Mbinu za kusugua meno

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,797
34,167



Toothbrush_0.jpg




Kusugua meno yako ni swala rahisi. Mbinu hii huwa na athari kubwa sana katika afya ya meno yako na afya yako kwa jumla.

Mbinu bora ya kusugua meno:

  • Kwa kutumia mswaki na kwa upole laini na itakayotoshea mdomoni mwako.
  • Mswaki kubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ile ndogo itakufanya kutumia wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ukiwa wahitaji usaidizi katika uchaguzi wa mswaki, zungumza na daktari wako wa meno.
  • Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi.
  • Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno inayolingana na urefu wa nywele wa mswaki.
  • Sugua meno yako angalau mara mbili kwa siku, unapoamka na kabla ya kulala. Ikiwezekana sugua meno yako baada ya kula chakula. Kama hauwezi, sugua mdomo wako hasa baada ya kula vyakula vya sukari.
  • Sugua meno kwa dakika mbili. Angalia kwenye saa kujua muda uliotumia.
  • Badilisha mswaki wako baada ya miezi mitatu au unywele ukijikunja.
Kumbuka kusugua pande zote za meno:

  • Sugua meno yako kutoka kutoka nyuma hadi mbele kwa upole.
  • Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo; ili unywele wa mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutania mahali ambapo chembechembe ya chakula haionekani
  • Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafuna chakula na sehemu ya ndani
  • Tumia unywele wa juu wa mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno yako ya juu; kwa mtindo wa juu na chini
  • Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha pumzi au harufu mbaya.
 
Meno ya watu wazima

Meno yako yapaswa kukaa siku zote za maisha au uhai wako, lakini lazima uyatunze vizuri. Watu wazima wanapaswa kutunza meno yao ilivyo kwa watoto. Utuzi bora wa afya ya meno ni dalili ya afya bora kwa jumla.
Matatizo ya meno, mdomo au kinywa mara nyingi huw ndizo ishara za matatizo mengine katika sehemu nyinginezo za mwili. Magonjwa kama vile ‘Osteoporosis' (Ugonjwa wa kupoteza mifupa na bone density) ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa kisukari mara nyingi huanza kama ugonjwa wa meno.

Hapa pana dalili au ishara unazoweza kuwa nazo ukiwa na matatizo ya meno:

  • Ufizi unaotoa damu
  • Harufu mbaya inayodumu
  • Ladha mbaya daima, mdomoni mwako
  • Mdomo uliokauku, inayosababishwa na matibabu

Tekeleza yafuatayo ukiwa na matatizo ya meno;


  • Mwone daktari wa meno mara moja au mbili kwa mwaka
  • Kunywa maji mengi; glasi 4 – 8 kwa siku hata kama hauhisi kiu
  • Kunywa vinywaji vidogo vilivyo baridi
  • Sugua meno mara kwa mara
  • Zingatia unayokula – ulaji wa vyakula visivyobora husababisha kuwa na meno na fizi isiyo na afya

Jifunze kuhusu kutunza meno yako ili yawe na afya:


  • Dawa ya meno iliyo na floraidi na maji siyo ya watoto tu. Husaidia kila mtu kupunguza uwezo wa kuwa na pengo
  • Sugua meno mara kwa mara hasa baada ya kula vyakula
  • Kula peremende kidogo na vyakula vya sukari kwa kiasi kidogo
  • Usisahau kutoa vyakula kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli
  • Kula vyakula halisi mara kadhaa kwa siku
  • Epukana na tumbaku na tumia vileo kwa kiasi kidogo
 
Meno ya watoto

smile_1_1.JPG




Watoto wenye meno nzuri hukua kuwa watu wazima wenye meno nzuri. Ukiwafunza watoto wako jinsi ya kusugua meno na kutoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli, isitoshe pia kuwapeleka kwa daktari wa meno mara mbili kwa mwaka watakua na meno nzuri na yenye afya
Hata kama meno ya watoto wako itang'oka kisha mengine yamee ni muhimu sana kuyaweka yakiwa safi. Meno ya mtoto wako mchanga huwa katika sehemu muhimu ambazo meno mengine yatamea vizuri akiwa mtu mzima.

Watoto wadogo:
Watoto wako wanapaswa kujifunza kuhusu utunzi bora wa meno kutoka kwako kwa mfano mwema kwa kusugua meno, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli. Wasaidie kusugua na kuondoa vyakula kwenye meno hadi wafikishe umri wa miaka 7 ama 8 ambapo wanaweza kutekeleza wenyewe. Hapa pana njia zitakazoweza kukusaidia.


  • Tumia mswaki ya mtoto iliyo laini na utie kiasi kidogo cha dawa ya meno iliyo na floraidi
  • Fuata maagizo jinsi ya kusugua meno ya mtoto wako lakini tekeleza haya kwa upole
  • Hakikisha kuwa umesugua meno ya mtoto wako kwa dakika mbili
  • Hakikisha kuwa mtoto wako amesuuzia mdomo wake na kutema dawa ya meno. Usiwache waimeze
  • Usisahau kuondoa vyakula katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli.

Hakikisha kuwa mtoto wako anatekeleza tabia hizi njema. Usiwaache wanywe vinyaji vingi baridi au vinyaji vya sukari. Hapa kwa wingi tunamaanisha zaidid ya moja kwa siku. Epukana na tabia ya kumpa mtoto wako vinyaji baridi na vyakula. Haya waweza kufanya mara moja tu. Unywaji wa vinyaji baridi ni mbaya kwa meno ya mtoto wako na ukuaji wake.
 
Meno ya watoto wachanga na watoto walioanza kutembea kidede

Watoto wachanga wenye meno nzuri hukua watu wazima walio na meno nzuri. Ukiwafunza watoto wako kusugua meno na kuondoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli kisha uwapeleke kwa daktari wa meno mara mbili kwa mwaka watakuwa na meno nzuri na yenye afya.
Hata kama meno ya mtoto wako itang'oka kisha wengine yamee, ni vizuri kuyaweka yakiwa safi. Meno ya mtoto wako mchanga huwa katika sehemu muhimu ambazo meno mengine yatamea vizuri akiwa mtu mzima.

Watoto wachanga na wale walioanza kuenda dede.
Ni muhimu na rahisi sana kuweka mdomo ya mtoto wako ikiwasafi; kwa kufanya hivi watazoea kuwa na ufizi ulio safi. Baada ya kila mlo/chakula pangusa ufizi wa mtoto wako na kitambaa chenye unyevunyevu au na shashi hii itaondoa mabaki yoyote ya maziwa.
Hata kama mwanao ana jino moja au meno kumi, huenda pia akawa na mapengo. Pindi ambapo jino moja linamea, anza kulisafisha kwa maji na mswaki mdogo ulio laini. Kisha pangusa mdomo wa mtoto wako. Mtoto wako akigusa meno ondoa uchafu kwa kutumi uzi spesheli. Anza kumpeleka mtoto wako kwa daktari wa meno jino la kwanza likimea au anapofikisha mwaka mmoja. Zingatia swala litakalotokea kwanza
Uozo wa meno huwa jambo la kawaida kwa watoto wachanga na wale walioanza kwenda cheche kutokana na kunywa vinyaji vingi vyenye sukari kama vile maji ya matunda au maji yenye sukari. Pia ni kawaida sana kwa watoto wachanga wanaolala na ‘bottles'.

Njia ya kuzuia uozo wa meno ya mtoto mchanga:

  • Anza kutunza meno ya mtoto wako pindi yanapomea
  • Usimpe mtoto wako maji mengi ya sukari na vinywaji baridi
  • Usimwache mtoto wako alale na chupa ya maziwa, maji ya matunda ama kinyaji chochote kile kitamu mdomoni. Ikiwa mtoto wako anahitaji kitu cha kumfarihi ili alale basi mpe mwigo wa kitu kama vile chuchu au nyonyo bandia ama jaza chupa na maji.
  • Usiwahi tia mwigo wa kitu chochote kile cha kumfariji mtoto kwa sukari au kitu kitamu
  • Ikiwa meno ya mbele ya mtoto wako na madoadoa nyeusi au ya hudhurungi (kahawia) fuata maagizo hapo juu kisha umpeleke kwa daktari wa meno mara moja.
 
Alama ya uchafu/madoadoa kwenye meno


Tumbaku, baadhi ya vyakula na vinyaji vyaweza kufanya meno yetu kuwa na alama ya uchafu na madoadoa kadri tunavyozidi kuzeeka. Alama hizi za uchafu au madoadoa hayasabibishi tatizo lolote la afya. Lakini watu wengi wanatamani kuwa na meno meupe.

Ni nini husababisha alama za uchafu au madoadoa kwenye meno
Baadhi ya vitu vinavyosababisha hali hii ni pamoja na:

  • Uvutaji wa sigara au biri na kutafuna tumbaku. Matumizi ya aina yoyote ya tumbaku yanaweza kuleta ugonjwa wa kansa, ikiwemo kansa ya kinywa. Uchungu ukizidi kwa muda wa siku mbili na zaidi, muone daktari wa meno, labda una jino lililovunjika
  • Vinyaji kama vile chai, kahawa, mkola na mvinyo wenye rangi nyekundu husababisha kuwepo na madoadoa kwenye meno. Chai na mvinyo nyekundu ni nzuri au bora kwa afya yako, lakini hakikisha kuwa umesugua meno baada ya kuvinywa.
  • Matunda kama vile beriberi ni nzuri pia, lakini huchafua meno. Sugua meno yako baada ya kuyala.

Unatibu vipi?
Ikiwa meno yako yana madoadoa au uchaafu, jaribu dawa ya meno itakayofanya yawe meupe. Unaweza kwenda kwa daktari wa meno akaya pausha ingawa ni bei ghali sana. Dawa ya meno husaidia sana ingawa hufanya kazi polepole.
 
Mashimo


Mashimo ni nini?

Mashimo ni uwazi ulio kwenye meno yako na hutokana na meno kuoza. Ingawa ni rahisi sana kuzuia mashimo, ni watu wengi huwa na mashimo. Daktari wako wa meno anaweza akakutibu mapengo ila ni vyema sana kuyatibu kabla hayajazidi au kuwa makubwa au kusabisha maumivu ya meno, ufizi kufura au uchungu wowote ule.

Njia zitakazokuwezesha kuzuia mashimo:

  • Sugua meno yako, kisha uondoe chakula iliyo kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli na umuone daktari wa meno mara kwa mara
  • Usile peremende kwa wingi na vyakula vitamu au vinywaji vingi vilivyo baridi na vinywaji vitamu. Jizoeshe kunywa kinywaji kimoja baridi kwa siku au peremende kidogo.
  • Kula matunda na mboga (itakayosafisha meno yako) ama jibini na mtindi (ambazo ni nzuri kwa meno na ufizi wako) kama kumbwe
  • Ili kutengeneza mate, tafuna sandarusi isiyo na sukari baada ya vyakula. Mate huwa na kemikali inayozuia meno kuoza.
  • Hakikisha kuwa unatumia dawa ya meno iliyo na floraidi. Floraidi hufanya meno yako kuwa na nguvu.
  • Dalili au ishara huwa zipi
  • Ukiona doa nyeusi au hudhurungi (kahawia) kwenye meno au wasikia maumivu ya meno ambayo haishi muone daktari wa meno haraka iwezekanavyo. Usipoende kupata matibabu ya meno, uozo uliopo kwenye meno huenda ikasababisha matatizo mengine kama vile kufura kwa ufizi, maumivu kwenye taya na kichwa kuuma.
  • Unatibu vipi?
  • Safisha/sugua meno yako vizuri, kula vyakula bora na upate uchunguzi wa meno mara kwa mara ili kuzuia matatizo haya.
 
Maumivu ya meno

Je, maumivu ya meno ni nini?
Jino likikuuma, hali hii hutokana na uchungu uliopo kwenye taya ya jino au meno mbili. Uchungu wa meno husababishwa na kitu kukwama katikati ya meno, pengo ama jino linalomea au lililovunjika kutokana na kuuma vitu vigumu sana.

Unaitibu vipi?

  • Suuza kinywa chako na maji vuguvugu kisha tumia uzi spesheli kuondoa chakula kilichokwama katikati ya meno. Ukiwa hauwezi kukiondoa kwa kutumia uzi spesheli, nenda ukamwone daktari wa meno.
  • Meza dawa za kupunguza uchungu
  • Tia barafu kwenye taulo kisha weka kwenye shavu lako kwa muda mfupi. Ikiwa shavu lako limefura; jaribu kutumia njegeve. Itakalibu uso wako kwa urahisi.
  • Uchungu ukiendelea baada ya siku mbili, muone daktari. Yaenda una shimo au jino limevunjika.
 
Meno iliyong'oka


Ukianguka au ugongwe kwenye mdomo kisha meno yako ing'oke, waweza ukarekebisha hali hii ukishughulikia haraka iwezekanavyo. Tunza jino hilo na uende kwa daktari wako wa meno ama chumba cha dharura haraka iwezekanavyo.

Fanya yafuatayo ikiwa jino lako limeng'oka au limelegea

  • Hakikisha kuwa u mzima. Ikiwa hauna fahamu ama una majeraha mabaya mtume mtu yeyote aitishe gari la wagonjwa
  • Ikiwa jino lako halijang'oka kabisa, linalegea tu, wacha mahali hapo ilipo kisha umwone daktari wa meno
  • Ikiwa jino lako limeng'oka kabisa, shikilia na enameli. Kumbuka kwamba haipaswi kushika mizizi iliyo kwenye ufizi
  • Suuza meno yako na maji. Usisugue
  • Jaribu kulitia polepole jino hilo katika shimo. Ikiwa halingii kwa urahisi, weka chini ya ulimi au katikati ya ufizi na shavu. Ikiwa utameza basi litie kwenye glasi ya maziwa, usiliwache likauke
  • Weka shashi au pamba kwenye shimo ikiwa latoa damu kisha shikilia na meno ya juu au chini
  • Nenda kwa daktari wa meno au chumba cha dharura haraka iwezekanavyo
 
Nafurahi nimeikuta hii thread, ni shule nzuri sana! Ubarikiwe Mr.
 
Asante mkuu, somo zuri. Ila mie muda mrefu sana kupiga mswaki, kama dk 5 minimum. Kuna madhara yoyote?
 
Good oral health education or oral hygiene instruction. However, the word "SUGUA" do not look like the meeaning of toothbrushing. Sufuria na chungu vinasuguliwa, meno mmmmh! Bora litafutwe neno muafaka kama kweli tunataka, bado tuendelee kwa sasa kupiga mswaki badala ya kusugua. Tanzania Dental Association mpo???
 
Back
Top Bottom