Mbinu ya medani ya Dr. Slaa na Chadema kunusuru ushindi ni hii hapa............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu ya medani ya Dr. Slaa na Chadema kunusuru ushindi ni hii hapa............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 20, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Hatua hizi mbili Chadema wamekuwa wakizipuuza lakini watakuja kujuta baada ya CCM, NEC na wakurugenzi wa halmashauri ambao NEC inawatumia kama wasimamizi wa chaguzi hii watakapokuwa wamechakachua matokeo ya kura zao:-

  1) Kuishinikiza NEC kuturudishia wapigakura haki yetu ya kimsingi na ya asili ya kulinda kura zetu tukiwa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupiga kura. Hili litazuia mashushu na wanajeshi kuingiza kura haramu za JK na wabunge wake ili kuchakachua matokeo ya matakwa yetu. Au hata kuwazuia au kuwarekodi waharibifu hao kuingia kwenye vyumba vya kura kwa minajili ya kuwarubuni mawakala.

  2) Endapo JK na CCM yake watafanikiwa kuwarubuni mawakala wa Chadema, Dr. Slaa anayo haki ya kuiomba mahakama kuu iagize kura zihesabiwe tena. Hata hivyo, kutokana na kesi inayoendelea mahakamani hapo tayari itabidi kwanza iwe imekifuta kifungu cha katiba kinachokataza mahakama zetu kuchunguza matokeo ya uraisi ambayo NEC tayari itakuwa imeyatangaza.

  Kwa hatua hizi, ushindi wa wazi wa Dr. Slaa na Chadema utakuwa umelindwa kisheria na ukombozi wa kweli wa Mtanzania utakuwa umeanza........
   
Loading...