Mbinu za CCM ni zile zile, mkuki kwa nguruwe

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,700
Habari wananchi,

Kuwekua na trend ya CCM kuulaumu aidha moja kwa moja au vinginevyo utawala uliopita ,sababu zinajulikana!

Mara nyingi tu utawala wa Magufuli na watu watu wake walikua wanawalaumu hadharani utawala uliopita; Mfano Ali Happi aliwahi kuwataja kabisa akina Kikwete kuwa wazee mmejichokea acha zamu yetu Rais afanye Kazi; Musiba mara nyingi sana amewahi kuwashutuma Rais kikwete na genge lake kuwa utawala wake ulikua wa kifisadi na ujanja ujanja, nani alikua nampa coverage, confidence na kumlisha maneno wafuatiliaji tunajua.

Kwani ndugu wafuatiliaji mmesahau zile audio clip za simu zilizovujishwa za akina Nape, Makamba, Mzee Makamba, X - Chief Secretary wa CCM Kinana na waziri wa mambo ya nje aliepita Membe?

Mara ngapi Hayati mwenyewe aliwahi kusema hii nchi tumecheleweshwa sana ?wenzake walikua wanajisikiaje?mnajua tulicheleshwa na nani? Simply ni tawala zilizopita.

Kwani mikataba mibovu ya makinikia waliingia akina nani? Kwanini mradi wa gesi ya mtwara Magufuli aliutelekeza na kuanzisha wa kwake wa umeme wa maji wa Stigglers Gorge?

Wafuatiliaji tunaziona picha zenu, tofauti ni kua Magufuli sasa hawezi kujitetea tu, ila kama lawama, malalamiko, kubeza utawala wake uliwafanyia wenzake sana tu, hamna jipya hapa tunachokiona ni gang la utawala uliopita kufurukuta ili dawa iwaingie, shukuruni tu mko chama kimoja ila jela zilikua zinawahusu kwa hasara mliyoisababishia na mnayoendelea kulisababishia Taifa.

Tanzania imekwama hapa sio kwa bahati mbaya,utawala mbovu, katiba mbovu ndio mzizi wa tatizo.

Acha wafu waendelee kutafunana.
 
Najiuliza tu kwa sauti: Kati ya wanaotawala na wapiga-ngojera & taarabu zisizo na mahadhi ya mwambao, akina nani wenye sifa stahiki za kuitwa ^wafu^ hapo kweli!? Najua majibu unayo.

Bi Mkubwa keshasema ^Kazi Iendelee^ japo kweli hatuna hakika ni kazi gani hiyo (maana si kwa hizo dabo kiki za Viingereza vya ^gentolmen^ hukoooo kwa M7), endapo ni kweli kama wasemavyo wengi kuwa Awamu ya 4 ndiye mshika-usukani tena kwa sasa!
 
Aiseee mkuu umetipatia mambo ya msingi sana hasa hili suala la gesi.

Tuliambiwa kabisa kuwa gesi ndiyo ingekuwa ni muaraobaini wa gonjwa la umeme na kuwa tuna kiasi kikubwa sana cha gesi.

Lakini mwendazake akaibuka na mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere, kumbe ilikuwa ni kuutupa mradi wa gesi.
 
Najiuliza tu kwa sauti: Kati ya wanaotawala na wapiga-ngojera & taarabu zisizo na mahadhi ya mwambao, akina nani wenye sifa stahiki za kuitwa ^wafu^ hapo kweli!? Najua majibu unayo. Bi Mkubwa keshasema ^Kazi Iendelee^ japo kweli hatuna hakika ni kazi gani hiyo (maana si kwa hizo dabo kiki za Viingereza vya ^gentolmen^ hukoooo kwa M7), endapo ni kweli kama wasemavyo wengi kuwa Awamu ya 4 ndiye mshika-usukani tena kwa sasa!
Heri awamu ya nne kuwa msaidizi wa awamu hii ya sita angalau tutapumua kuliko awamu iliyopita maana walituendesha kwa visasi.
 
Back
Top Bottom