Mbinu za kudhoofisha upinzani: Jk ajifunze kwa Kibaki... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu za kudhoofisha upinzani: Jk ajifunze kwa Kibaki...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 9, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Sakata la CCM kubadilisha kanuni ni mbinu ya kuwazuia Chadema wasionyeshe uwezo wao na vipaji vyao vya uongozi Bungeni kupitia kamati za udhibiti wa matumizi ya fedha............................

  Sakata la katiba mpya na CCM kuja na muswada wao ili kumzibia umaarufu Mbunge wa Chadema wa ubungo Mnyika John......na kijana mbichi huyo .......vile vile ni mbinu ya CCM kujaribu kuwanyang'anya Chadema Ilani yao ya uchaguzi na CCM kujimilikisha..........isivyo halali na kinyume cha matarajio ya watanzania walio wengi.......................

  Angelikuwa ni Kibaki angelifanyaje?

  Kibaki ambaye utaalamu wake wa kuwadhoofisha wapinzani wake sasa ni somo kwa wanafunzi wa utawala wa umma tunajifunza yafuatayo..................

  Raila Odinga ambaye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Kibaki alipewa nafasi ya kujimaliza mwenyewe kupitia uwaziri Mkuu.......................Hivi sasa wa-Kenya- ukiondoa wajaluo wenzie Raila- baada ya kuona ukabila uliokithiri wa Raila Odinga hawana hamu naye na sasa hivi wanatafuta vifungu vya kikatiba na sheria kumfukuza kazi ya Uwaziri Mkuu......................................

  Uzoefu huu unatuongoza kuamini ya kuwa CCM na hasa JK mbinu zake za kuipiga vita Chadema ili isiweze kutoa mchango katika ujenzi wa nchi hii zitawajenga Chadema badala ya kuwabomoa na wapigakura watawaunga mkono Chadema- comes 2015- kwa sababu moja tu CCM iliwanyima nafasi yao ya kisheria kuonyesha vipaji vyao kwa kujua wangeliizidi CCM kete za uchapaji kazi....................................

  Angelikuwa JK ndiye Kibaki mbinu yake ingelikuwa ..................."Waache wafu wazike wafu wenzao........." na hivyo kufuata ushauri wa Nyerere kwa CCM mwaka 1995 aliposema.................................."mwacheni Mrema.......................wale wanaotaka kumbeba kama mfu........waacheni.............msiwabughudhi............" Nyerere aliyatamka maneno mazito hayo huku akicheka.......................lakini makada wake kama JK yaelekea somo hilo liliwapita pembeni........hawakumpata mzee kifimbo alimaanisha nini............

  Kwa hiyo JK anashauriwa kuacha ubabe wa kuendesha nchi na kuiga mfano wa Kibaki wa kuwaacha wapinzani waonyeshe vipaji vyao na kama vina walakini jamii tu ndiyo kipimo cha mwisho..........................kwa kuwazibia mwanya wa kufanya kazi Bungeni, JK kwa upeo wake finyu anafikiri kawabomoa kumbe amewajenga sana Chadema................miongoni mwa jamii...........Tatizo la JK ni kuwa hana leadership skills kama alizonazo Mwai Kibakl wa Kenya...........

  Ushauri wangu kwa Chadema ni huu: Msimchukie JK kwa kuwa kupitia ubabe ubabe wake ndiyo anaanza kuwakabidhi nchi bila ya kujijua.............au hata kutaka mwenyewe...................just play your cards closer to your chest...................Unintentionally, though.....JK is slowly but surely handing over power to you.......May the Almighty God bless you in all your endeavors................
   
 2. d

  dicaprio Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Rutas ........ this is grand ...... MAY GOD BLESS TANZANIANS :clap2:
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii thread yako ina matatizo if you read it and make a critical analysis: kibaki na jk hawafanani kwa namna kubwa sana, kwa mfano kibaki was a former economics lecture of the university, jk? watu wengi wa kenya ni waelewa wa mabo ya taifa lao hivyo kibaki haongozi kwa starehe hiyo nchi, jk kila siku kwenye ndege!; halafu IQ za hawa jamaa ni far apart; n.k,n.k
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii mbinu ya Kikwete ni safi saaaaana maana inawapandisha kasi pressure Chademe ili kuharakisha mlipuko wa nguvu ya umma!!!!!!!!!!!!Ninyi subirini tu mtayaona si muda mrefu ujao!!!!!!!!!!! Kuna usemi wa falsafa kwamba ukiondoa haki UNAUA amani: na ndicho wanachofanya sisiemu tangu uchaguzi mkuu (aliyeshika utawala=27%; aliyeshindwa=64%; wabunge kibao bungeni kwa mlango wa uani including PM-wabunge wa mserereko bila kuchaguliwa+wabunge waliotokana na kuporwa kwa nguvu ushindi wabunge wa upinzani hasa CDM); tukio la Arusha; tukio la jana bungeni: Chadema endeleeni kukusanya data halafu mje kwetu nguvu ya umma ili waone ya Tunisia , Misri na Yemen!!!!!!!!!!! Sasa hivi bado tunacheke lakini wale polisi wanaowategemea tutawakimbiza kama Misri!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tena wabunge wa sisiemu waongeze bidii kupora haki tu!!!!!!!!!!!!
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Rutas  ........ this is grand ...... MAY GOD BLESS TANZANIANS  :clap2:
  We are a team..................................
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Hii thread yako ina matatizo if you read it and make a critical analysiskibaki na jk hawafanani kwa namna kubwa sanakwa mfano kibaki was a former economics lecture of the universityjkwatu wengi wa kenya ni waelewa wa mabo ya taifa lao hivyo kibaki haongozi kwa starehe hiyo nchijk kila siku kwenye ndege!; halafu IQ za hawa jamaa ni far apartn.k,n.k
  Maono yako ni mema na ndiyo maana nimemshauri ajifunze kutoka kwa Kibaki ambaye ana Iq kubwa kuliko ya JK...............na jinsi JK anavyokwenda anawajenga Chadema badala ya kuwabomoa...............................
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Lowassa 'bosi' wa Sitta, Membe
  Wednesday, 09 February 2011 21:45

  LYATONGA AMRITHI DK SLAA, ZITTO, SERUKAMBA, JANUARI NAO WAULA
  Exuper Kachenje, Dodoma
  WABUNGE jana waliwachagua wenyeviti wa kamati 16 za Bunge zilizotangazwa juzi usiku na Spika wa Bunge, Anne Makinda, huku waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

  Hatua hiyo inamweka Lowassa kuwa bosi mpya wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwani watalazimika kuripoti kwake masuala yote yanayohusu wizara zao katika vikao vya kamati hiyo nyeti.

  Habari zinasema Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo. Zungu alikuwa akishikilia nafasi hiyo wakati wa bunge la tisa, wakati kamati hiyo ilipokuwa ikiongozwa na Mzee John Malecela.

  Taarifa za uhakika za uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo unaonyesha kuwa Zitto Kabwe, John Cheyo na Augustino Mrema wametwaa uenyekiti wa Kamati za Fedha ambazo kwa mujibu wa kanuni za Bunge hushikiliwa na wabunge wa upinzani.

  Kadhalika Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, akiongoza kamati inayosimamia Wizara ya Ujenzi, inayoongozwa na Waziri, Dk. John Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, pia Wizara ya Uchukuzi inayoongozwa na Waziri, Omar Nundu na Naibu wake Dk. Athuman Mfutakamba.

  Juzi Spika Makinda alitangaza kamati hizo zikiwa na sura na wajumbe mchanganyiko, pamoja na wajumbe kati ya 15 na 28 wengi wakiwa wapya na mabadiliko ya sura katika kamati hizo yakikutanisha wabunge wa vyama tofauti.

  Hali hiyo inaweza kuzifanya kamati hizo kuwa na changamoto kubwa katika kazi zake kutokana na wabunge hao wa vyama tofauti kuwa na itikadi na mitazamo tofauti ya kisiasa na utendaji wa shughuli za umma katika kamati hizo.

  Matokeo yanaonyesha kuwa, Zitto amerejeshwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma,huku Mrema akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambayo Bunge lililopita ilikuwa ikiongozwa na Dk Willibrod Slaa wa Chadema.

  Cheyo naye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nafasi ambayo aliishika pia katika bunge la tisa.

  Habari hizo zinaonyesha kuwa Januari Makamba(CCM)aliyembwaga William Shellukindo jimbo la Bumbuli uchaguzi mkuu uliopita ataongoza Kamati ya Nishati na Madini na Jenista Mhagama akiongoza Kamati ya Maendeleo ya Jamii.

  Kabla ya kubwagwa na Makamba, William Shellukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini katika Bunge la tisa lililoishia mwaka 2010.

  Kamati ya kanuni za bunge tayari inaongozwa na Spika Makinda na naibu wake Job Ndugai akiwa makamu.

  Mpangilio wa kamati hizo, inaonyesha kuwa kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe (Chadema) ni mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi, akiwa na mtangulizi wake, Hamad Rashid Mohamed (CUF) aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika bunge la tisa.

  Katika kamati hiyo yenye wajumbe 23 wapo pia Abdallah Kigoda, Rostam Aziz na Mohamed Missanga wote wa CCM.

  Lowassa katika kamati anayoingoza, pia wapo wabunge wawili wa majimbo ya Ilala, Zungu na Eugen Mwaiposa wa jimbo la Ukonga wote wa CCM wakikutanishwa na Rachel Mashishanga (Chadema) na Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) katika kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na wajumbe wengine ambao jumla yao ni 20.

  Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ina wajumbe 20 huku baadhi ya wajumbe watakaokutanishwa na kamati hiyo wakiwa, Nimrod Mkono, Andrew Chenge wa (CCM), Tundu Lisu, Halima Mdee na Mustafa Akunaay wa Chadema, pamoja na Felix Mkosamalali wa NCCR.

  Cheyo wa UDP anayeongoza Kamati ta Hesabu za Serikali yenye wajumbe 15, baadhi ya wajumbe wake ni Hezekiah Chibulunje (CCM), Vicent Nyerere na Lucy Owenya wa Chadema.

  John Mnyika (Chadema), Zainab Kawawa (CCM), Rukia Kassim Ahmed wa CUF watakutanishwa katika kamati ya Sheria Ndogo ambayo pia inaundwa na wajumbe 15.

  Kwa mujibu wa matangazo ya Bunge, Kamati ya Miundombinu ambayo itaongozwa na Serukamba, itakuwa na wajumbe 26 huku baadhi wakiwa Anne Kilango,Mohamed Shabiby(CCM), Said Amour Arfi (Chadema), Regia Mtema (Chadema) ambapo pia wamo Mohamed Habib Mnyaa(CUF) na Moses Machali wa NCCR.

  Christopher Ole Sendeka na Makamba wa CCM pamoja na wajumbe wengine jumla wakiwa 27 wanaunda Kamati ya Nishati na Madini inayomjumuisha pia Profesa Kulikoyela Kahigi wa Chadema na Yusuph haji Khamis wa CUF.

  Baadhi ya watakaokutanishwa katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Zitto (Chadema) ni Jerome Bwanausi (CCM) na Amina Mohamed Mwidau (CUF)ambapo kamati hiyo ina wajumbe 15.

  Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mrema itakuwa na wajumbe 15 huku baadhi ya watakaokutanishwa wakiwa ni Zabein Mhita, Godfrey Zambi wa CCM, Joseph Selasini na Susan Kiwanga (Chadema) na Kurthum Juma Mchuchuli wa CUF.

  Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira itawakutanisha wajumbe 28 baadhi wakiwa ni Philemon Ndesamburo (Chadema) Magdalena Sakaya (CUF), Hamad Yusuph Masauni, Zhakia Meghji na James Lembeli wa CCM.

  Profesa David Mwakyusa, Profesa Peter Msolla, Nameloki Sokoine wa CCM, Rose Kamili wa Chadema, Salim Hemed Khamis wa CUF watakutanishwa katika kamati ya Kilimo, Mifugo na Mazingira yenye wajumbe 27, ambapo Livingstone Lusinde (Kibajaji), Jenista Mhagama wote wa CCM, Joseph Mbilinyi(Chadema) na Moza Abedy Saidy wa CUF watakutanishwa katika kamati ya Maendeleo ya Jamii yenye wajumbe 24.

  Kamati ya Viwanda na Biashara yenye wajumbe 26 itawakutanisha Chiku Abwao, Godbles Lema na Ezekiel Wenje(Chadema), Gaudence Kayombo na Stella Manyanya pamoja na wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo huku wajumbe 14 wakitoka CCM na 12 vyama vya upinzani.

  Kamati nyingine zilizoundwa ni kamati ya huduma za jamii ikiwa na wajumbe26, kamati ya masuala ya ukimwi ina wajumbe 20 na kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge iliyo na wajumbe16.
  Comments

  12  0 #18 CAROLINE 2011-02-10 07:57 Kafulila na Hamadi wanachofurahia ni kushangiliwa na wabunge wa CCM, lakini hawajui wanaua upinzani nchini. Kama vyama vya siasa mmeshindwa kuendesha vyama vyenu bila CCM basi rudini kundini.Mimi nilitegemea mtu kama Kafulila na Hamadi wangepiga vita vyama vinavyoishabiki a CCM kwani imerudisha taifa letu nyuma sana.
  CHADEMA endelezeni mapambano kwani tunajua iko siku mtaleta ukombozi na sio mbali ni mwaka 2015.Kila mbunge wa CCM anayeshabikia u[NENO BAYA] pale bungeni tunamuona na tunamsubiri kwenye uchaguzi 2015. Huo uchafu wa kupiga makofi utawaisha.

  Quote

  #17 mhogo mchungu 2011-02-10 07:39 Quoting PETRO O NGARIKONI:
  Hakika tumemrudishia Meno Lowasa na kupunguza makali ya Utendaji wa Dr(to be) Samuel Sitta tunayetegemea kuwa ni mzalendo wa pili nani ya Chama Cha Mapinduzi iliyoshindwa kutofautisha wazao na wazungu, warabu na hatimae kuibariki malipo ya kambuni hewa ya Downas.

  Hivi wabunge wa CCM mbona mnamacho lakini hamuoni? Mbona mnauwezo lakini hamtumii? Au mmelogwa?
  Tafadhal na omba niwaondowe kamati ya wazalendo waliojiegemea CCM inaoongozwa na Dr(t be) Samwel sitta, Dr Harson, Christopher Ole SENDEKA na Nemrod Mkono

  Kwanini mnatoa kura zenu kwa Lowasa anayesadika kuwa sio mzuri

  wote hao lao ni mmoja wameahidiwa percent fulani kwenye ya malipo ya Dowans yatakayo fanyika kesho kutwa.Wadanganyika hii imekula kwetu. Mola tuepushe na hili janga.

  Quote

  #16 mhogo mchungu 2011-02-10 07:33 Jamani maumivu mengine yanakuja.Lowasa na mkakati wa uraisi 2015.Jamani huyu mtu ni mjanja sana kwani kamati aliyopewa ndio moja wapo ya mkakati wake wa kugombea uraisi 2015 mnaweza msinielewe kwa sasa ila wakati utakapofika wa yeye kuingia ikulu na kutuletea tene kaka,dada, baba na mama zake Richmond na Dowans ndio hapo tutalia na kusaga meno.
  Quote

  +1 #15 pallaa 2011-02-10 07:32 Hongera Lowasa kwa Uroho wa kutaka tena kuinyonya nchi
  Quote

  +1 #14 PETRO O NGARIKONI 2011-02-10 07:25 Hakika tumemrudishia Meno Lowasa na kupunguza makali ya Utendaji wa Dr(to be) Samuel Sitta tunayetegemea kuwa ni mzalendo wa pili nani ya Chama Cha Mapinduzi iliyoshindwa kutofautisha wazao na wazungu, warabu na hatimae kuibariki malipo ya kambuni hewa ya Downas.

  Hivi wabunge wa CCM mbona mnamacho lakini hamuoni? Mbona mnauwezo lakini hamtumii? Au mmelogwa?
  Tafadhal na omba niwaondowe kamati ya wazalendo waliojiegemea CCM inaoongozwa na Dr(t be) Samwel sitta, Dr Harson, Christopher Ole SENDEKA na Nemrod Mkono

  Kwanini mnatoa kura zenu kwa Lowasa anayesadika kuwa sio mzuri

  Quote

  -3 #13 poly 2011-02-10 07:23 wakati cuf ikiongoza kambi ya upinzani, hizo kamati tatu nyeti ziliongozwa na slaa(chadema),z itto(chadema) na cheyo(udp). Sasa chadema walitaka wachukue wao nafasi hizo zote katika bunge hili. Je nani ni mroho na mchoyo wa madaraka kati ya cuf na chadema? Tutumie hekima kutafakari na sio jazba!!!!
  Quote

  +1 #12 flika 2011-02-10 06:45 Very technical. wapinzani waliopewa uenyekiti wote wepesi, wananunulika. Wangempa Wenje, Mdee, Lema, Ndesa, Mnyika... Anyway ndo faida ya wingi. 2015 Tuchukue nchi tusigombee kuwa 'wapinzani rasmi'
  Quote

  +2 #11 Gombera 2011-02-10 05:48 Huyu Lowasa hakuna viongozi wengine?
  Quote

  +1 #10 mimi 2011-02-10 05:22 Quoting James Mlokozi:
  Nawapongeza sana wabunge kwa kuwatosa Kafulila na Hamad Rashid, lakini nawashangaa sana wabunge kwa kuwachagua Lowasa, Serukamba na Mrema. Hivi mnafikiria nini kuwaweka watu hao kwenye kamati nyeti namna hii na kuwapa madaraka makubwa hivi????? Lakini nawapongeza Lowasa na Kundi lake kwa mafanikio makubwa ya kuiteka kamati ya uongozi ya Bunge letu tukufu. Maana kwa uchaguzi huu wa wenyeviti wa kamati sasa mazingira ya 2015 ni meupeee kwa Lowasa na wenzake. Pamoja na pongezi hizi kwa Lowasa, natoa pole kwa watanzania wote kwasababu naanza kuona kiza kinaingia tayari kwa 2015. Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie nisemayo. Asanteni

  hapati kitu huyo mtu..cha msingi tuanze kuwajenga kizazi kitakachopiga kura 2015 nikimaanisha watoto kati ya 13-18, ubaya wa hawa watu na jinsi wanavyoleta hali ngumu nchini sababu ya ufisadi..changamoto kaeni na wadogo zetu na watoto wetu kuwaelimisha hao ndio wapiga kura wa baadae hao.

  Quote

  +1 #9 elibariki yerald 2011-02-10 05:09 hivi mrema ana lipi jipya zadi ya kukaa na mkuchika kiutetea CCM hivi hawa jamaa wana akili kweli? CHADEMA vipi? nafikiri kama tumesali[NENO BAYA]...
  Quote

  +2 #8 elibariki yerald 2011-02-10 05:07 haya ni madudu na upinani naona umejiua mgoja tuone, utakaaje na wanafiki.?
  Quote

  +2 #7 anonymous 2011-02-10 04:11 [​IMG] kwani huyo lowasa ni mungu hadi astahili tena uongozi? nafasi hio ilifaa apewe sita ila ni ucakachuaji tu utaendelea kwa yeye kupewa hio nafasi Tanzania amkeni!!!!!!!
  Quote

  +2 #6 nop 2011-02-10 02:50 tufikie wakati tusiwe wanafiki, maaana historia itatuhukumu. chadema endeleeni kuwa wavumilivu, mnahoja za msingi japokuwa zinapindishwa, kila kitu kina mwisho mwake
  Quote

  +3 #5 BISHA 2011-02-10 02:24 Mama Makinda hongera sana, lakini jana ulikuwa mpole sana ungewapiga Hamadi na Kufulila vibao kwa kuwasumbua bungeni wakililia madaraka. Chadema ni wavumulivu sana na ndio maana walitoka nje kuliko kuendelea na malumbano na kitu ambacho hakitawezekana. Hongereni sana ndio utulivu huo unatakiwa sio kulumbana na vitu ambavyo vipo wazi.

  Isipokuwa CHEYO hakustahili kupewa kamati huko bungeni kwa sababu ni mbinafsi. Huyu miaka nenda rudi ni mbunge lakini hakuna anachowafanyia watanzani hata kwa mawazo au ushauri hakuna. Kama mwenyekiti wa chama basi apite hate kwenye mikoa watu wamjue. Yaani ukimsikia huyu mtu ni hapo bungeni akimaliza anaenda kujifungia ndani.

  Afadhali hata Mrema utendaji wake unajulikana na bado anaendelea kupambana na wachagga huko kishumundo. Na tunasikia anavyofanya kazi hata kwenye chama chake.

  Quote

  +1 #4 Najaribu 2011-02-10 02:03 Mhifadhi kweli uko sahihi kuwa upinzani wenyewe umeshindwa kuona jinsi wanavyoipeleka nchi hasa pale akina Kafulila na Hamad wasivyokuwa na uwezo wa kuona mbali wakaacha kuisupport CCM. Hivi wangesimama imara wote kukisupport CHADEMA chenye nguvu kubwa kiupinzani si wangefanikiwa kuwatikisa japo kidogo CCM? Sasa wamemfaulisha Lowassa kuwa Rais 2015.

  Ndugu wananchi, nianrudia tena wito wangu, TUAMKE, SAA YA UKOMBOZI NI HII. NI HAPA AMBAPO DOWANS INATUTENGENEZEA MAZINGIRA YA KUPIGA KURA YA KUKOSA IMANI NA SERIKALI.

  Quote  12
  Refresh comments list
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Sitta 'kuwajibika' kwa Edward Lowassa


  Pia wamo Bernard Membe, Mwinyi na Nahodha

  Na Waandishi Wetu, Dodoma

  UCHAGUZI wa wenyeviti wa Kamati za Bunge umemrejesha Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa kwenye uongozi ndani ya mhimili huo
  akishika uenyekiti wa Kamati muhimu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayosimamia wizara nne nyeti, zikiwamo zinazoongozwa na aliyekuwa spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta na Bw. Bernard Membe.

  Ukiacha Wizara ya Afrika Mashariki inayoongozwa na Bw. Sitta na ile ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa inayoongozwa na Bw. Membe, pia kamati hiyo ya Lowassa inazisimamia Wizara za Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inayoongozwa na Dkt. Hussein Myinyi na ile ya Mambo ya Ndani ya nchi inayoongozwa na Bw. Shamsi Vuai Nahodha.

  Bw. Lowassa aliyekuwa mjumbe wa kawaida wa kamati hiyo katika Bunge la tisa lililoongozwa na Spika Bw. Sitta, alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu baada ya kutajwa katika kashfa ya Richmond, hatua iliyosababisha Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya Februari 2008.

  Kutokana na sakata hilo, Bw. Sitta na Bw. Lowassa wameendelea kuwa katika pande mbili hasimu, zenye mafuasi wanaopingana, hadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanachotoka kikaamua kuunda Kamati iliyoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwapatanisha, hatua ambayo inaonekana haikuzaa matunda.

  Kwa upande mwingine, Bw. Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kusaka urais mwaka 2015, uchaguzi wa jana utakuwa umemkutanisha moja kwa moja na Bw. Membe ambaye pia anatajwa kujiandaa kuwania nafasi hiyo, safari hii wizara yake ikisimamiwa na kamati inayoongozwa na mshindani wake.

  Kama harakati hizo za kwenda ikulu ni za kweli, Bw. Lowassa kwa nafasi hiyo atakuwa amelamba dume kwa kuwa itamwezesha kupata taarifa muhimu za Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

  Mbali na Bw. Lowassa wengine waliochaguliwa kuongoza kamati ni pamoja na Bw. Mshirika wake wa karibu, Bw. Peter Serukamba atakayeongoza Kamati ya Miundombinu inayosimamia wizara za ujenzi na Miundombinu, Bw. Januari Makamba (Kamati ya Nishati na Madini) na Bw. Zitto Kabwe anaendelea kuongoza Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

  Kamati nyingine ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa itakayoongozwa na Bw. Augustino Mrema akichukua nafasi iliyokuwa ya Dkt. Willibrod Slaa kipindi kilichopita, Bi. Margaret Sitta atakayeongoza Kamati ya Huduma za Jamii na Bw. John Cheyo ataendelea kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali.

  Kwa upande wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala mwenyekiti ni Bi. Pindi Chana na Kamati ya Maliasili na Utalii, Bw. James Lembeli.

  [​IMG]


  1 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Ama kweli tumekwisha kama wenyeviti ndio hao wabunge tuliowachagua wameamua kuwapa sehemu nyeti mafisadi ok! wananachojali wabunge hao ni matumbo yao na si wananchi.
  yaaani wanadanganywa na pesa kwa ajili ya kuuza utu.

  February 9, 2011 8:57 PM
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  PHP:
                  1 Maoni:          

      [
  IMG]http://img1.blogblog.com/img/blank.gif[/IMG]  
   
  Anonymous said...  Ama kweli tumekwisha kama wenyeviti ndio hao wabunge tuliowachagua wameamua kuwapa sehemu nyeti mafisadi okwananachojali wabunge hao ni matumbo yao na si wananchi.
  yaaani wanadanganywa na pesa kwa ajili ya kuuza utu
      
  February 92011 8:57 PM 
  Maoni haya yanaonyesha watu hawana imani na hizi kamati za Bunge kutokana na viongozi wake wengi kuhusishwa na ufisadi.............................hii inaashiria ya kuwa CCM ilibadili kanuni ili kuwabana Chadema wasitoe viongozi wa kamati za kudhibiti serikali ila vibaraka wa serikali wazishike hizo kamati.................................kupitia upinzani.......................
   
 10. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mwenendo huu lazima siasa zirudi mtaani.........................
   
 11. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfano uliotoa kuwa eti Kibaki alimpatia U PM Raila ni mfano wa Ki-ccm wa kupotosha ukweli! pia maneno uliyojazia eti Wakenya wamemchoka RAO si sahihi hata kidogo kwani bado anapendwa na Wakenya wengi ukiacha wabunge wa ki Kalenjin ambao wanadhani kuwa Raila hajawatetea kuhusu Mashitaka ya The hague!!
  Kuhusu kudhoofisha upinzani Kibaki ndiye anapashwa kujifunza kwa Kikwete maana Kibaki hana pa kutokea. Aliiba uchaguzi, wakenya wakamnasa mpaka akalazimika kuunda serikali ya kugawana madaraka, aliteua rafiki yake Ringera kuongoza TAKUKURU ya Kenya Bunge likamkatalia kwamba amekiuka utaratibu, juzi juzi ameteua Jaji mkuu na mwanasheria mkuu akajikuta anapambana na nguvu ya weledi wa Wakenya. Wakenya wako Ngangari hawatishwi na polisi, hawagawiwi kofia na Kanga wakaufyata, hawaungi mkono Chama kishabiki na wala serikali haiwezi kuwadanganya wakakubali hivi hivi.
  Mzee nahisi thread yako haina pa kujishikia ingawa ulikuwa na nia njema!
   
Loading...