Mbinu za kutumia ili kuchambua ukusanyaji wa Data/Taarifa binafsi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Unaweza kutumia mbinu kadhaa kuchambua usindikizaji wa data. Baadhi ya chambuzi hizi ni:

1. Msindikaji anapaswa:
i. kuzingatia faragha/usiri wa wenye data;
ii. kutekeleza usindikaji kwa njia ya haki na iliyo halali;
iii. kuwa na kusudi maalum na lengo mwafaka ya kuendeleza usindikaji huo;
iv. kukusanya data toshelevu;
v. kumpa mteja wako maelezo ya kibusara kuhusu sababu za kuchukua data fulani;
vi. kuweka data sahihi;
vii. kuhifadhi data kwa muda unaohitajika; na
viii. kuhakikisha kuwa data inayosindikwa nje ya Nchi inasindikwa katika nchi zilizo na sheria mwafaka za ulinzi wa data.

2. Sababu/Masilahi Mwafaka - Shirika lolote linalosindika data linapaswa kuwa na sababu halali za kusindika data husika. Ikiwa halina sababu halali, usindikaji unapaswa kusimamishwa, na data hiyo kutupiliwa mbali, ili kuzuia matumizi mabaya na haramu ya data hiyo.

Mfano wa sababu mwafaka ni shirika kukusanya data ya watu waliohudhuria sherehe yao ili kuwajibika kifedha; au shirika kukusanya nambari za simu na maelezo mengine ya kuwasiliana na wateja ili kuwasiliana nao baadaye.

Ili kupima na kutambulisha sababu mwafaka, unaweza uliza haya maswali;
a) Shughuli zako za usindikaji wa data ni zipi?
b) Je, kwa nini unaokota na kusindika data binafsi? Ni kwa mujibu wa sheria?
c) Unakusanya data ya aina gani ili kuendeleza shughuli za usindikaji?
d) Data itahifadhiwa kwa muda gani?
e) Ni aina gani ya data haihitajiki?
f) Unahakikishaje kuwa data iliyokusanywa ni bora?
g) Kwa kila shughuli ya usindikaji wa data, ni kwa nini unakusanya data unayokusanya? Kwa mfano ni kwa ajili ya kufuata sheria fulani, au ni kwa ajili ya kuweka vitabu vya kifedha (accounting)?
 
Back
Top Bottom