Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 14,058
- 28,581
Amani iwe nanyi wadau,
Nikiwa sijaonekana kwenye jukwaa hili kwa kipindi sasa huku nikiwa sijapost kitu humu kwa muda mrefu sasa, napenda kuwasalimu wote na kuwaambia kuwa tuko pamoja kwenye ujenzi wa taifa.
Nikirudi kwenye mada kuu ndugu zangu nadhani wote kwa pamoja mtakumbuka hotuba murua aliyoitoa ndugu magufuli wakati akihutubia taifa siku ya kuapishwa kwake hasa kile kipande alichosema "uchaguzi umeisha na raisi ni John Pombe Magufuli, sasa ni kazi tu". Hiki ni kipande murua sana ambacho kwa mtu anayefikiri sawasawa na kuitendea haki akili yake aliyopewa na Mungu bila shaka atajua kuwa pale muheshimiwa raisi alikuwa anamaanisha kuwa Hapa ni kazi tu na kipindi cha watanzania kuendekeza tantalila na siasa huku wakiwa nyuma kimaendeleo basi sasa ni mwisho.
Kilichonifanya niandike huu uzi ni hizi mbinu za hawa washindwaji wa uchaguzi wa mwaka jana wanaojiita UKAWA ambazo zimeegemea katika njia za utekelezaji 3;
1. Ni kuponda kila anachokifanya Magufuli wakidhani kuwa watamkatisha tamaa au kumrudisha nyuma- Hili limeonekana kwenye thread nyingi humu zinazoanzisha na watu wa UKAWA na pia kwenye habari zinazoandikwa na kutangangazwa kwenye media zilizokuwa zinaibeba UKAWA katika uchaguzi wa mwaka 2015 kama Mwananchi, Mtanzania, Citizen, Tanzania Daima, Nipashe, ITV, Mawio na Mwanahalisi.
2. Ni kwa watu wa UKAWA kuanza kutengeneza thread kuwa eti wanajuta kumchagua Magufuli wakati hawa wote walikuwa wanajulikana kuwa walikuwa ni watu wa UKAWA na Lowassa, watu hawa ni kama KIBO 10, SAMURAI, SALARY SLIP NA WENGINEO.
3. Mbinu zilezile za kitoto za wanasiasa wa ukawa kujifanya wanamkandia Magufuli na kumwambia awataje mafisadi, wakwepa kodi, mbinu mfu zisizo na vision nzuri inayoeleweka.
Hizi na baadhi ya mbinu wanazozifanya hawa watu wa UKAWA ikiwemo ya juzi ya kuwalaghai watu eti waliingia na peni zenye kamera kwenye kikao cha kuchagua Meya ili tu kujikweza kujifanya wako hai bado kumbe hata kwa hayo wanayojitangazia na kujisifia nayo kwa watu wenye akili wanaona ni mambo ya kitoto yasio na msingi kwenye mustakabali wa maisha ya mwananchi wa Tanzania anayeitaji kazi na utendaji uliotukuka ili maisha yake yabadirike.
Kusema kweli nawasikitikia hawa ukawa na hizi mbinu zao mfu zisizo na kichwa wala miguu kwa sababu naona hawajui kusoma alama za nyakati.Nyakati ya sasa sio ya siasa siasa na tantalila bali kufanya kazi huku impact ya kazi iyo ikiwa inaonekana tena positively. Hii ndo sera kuu ya Magufuli na mkakati wake mkuu ambao anautekeleza sasa kwa weredi uliotukuka.
Napenda kuiwakumbusha wana UKAWA kuwa hii ni awamu ya tano, awamu ya kazi zinazoleta matokeo chanya na sio siasa na tantalila.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu mbariki raisi Magufuli na watanzania wote.