Mbinu ya kupunguza misongamano makanisani kipindi cha Pasaka na siku zijazo - salamu zangu za Pasaka

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,695
2,000
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wazito kufuata maelekezo ya serikali na wataalam wa afya. Mfano, Jumapili ya Matawi, waamini walishona makanisani utafikiri misa haziwezi kuwa televised, streamed and broadcast on radio live. Kenya wanatumia teknolojia, Vatican ndio usiseme, ni tek kwa kwenda mbele. Kwa wakristo wakatoliki, tumeshuhudia mikusanyiko ya ibada za kanda na jumuiya ikiendelea eti watu wananawa na ku-sanitise, je, vipi kuhusu mita moja na zaidi? Vipi kuhusu kupiga chafya na kukooa?

Rai yangu ni kuwa ibada zote za Pasaka ziendeshwe kwa teknolojia kama live TV, radio, and live streaming ili watu wabaki majumbani mwao. Ibada ni zaidi ya moja, na kila ibada coronavirus waweza kuachwa kwenye viti, hivyo ukinawa wakati wa kuingia waweza wabeba ukiwa ndani kutoka kwenye benchi. Cha msingi TANESCO wasikate umeme. Kwa wakristo wanaopokea chakula cha bwana (Ekaristi), nashauri, chakula hicho kiwekwe kwenye pakiti kama crisps, halafu viongozi wa kanda wakachukue kanisani, halafu wale wa jumuiya wazigawe kwa waamini kwenye nyumba zao. Kama tuambiwavyo, ukipokea bila kujiandaa, basi unakula hukumu, basi naamini zitatumika vizuri. Na ambaye hazimhusu akila, nafikiri hukumu itakuwa mara dufu.

Halafu sadaka tutapeleka kwa M-PESA (jina hili linawakilisha mitandao yote), baada ya kupata namba ya simu ya paroko, na nakala ya sms kum-forward-ia mtunza hazina kwani paroko anaweza hasitoe taarifa kamili kutokana na kutingwa na kazi za kiroho.

Waziri wa afya kesha sema sasa tupo kwenye local transmission kuelekea community transmission, lakini watu bado wana shingo ngumu, masikio yamejaa pamba, wakati mifumo yetu ya afya haiwezi kuhimili hiyo community transmission.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom