Mbinu wanazotumia ulimwengu wa giza kupotosha ukweli kuhusu Mungu

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,381
1,414
Hi Guys!

Moja kwa moja kwenye mada. Niwaombe moods wasiedit majina, nikiyapa yaanze na herufi ndogo ni herufi ndogo hivyo hivyo, herufi kubwa ni herufi kubwa hivyohivyo.

Haya tuendelee, nimeona kuna thread humu imeelezewa kwa kina kweli kumbe inapotosha raia. Hivyo na mimi nimeona nichukue jukumu la kuja kuwaokoa raia wanaopotea kama maandiko yanavyosema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa kuwa na maarifa."

Kuna member ameanzisha thread kuhusu "mungu wa freemasonry" akimnadi kuwa ni mungu mkuu kuliko Mungu aliyezifanya mbingu na nchi, na alijaribu kumbadilishia Mungu wetu jina na kumwita alivyoona yeye lakini Mungu wetu wala haitwi hivyo.

Hiyo thread iliwasha taa ya hatari kwenye ufahamu wangu nikijua fika hizo ni mbinu kadhaa za ulimwengu wa giza kupotosha ukweli kuhusu Mungu wetu wa mbinguni.

Basi moja kwa moja nizibainishe mbinu hizo kama ifuatavyo, na kabla sijaanza kubainisha nieleze tu kwaufupi ni kwamba miungu mingi ilianza kile kipindi cha Mwanzo sura ya 6 na kuendelea, na asilimia kubwa ya miungu hiyo ni nafsi mbalimbali za wanadamu waliowahi kuishi duniani wakaamua kujitukuza na kuabudiwa badala ya Mungu aliyezifanya mbingu na nchi na kuabudiwa. Kuna mungu mmoja pia alianzia kwenye hiyohiyo Mwanzo sita nafsi yake imejigawa huko na huko kila mahali ila na yeye ni nafsi iliyojitukuza vilevile na amebudiwa na umati mkubwa haswa.

Sitajibu maswali kwa sababu sitaki kushindanisha imani. Unachotakiwa kukifanya ni "take it or leave it"

MBINU ZINAZOTUMIWA.

1. WANAKUAMINISHA KWAMBA mungu WAO NDIYE mungu MKUU NA MUUMBAJI

Hii ni mbinu wanayoitumia na hapa wanaweka maneo mengi mazuri yatakayokuvutia uone kuna ukweli ndani yake kumbe siyo. Ulimwengu wa giza hawana jipya, utendaji kazi wao umeiga mbinu ambazo utendaji kazi wa Mungu wa kweli unatumia, hivyo mtu pasipo kufikiri anaweza akaona mbona kama kuna ukweli ndani yake kumbe ni uongo. Hata mitume na manabii wa uongo, wote ibada zao unaweza ukaona zinataka kufanana fanana vile na ukweli, ila wanatambulikana kwa matunda yao kama vile ambavyo imeandikwa "Mtawatambua kwa matunda yao", wengi ni waganga wa kienyeji wanatumia mizimu yao kuwatabiria watu kama ilivyotokea kipindi kile cha Mfalme Sauli alivyoona yamemshinda akaenda kwa mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, ndicho wanachokifanya hawa wa sasa, na wana miungu yao ila unaweza ukadhani ni ukweli kumbe uongo.

2. WANA yesu WAO WA UONGO NA KWA miungu MINGINE MARA NYINGI HUYO yesu WAO WA UONGO UTAKUTA YUKO MSALABANI ANATIA HURUMA KWELI, LAKINI KUMBE NI JANJA YAO.

Kama tunavyojua takribani zaidi ya miaka elfu mbili hivi iliyopita alikuja mtu aliyetikisa ulimwengu hasa ulimwengu wa giza, yaani YESU KRISTO. Matendo yake aliyotenda akiwa duniani yaliacha alama na hayasahauliki, kwani hadi leo umati mkubwa wa wanadamu huenda nchi ya Israeli kushuhudia kwa vitendo matendo yaliyotendwa na mwamba huyu aitwaye KRISTO YESU.

Sasa ulimwengu wa giza ukapiga hesabu tunafanyaje, maana matendo yake yalikuwa dhahiri. Wakaja na mbinu kwamba kila miungu wamtengeneze yesu wao wa uongo ili wanapoteka nafsi za wanadamu zikifikishwa huko zione aah kumbe tuko sehemu salama kumbe siyo, hii pia ni tatizo kutokana na watu wengi kutokuwa na kina katika imani na neno, nafsi inadanganyika kirahisi sana.

3. WANA MBINGU ZAO NA JEHANUM ZAO ZA UONGO.

Hii mbinu wamefanikiwa kidogo sana kuwaaminisha watu kwamba hakuna Jehanum, wengine wakidai hakuna mbingu.

Wanapotosha kwamba mahali panapoitwa toharani, eti kwamba mtu akifa na dhambi anaenda toharani kwa muda anateseka kulingana na dhambi zake kisha anaenda mbinguni. Huu ni uongo, na mbinu hii imefanya wanadamu wajisahau sana na kuishi maisha ya dhambi kisa eti kuna toharani halafu mbinguni.

Pia wengine wanajehanum zao wanaaminisha nafsi za wanadamu wasipotenda hizo kazi zao za giza kwa bidii wataingia huko, kuna wengine wanasema wamepelekwa mbinguni na jehanum ndo hao sasa wamedanganywa na wanakuja kudanganya watu.

Mbingu ipo na Jehanum ipo kwa siku za mwisho hakuna toharani. Wengine wanasema Mungu ni wa huruma eti hataweza kuwaangamisha umati mkubwa wa wanadamu Jehanum na kuhalalisha matendo ya dhambi, pasipo kujua kwamba Mungu akisema amesema, na Neno lake litatimia.

4. MAFUNDISHO YA KISHETANI.

Nyakati hizi ni nyakati za mwisho za hatari, watu wamejitenga na imani na kausikiliza mafundisho ya kishetani.

Mafundisho haya huwafanya watu wasiamini ukweli kuhusu Mungu wa kweli badala yake huwafanya waamini mafundisho ya uongo zaidi.

5. UJIO WA VIUMBE WA AJABU

Kuna viumbe wa ajabu hutokea na kuteka nafsi za wale watu waliokwenda kuwashangaa. Watu wakawaona kama viumbe wenye akili zaidi na wengine wakafikiri ndiyo miungu ya kweli kumbe siyo.

Nikipata nafasi ntakuja kuongeza mbinu zingine wanazozitumia.
 
Umeruka ruka tu hujaleta fact zaidi ya mipasho Ile Ile tunayoikataa kila siku vitisho vitisho uchwara na blaa blaa tu

Kiufupi hata hivyo dini zilizotoka middle east ni copy and paste kutoka katika maandiko ya Sumerian na Assyrian civilization wayahudi waliziedit Ili ziendane na tamaduni zao hakuna mungu wa kweli Wala Mungu wa Nini
Binadamu hajawahi umbwa na kiumbe anayeitwa Mungu Kama baadhi ya ngano za kiyahudi zinavyodai ila sisi ni failed project ya annunak viumbe toka sayari ya nibiru waliotudevelop kutoka primitive yaani watu pori mbaka tukawa modern human Ili kuwasaidia kuchimba madini yatakayowasaidia kurecover sayari yao iliyoharibiwa na vita vya nuclear wakigombania umiliki wa anga katika garaxy yao!
 
Nimesoma ila soma Zaid vitabu mnk bado uajjibu swal ulilo jiukiza wee mwenyew
 
Umeruka ruka tu hujaleta fact zaidi ya mipasho Ile Ile tunayoikataa kila siku vitisho vitisho uchwara na blaa blaa tu

Kiufupi hata hivyo dini zilizotoka middle east ni copy and paste kutoka katika maandiko ya Sumerian na Assyrian civilization wayahudi waliziedit Ili ziendane na tamaduni zao hakuna mungu wa kweli Wala Mungu wa Nini
Binadamu hajawahi umbwa na kiumbe anayeitwa Mungu Kama baadhi ya ngano za kiyahudi zinavyodai ila sisi ni failed project ya annunak viumbe toka sayari ya nibiru waliotudevelop kutoka primitive yaani watu pori mbaka tukawa modern human Ili kuwasaidia kuchimba madini yatakayowasaidia kurecover sayari yao iliyoharibiwa na vita vya nuclear wakigombania umiliki wa anga katika garaxy yao!
aisee
 
Point yako iko hapo kwenye mbinu namba moja
 
Sema wa biblia waliwai kuja tu unadhani wangewai kuja wa miungu ya kigriki ingekuwaje?
Asili ya miungu hiyo walianza pale wanawake wa kibinadamu walipoonekana wazuri wakaja kuolewa na viumbe ambao asili yao sio wanadamu.
 
Umeruka ruka tu hujaleta fact zaidi ya mipasho Ile Ile tunayoikataa kila siku vitisho vitisho uchwara na blaa blaa tu

Kiufupi hata hivyo dini zilizotoka middle east ni copy and paste kutoka katika maandiko ya Sumerian na Assyrian civilization wayahudi waliziedit Ili ziendane na tamaduni zao hakuna mungu wa kweli Wala Mungu wa Nini
Binadamu hajawahi umbwa na kiumbe anayeitwa Mungu Kama baadhi ya ngano za kiyahudi zinavyodai ila sisi ni failed project ya annunak viumbe toka sayari ya nibiru waliotudevelop kutoka primitive yaani watu pori mbaka tukawa modern human Ili kuwasaidia kuchimba madini yatakayowasaidia kurecover sayari yao iliyoharibiwa na vita vya nuclear wakigombania umiliki wa anga katika garaxy yao!
We ndo umeongea pumba kabisa, yaani lengo mwanadamu duniani ni kuwachimbia Annunak madini 🤣🤣,sasa mbona hawaji kuyachukua😂😂,au wewe uliwaona wapi wakija kuchukua hayo madini yaliyopotea🧐,
Kama hukubali uwepo wa Supernatural beings(God, Satan, spirits,etc),ni heri useme tumeevolve kutoka kwa nyani(kama kiranga) itamake sense ,kuliko bangi zisizo na logic unazo tuletea humu🤓
 
Aisee

Una upeo mdogo Sana juu ya haya mambo na Afrika Bado Kuna ujinga mwingi Sana, tatizo elimu tunazopewa za kukariri zinatutesa ndugu hebu jaribu kujisomea ujue
Dunia imepitia civilization ngapi
Kam huijawahi jua mambo ya Assyrian, Sumerians, Babylon, Aztec,misri,dogon tribe
Huwezi jua juu ya historian ya mwanadamu japo upate mwanga

Hivi unajua kwanini jamii za kale zilikua zinaabudu miungu jua?

Kwa taarifa yako ndugu viumbe wanaitwa aannunak kutoka sayari ya nibiru waliwahi kuja hapa Duniani na wakaanzisha mambo mengi Kwa binadamu tuliokua primitive yaani watu pori na kutupa elimu ya nyota,ujenzi,uchimbaji madini,ufuaji vyuma,mavazi,mapambo,mziki,na mengine mengi Sana
Lengo kubwa la hao viumbe ni kupata madini na binadamu Kama man power yao ndio maana mbaka Leo baadhi ya maeneo Kama mwenemutapa Zimbabwe Kuna machimbo ya ajabu yakushangaza ya kale,misri, Aztec mexico,Indonesia, Kuna piramid ambazo ni kazi za ujuzi na maarifa ya hao viumbe na walipomaliza mission yao wakarudi kwao

Baada ya kuondoka binadamu wakaanza waabudu Kama miungu kutoka juu na wakaamini Ipo siku watarudi na ndio maana jamii Kama Aztec wakawa wanawatoa watu kafara Kwa hao miungu hua Ili kuwaomba warudi maana walikua ni neema kwao
Angalia movie ya apocalipto ya mell Gibson utaona nayoyasema
Juu ya hizo ibada za mungu jua
Hata wayahudi walikopy hayo maandiko kutoka vitabu vya kale angalia hata book of Enoch kinaelezea mwanzo wa hao miungu ambao wamewapa jina la malaika

Soma wewe mambo yapo wazi tu Afrika tupo nyuma Sana Sana!
 
Bado hujajibu swali wewe uliwaona lini wamekuja kuchukua hizo dhahabu🤓,na achana na hizo historia uchwara,unawezaje kunithibitishia kisayansi(astronomical,etc),uwepo wao because as far as we know science hasn't detected the existence of other intelligent life forms apart from human beings,wewe ndiyo pumba wa mwisho unapretend kuwaenlightened while still your in the dark,acha kudanganywa na conspiracy theorist,hiyo theory yako ya Sumerians, Lemurians etc isn't viable in the scientific world
 
Wimbi la manabii wa uwongo ndio balaa ni hatar sio poa.
Wamejaa kila kona na mafundisho yao ya uongo. Kwa sasa safari za kwenda Nigeria zitapungua, wanasumbua sana.
 
Ni hatar yani.
Kuna jamaa alikua anasumbuka kwa waganga kutafuta utajir, then baadae akaachana na hizo mambo akaamua kuokoka.

Aliokoka akawa anatoa na shuhuda ya maisha yake na kumtaja Nabii aliye msaidia kuokoka.

Baada ya siku kadhaa karudi tena na shuhuda baba ake wa kiroho yani huyo nabii katembea na mke wake na kamtishia asitoe hiyo siri atakufa. 😂😃

Kuna YouTube channel zimeniteka sana siku hizi ni mwendo wa shuhuda tu
 
Una upeo mdogo Sana juu ya haya mambo na Afrika Bado Kuna ujinga mwingi Sana, tatizo elimu tunazopewa za kukariri zinatutesa ndugu hebu jaribu kujisomea ujue
Dunia imepitia civilization ngapi
Kam huijawahi jua mambo ya Assyrian, Sumerians, Babylon, Aztec,misri,dogon tribe
Huwezi jua juu ya historian ya mwanadamu japo upate mwanga

Hivi unajua kwanini jamii za kale zilikua zinaabudu miungu jua?

Kwa taarifa yako ndugu viumbe wanaitwa aannunak kutoka sayari ya nibiru waliwahi kuja hapa Duniani na wakaanzisha mambo mengi Kwa binadamu tuliokua primitive yaani watu pori na kutupa elimu ya nyota,ujenzi,uchimbaji madini,ufuaji vyuma,mavazi,mapambo,mziki,na mengine mengi Sana
Lengo kubwa la hao viumbe ni kupata madini na binadamu Kama man power yao ndio maana mbaka Leo baadhi ya maeneo Kama mwenemutapa Zimbabwe Kuna machimbo ya ajabu yakushangaza ya kale,misri, Aztec mexico,Indonesia, Kuna piramid ambazo ni kazi za ujuzi na maarifa ya hao viumbe na walipomaliza mission yao wakarudi kwao

Baada ya kuondoka binadamu wakaanza waabudu Kama miungu kutoka juu na wakaamini Ipo siku watarudi na ndio maana jamii Kama Aztec wakawa wanawatoa watu kafara Kwa hao miungu hua Ili kuwaomba warudi maana walikua ni neema kwao
Angalia movie ya apocalipto ya mell Gibson utaona nayoyasema
Juu ya hizo ibada za mungu jua
Hata wayahudi walikopy hayo maandiko kutoka vitabu vya kale angalia hata book of Enoch kinaelezea mwanzo wa hao miungu ambao wamewapa jina la malaika

Soma wewe mambo yapo wazi tu Afrika tupo nyuma Sana Sana!
Kwahiyo huoni kwamba hao viumbe wako ni hovyo kabisa, wameshindwa kabisa kutengeneza madini yao wenyewe, wanakuja kuyataka madini yaliyoumbwa na Mungu Muumbaji. Wanaweza nini sasa?
 
Ni hatar yani.
Kuna jamaa alikua anasumbuka kwa waganga kutafuta utajir, then baadae akaachana na hizo mambo akaamua kuokoka.

Aliokoka akawa anatoa na shuhuda ya maisha yake na kumtaja Nabii aliye msaidia kuokoka.

Baada ya siku kadhaa karudi tena na shuhuda baba ake wa kiroho yani huyo nabii katembea na mke wake na kamtishia asitoe hiyo siri atakufa.

Kuna YouTube channel zimeniteka sana siku hizi ni mwendo wa shuhuda tu
Uongo uongo mwingi, pia watu hawana kina katika imani wanatekeka kirahisi sana.
 
thread ndefu halafu bado imekaa kiutopolo. ulikuwa na nafasi ya kuifupisha kwa kuandika paragraph mbili tu na bado ungeeleweka.
 
Umeruka ruka tu hujaleta fact zaidi ya mipasho Ile Ile tunayoikataa kila siku vitisho vitisho uchwara na blaa blaa tu

Kiufupi hata hivyo dini zilizotoka middle east ni copy and paste kutoka katika maandiko ya Sumerian na Assyrian civilization wayahudi waliziedit Ili ziendane na tamaduni zao hakuna mungu wa kweli Wala Mungu wa Nini
Binadamu hajawahi umbwa na kiumbe anayeitwa Mungu Kama baadhi ya ngano za kiyahudi zinavyodai ila sisi ni failed project ya annunak viumbe toka sayari ya nibiru waliotudevelop kutoka primitive yaani watu pori mbaka tukawa modern human Ili kuwasaidia kuchimba madini yatakayowasaidia kurecover sayari yao iliyoharibiwa na vita vya nuclear wakigombania umiliki wa anga katika garaxy yao!
Hiyo yako pia ni hadithi tu blaa blaa nyingi kama sungura na fisi. Kasome vizuri Annunaki genesis, soma hicho kitabu ukitafakari. Utagundua ni hadithi za kitotosana
 
Back
Top Bottom