The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Miradi ndio uti wa mgongo wa taasisi zisizo za kiserikali (NGOs), kupitia miradi taasisi huweza kujiendesha, kutimiza malengo yake ya kimkakati (Strategic objectives) na pia kufikia uono wake (vision attainment). Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufadhili miradi imekuwa ni changamoto kwa taasisi nyingi na kupelekea baadhi ya taasisi kusitisha shughuli.
Ili taasisi iweze kupata fedha kutoka kwa mfadhili kwa ajili ya kutekeleza mradi; haina budi kuwa na ujuzi katika mbinu na matakwa yatakiwayo na mfadhili husika. Mbinu zifuatazo endapo zitatumika ipasavyo zitaiwezesha taasisi husika kupata fedha za mradi kutoka kwa mfadhili yeyote.
· Kuwa na ufahamu juu ya taasisi ambazo zinatoa fedha za miradi. Kuna taasisi za ndani kwa mfano Foundation For Civil Society, hawa wanatoa kuanzia Shilingi milioni 20 ( kwa miradi midogo yaani Innovative projects ya mwaka mmoja) mpaka Shilingi milioni 250 (kwa miradi mikubwa ya miaka mitatu yaani Strategic projects), wanafadhili miradi iliyojikita katika utawala bora (Good governance), kujengea taasisi uwezo (CSOs capacity development) na maendeleo ya kiuchumi (Economic development)
Kwa upande wa taasisi za nje kuna Danish International Development Agency (DANIDA), Agency Francaise de Development (AFD), UK Government Department for International Development (DFID), European Union (EU) na zingine nyingi. Baada ya kuzifahamu taasisi hizi; ni vyema ukafahamu pia wakati gani wanaanza kupokea maombi kwa ajili ya fedha za miradi.
· Kuwasilisha andiko zuri la mradi (Effective project proposal), hii ndio dira inayoonesha ni namna gani mradi utatekelezwa na nini kinatarajiwa baada ya utekelezaji .Uwasilishaji wa maandiko thabiti ya miradi imekuwa ni changamoto kwa taasisi nyingi hapa nchini, maandiko mengi yanakosa uhalisia na hayapimiki (unrealistic and can’t be measured) Kuna miundo mbalimbali katika uandaaji wa haya maandiko, na kila mfadhili huwa na muundo anaopendekeza. Hivyo ni vyema taasisi husika ikafahamu mfadhili anataka muundo gani katika andiko kisha kuliandaa kikamilifu na kuwasilisha.
· Kuwa mshindani (Be competitive) upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi umejaa ushindani kwa kiasi kikubwa. Hivyo ni jukumu la taasisi husika kuibuka mshindi katika ushindani huu ili kuweza kupata hizo fedha. Njia bora na ya uhakika ya kuwa mshindani ni kuhakikisha unatimiza vigezo na masharti yote utakiwayo na mfadhili; kama vile uwasilishaji wa taarifa za benki, nakala ya katiba ya taasisi, barua ya utambulisho kutoka mamlaka za mitaa n.k, pia uwasilishaji wa nyaraka unapaswa kufanywa mapema kabla ya muda kuisha.
· Kuwa na ushirika madhubuti (Having an effective partnership), mashirika kama Umoja wa Ulaya (EU) mara nyingi hutoa fedha kwa miradi ambayo inatekelezwa katika ushirika. Imekuwa ni tatizo kubwa kwa taasisi nyingi hasa pale zinapotakiwa kuchagua taasisi-mshirika ili waweze kupatiwa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi. Kutokana na kutojiandaa mapema katika kutafuta mshirika sahihi, taasisi nyingi hujikuta zinashindwa kutimiza vigezo vya kutafuta ushirika na hatimaye kukosa fedha kutoka kwa mfadhili.
· Usimamizi madhubuti wa mradi (Effective project management), ni bahati mbaya sana taasisi nyingi hutoa nafasi za ajira pindi tu fedha za mradi zinapopatikana, baada ya mradi kuisha; ajira zinafika kikomo. Hivyo taasisi kila siku hujikuta iko na watu wapya katika kutekeleza miradi. Hali hii huifanya taasisi kutokuwa na watu wenye uelewa katika usimamizi wa miradi inayofadhiliwa na mfadhili husika, hivyo huleta changamoto katika ufikiaji wa matarajio ya mfadhili.
The Consult: +255 719 518367
Dar es Salaam