Mbinu mpya za kunyamazisha wakosoaji

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,096
2,000
Serikali ya awamu ya tano mpaka sasa inalaumiwa kwa kutopenda kukosolewa. Inapenda kupongezwa, kushangiliwa au kuikalia kimya. Watu wamenyamazishwa. Wanaoruhusiwa kutukana mitandaoni na hadharani ni CCM tu. Wanaoruhusiwa kuandamana na kufanya mikutano ya ndani na nje ni CCM tu. Hii haijatosha kuzima kiu ya kunyamazisha wakosoaji. Kuna mbinu mpya zimekuja:

-Ukiikosoa serikali, unatumiwa na Maafisa Uhamiaji ili kuhakiki uraia wako. Baadhi ya viongozi wa dini na asasi za kiraia wamepelekewa barua wathibitishe uraia wao haraka iwezekanavyo. Wamo maaskofu wa TEC, CCT na asasi za kiraia kama ile ya Mama Bisimba.

-Ukithibitisha wewe ni raia, unatumiwa "Msamaria mwema" wa kukujulisha mipango ya kukumiminia risasi au kukupoteza kama waliopotea. Unahakikishiwa kuwa ukifanyiwa hivyo hakuna lolote litakalotokea na watakaofanya hivyo watapandishwa vyeo. Baadhi ya wabunge na wanasiasa wameishakutana na msamaria mwema huyo. Utitiri wa wanaohama vyama uko katika kundi hili.

-Matumizi ya TRA na ile taasisi ya kudhibiti madawa ya kulevya ni jambo la kawaida kwa wakosoaji wenye ukwasi wa fedha mali nyinginezo.

Lakini katikati ya zoezi hili, watekelezaji wanadai fedha nyingi. Kiwango cha rushwa hapa nchini kimepanda bei. Hakuna afisa wa kitengo anayehongwa laki tano tena!

Siamini kama wakubwa wanajua haya yanayoendelea ndani ya nchi.
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,072

Kuandika mnajua Kweli, tatizo ukiwekwa kwenye kumi na nane kuthibitisha maelezo yako ni mwendo wa mavi debe, natoa njambe kibao!
 
mansolata

JF-Expert Member
Aug 8, 2016
503
500
Kijana owa umkosowe mkeo akipika wali mbichi
Kuikosoa serikali ni kuwapandisha vyeo wasiojulikana
 
emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,742
2,000
Tanzania inaelekea kuipita Rwanda, Burundi na Uganda kwenye udikteta, natabiri kwa ukatili unaoendelea Tanzania itakuja kuwa nchi ya ajabu sana na sijui tutakimbilia wapi. Na mimi nailihisi hii hama hama si bure wametishiwa kuuawa kama Ben Saanane na wengineo. Fikiria mtu eti ofisi yake imepigwa bomu alafu baadae eti anarudi ccm, huyo mtu atakuwa punguani kama dhamira yake itamtuma hovyo! There must be an extraordinary force behind him.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom