Mbinu utakazotumia kurudisha biashara yako kwa mtaji wa shilingi 150,000

Kigorohe

Senior Member
May 21, 2019
160
252
Habari zenu wana JF! Kwanza nitangulize shukurani zangu za dhati kwenu kwani nimekuwa nikijufunza mambo mbalimbali kutoka kwenu, asanteni sana.

Nipende kwenda moja kwa moja katika mada, mimi ni kijana ambaye ni mpambanaji lkn pia nipo moja ya chuo kikuu kilichopo hapa Tanzania. Jamani mimi katika harakati za kusaka pesa nilijaribu kusaka mtaji mpaka nikafikisha takribani 760,0000 mnamo mwezi wa 7. Niliendelea kupambana lkn nikaendelea kupata pesa kidogo kidogo.

Ila sasa kusikitisha sasahivi nimebakiza 150,000 pekee na nahitaji 500,000 kwajili ya ada ili kwenda kuendelea na masomo ifikapo mwezi wa 11. Naombeni msaada wanu ni biashara ipi nitafanya kwa siku hizi chache zilizo bakia kwa kutumia mtaji wa Tsh. 150,000?

Karibuni na Mungu awabariki! Mi nipo Mwanza
 
Dah! Pole sana mkuu kwa hili ase ngoja waje wajuzi...ila kama ni mtu wa kubeti basi ukiweka mkeka mapema tu hela inarudi yani
 
Habari zenu wana JF! Kwanza nitangulize shukurani zangu za dhati kwenu kwani nimekuwa nikijufunza mambo mbalimbali kutoka kwenu, asanteni sana.

Nipende kwenda moja kwa moja katika mada, mimi ni kijana ambaye ni mpambanaji lkn pia nipo moja ya chuo kikuu kilichopo hapa Tanzania. Jamani mimi katika harakati za kusaka pesa nilijaribu kusaka mtaji mpaka nikafikisha takribani 760,0000 mnamo mwezi wa 7. Niliendelea kupambana lkn nikaendelea kupata pesa kidogo kidogo.

Ila sasa kusikitisha sasahivi nimebakiza 150,000 pekee na nahitaji 500,000 kwajili ya ada ili kwenda kuendelea na masomo ifikapo mwezi wa 11. Naombeni msaada wanu ni biashara ipi nitafanya kwa siku hizi chache zilizo bakia kwa kutumia mtaji wa Tsh. 150,000?

Karibuni na Mungu awabariki! Mi nipo Mwanza
Kwa muda uliobaki ni bora ukatulia, hakuna biashara itakayo kupa faida ya iyo pesa ndan ya muda mfupi,

Kama unaroho ngumu na maishani mwako unabahat jaribu kubet, chukua 50k, kuanzia wiki ijayo epl, uefa inacheza jaribu bahat yako, nakwambia unaweza piga pesa ndefu tu, vile vile unaweza liwa hio 50k yote, kama unafuatilia mpira jaribu kucheza mkuu, odd mbili tu zinakupa laki,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom