tya02
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 850
- 1,061
Habari zenu,
Wengi wetu tukimenya vitunguu maji na kuvikatakata mara nyingi tunatoa machozi.
Sasa chukua kikombe au bakuli tia chumvi na maji halafu weka pembeni huku ukikatakata vitunguu vyako; kamwe hautotoa chozi wala hutowashwa.
Jaribu leo.
Njia mbadala 1:
Njia mbadala 2:
Njia mbadala 3:
Njia mbadala 4:
Wengi wetu tukimenya vitunguu maji na kuvikatakata mara nyingi tunatoa machozi.
Sasa chukua kikombe au bakuli tia chumvi na maji halafu weka pembeni huku ukikatakata vitunguu vyako; kamwe hautotoa chozi wala hutowashwa.
Jaribu leo.
Njia mbadala 1:
Pia anaweza kukiloweka kitunguu kwenye maji ya moto kwa dk 3 kabla ya kukikata Au kukiweka kwenye freezer kwa dk 10 kabla ya kukikata. Zote hizo zinasaidia
Njia mbadala 2:
Kata kipande kidogo cha kitunguu halafu kiweke kichwani. Kisha endelea kukata kitunguu kama kawaida wala machozi hayatakutoka.
Njia mbadala 3:
Mimi huwa ninavimenya vyenyewe kwanza kabla ya vitu vingine kama nyanya na karoti, then naviacha kwenye yale maji yakuoshea, so hadi nikimaliza kumenya na kukata vitu vingine ndo navitoa kwenye maji na kuvikata.
Naona hii ni simplest way coz u don need any extra things lyk chumvi, sijui bakuli la maji pemben au kuweka kipande kichwani, but also najua kuna umuhimu wa hiyo kemikali yake kwenye mwili ila mambo ya kububujikwa machoz kila mara nehiii.
Njia mbadala 4:
njia nyingine rahisi ni kukata kitunguu huku ukiwa unatafuna kitu chochote iwe big g au carrot mradi uwe unatafuna hakitakuathiri na ni njia nyepesi