Mbinu za Vibaka wa Mbagala.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,647
Jamani hii ni kweli kabisa, yamenikuta.
Ilikuwa hivi,
Ilikuwa mida ya alfajiri mi na waifu tumejihimu tunaelekea kituo cha dala dala ili tuwahi daladala tukamwone ndugu yangu mgonjwa aliyelazwa ktk Hospitali ya Muhimbili.
Kama unavyojua mida ya mapema kama hiyo dala dala huwa ndo kwanza zinaamka.
Wakati tunakaribia kituo cha daladala tukasikia sauti ya mpiga debe..."Mtonganiii.....Temekee....Kariakoo...
..Muhimbiliiii wahi bado wawiliiiii"
Nikamhimiza waifu akaze mwendo kwani tusije tukaikosa hiyo daladala
huku nikimpigia mkwara kuwa nitamwacha 'kwenye mataa' mi niwahi kama hatokaza mwendo.
Sasa tukawa tunaikaribia ile daladala ambayo tulikuwa tukiona imewasha taa za mbele kutokana na kigiza kile cha alfajiri.
Ingawa nilijiuliza mbona taa za nyuma haziwaki lakini sikutilia maanani.
Kuikaribia karibu zaidi ndo hapo tulipobaki hoi.
Kumbe pale tulipofikiri imepaki gari, palikuwa wamesimama jamaa wawili wamewasha tochi ambazo kwa mbali tulifikiri ni taa za gari,
pembeni palikuwa na jamaa mwingine anapiga yale mayowe ya kuita abiria.
Wakati mi na waifu tumetahamaki, ndidpo walipotokea jamaa wengine wapatao nane au zaidi mikononi wakiwa na mapanga makalii.
Nikawa mpole huku waifu akinisihi nisilwaletee ubishi vile vipande vya watu (unazani ningethubutu!!)
wakatupora kila kitu (kasoro mavazi) ikiwemo chupa ya uji wa mgonjwa na vitafunwa.
Bahati nzuri hawaku tujeruhi.
Na safari ikafia hapo.
Ingawa mi na waifu tumekubaliana tusimsimulie yeyote, ila mi nimeona kwa tahadhari niwahabarishe wana JF.
 
Mpola waitu, Naona bora kila mtu anunue bastora, zinauzwa madukani, maana jana usiku saa 4 usiku majambazi yamevamia huko mbagala kingugi na kuua mtu mmoja kujeruhi kadhaa ikiwa ni pamoja na kuiba vitu kadhaa.
 
Mpola waitu, Naona bora kila mtu anunue bastora, zinauzwa madukani, maana jana usiku saa 4 usiku majambazi yamevamia huko mbagala kingugi na kuua mtu mmoja kujeruhi kadhaa ikiwa ni pamoja na kuiba vitu kadhaa.

Mbaya zaidi muda mfupi tu mara baada ya tukio, askari polisi nao ndo haoo wanajivuta.
Na watafanya doria kwa wiki mbili tatu baada ya hapo kimya hadi tukio lingine.
 
Mbagala....kudadeki, hiyo kali.
nisemenini, nikupe pole sana.
Mkuu hatimaye leo nimecheka tena, nimefurahi sana. nimecheka sana, mkasa huo , niyamsimulia na mama watoto wangu home.
pole lakini, mpe pole wife wako.
 
Duuh hiyo mbinu nimeikubali.,ni changamoto kubwa sana kwa wanausalama maana kadri polisi wanavyotafuta njia ya kupambana na vibaka ndivyo vibaka wanavyozidi kubuni mbinu mpya kila kukicha.
 
Yaani hiyo kali. Pole sana ndibalema. Ni somo zuri pia kwetu asante.
 
pole mkuu!! ila kama ka movie fulani hivi. Am very sorry but its very Enterining invention by those guys
 
Ndibalema, wewe ni mtunzi mzuri wa hadithi.....sioni ukweli wa tukio zima!
 
Nakupa pole mkuu na kwanaodhani ni changa la macho tembeleeni maeneo hayo pamoja na tandika yote. Ukiona mbele yako kuna watu na kanzu zao na ukakosea kudhani ni waswahilina wanawahi masjid ujue ndo kiama chako. Mkuu nakupongeza kwa kutuanikia mbinu yao hii mpya.
 
Mhubiri 1:9. Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. Ndiba wizi huo ulienea sana miaka ya tisini mwanzoni maeneo hayohayo ya wilaya ya Temeke kama Mtoni kwa Aziz Ally. Pamoja na hayo pole mkuu
 
kwanza pole sana mkuu na nashukuru Mungu kwamba wewe na mkeo wote mko salama kutokana na tukio hili.

hii stahili ya hawa wezi ni kali mno na nivizuri ulivyoiweka humu ndani hili wengine tuwe makini.

asante sana kwa taarifa hii kusema kweli wezi wetu kiboko hapa niwavulia kofia.
 
The Following 1 User Says Pole to Ndibalema For This Useful Post:
Ebbynature (today)
 
pole kwa kweli inasikitisha ingawa huwezi kuamini lakini yanatokea.

Shukuru Mungu mmebaki salama maana siku hizi wanasema ama zao ama zako. wanajua wakikamatwa kama sio kuuwawa basi ni kuchomwa moto. hivyo lazima na wao waue.
 
Duh!! hawa jamaa mbona wako creative sana?
si wafanye kazi halali inaweza ikawalipa zaidi!
 
Mkuu ndibalema pole sana. kweli nimecheka sana leo hii inathibitisha ule usemi kwamba kuishi mjini ni sawa na kufika form 4, hiyo creativity si mchezo
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom