambazi, pia alama ya jembe na nyundo ni alama ya kikundi kinachoua watu kwa nyundo na kuwachimbia kaburi kwa jembe huko ulaya uatakubali?
   
 9. Fungameza

  Fungameza Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Achana na dhana zisizo na mashiko lete facts bwana.
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,597
  Likes Received: 4,715
  Trophy Points: 280
  CCM ndiyo zao huoni wanavyolambishana sumu wenyewe kwa wenyewe.Muulize Mwakyembe atakujuza kuwa CCM ni nomaaaaaaaaaaaa.
   
 11. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kama banda lililochomwa Igunga lilikuwa la kiongozi wa CCM. Je ulitaka akaseme wamepanga banda lake lichomwe? Nchi nyingine chama wanamhonga mtu aanze kukitukana chama chake cha upinzani. Kisha anapoanza kushunghulikiwa na chama chake, waliomuhonga wanamuua ili ionekana ameuawa na chama chake.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  na kama ni chadema basi wangepiga waandishi wa jamboleo na uhuni sorry uhuru.

  mwananchi na mtanzania wanaripoti vizuri habari za kampeni za chadema na hata wao haiwaingii akilini na kwa taarifa yao ccm hawa waaandishi wameshashtukiamchezo wao mchafu.

  ngojeni wageuze kibao.
   
 13. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Arumeru mashariki hakuna Al-Shabab kama kule Igunga? Mukama atakuja na mbinu hiyo soon.
   
 14. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAKUNA MAHALI WAMEWAHI KUBANWA KWA KARIBU PASITOKEE VURUGU zinazodaiwa kusababishwa na wapinzani.
  Kama wapinzani ndio wanaosababisha vurugu basi wangekuwa wanafanya hivyo hata maeneo mengine ambapo ushindi wa Chama tawala huwa ni dhahiri.
   
 15. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru viongozi wa ccm kwa kuacha kuendelea kutumia vurugu. Naomba hata siku ya uchaguzi waache kura zihesabiwe. Hata mkishindwa basi onyesheni mfano wa ustaarabu.
   
Loading...