Mbinu mpya ya watu kupiga Pesa Makanisani, viongozi wa makanisa chunguzeni hizi taarifa za misiba kabla hamjaanza kuchangishana rambirambi

BM X6

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
1,360
4,149
Hii Dunia ni Mungu pekee ndio anajua sisi viumbe wake namna tunavyoishi, Inawezekana mm ndio nimechelewa kujua haya mambo, pengine yapogo na watu wanavuna pesa kwa mtindo huu, ila kwa upande wangu hii ni Mara ya kwanza kushuhudia hii kitu tena kutoka kwa ndugu.

Anyways, nina ndugu yangu anaishi Dar es salaam ila kwao ni Mtwara, ni Mama mtu mzima anakaribia 42 hivi na ana mtoto mmoja, mwanae anafanya kazi za ndani hapo hapo Dar.

Sasa kilichokuja kutokea, huyu Mama kwanza ni mtu wa Dini sana (Mkristo) halafu ni mtaratibu sana, kuna kanisa moja wanajiita 'waaminio' na kuna Nabii wao anaitwa WILLIAM BRANHAM (Pichani). Ukiacha Jumapili pia wanafanya ibada Jumatano na Ijumaa kuanzia saa kumi jioni, ijumaa hii liyopita huyu mama alienda ibada kama kawaida yake ambapo alipofika alimfuata mmoja wa viongozi aliyekuwepo siku hiyo nakumjuza taarifa za msiba wa Mama yake mzazi (Mama yake anaumwa kwa muda sasa Mtwara) basi bila kupoteza muda yule Kiongozi aliwajuza na watu waliohudhuria ibaya siku hiyo ile taarifa ya msiba huku akimpatia elfu 50 ya nauli yule mama na kumuahidi nauli ya kurudi toka msibani

Huyu mgonjwa anayedaiwa amekufa mimi namuita Bibi ila sio Bibi yangu mzaa Mama wala Baba, na hizi taarifa za msiba zilinifikia nilijuzwa na jirani yake Mama mkubwa (wote wanasali kanisa moja) sasa ukipata taarifa ya msiba kikawaida ni lazima uwajuze wengine, ndio hapo nilipo staajabishwa baada ya kumpigia Dogo flani kule mtwara kama amepata taarifa hizi za msiba, akaniuliza "wewe nani kakupa hizo taarifa kwasababu nimetoka muda si mrefu huko kwa mgonjwa ni mzima lakini hali yake si nzuri" nikamwambia taarifa nimezipata Dar ila huyu Dogo alivyonambia tu hali ya mgonjwa sio nzuri, mm moja kwa moja nikaiwekea tiki ile taarifa kwamba huenda dogo wakati anaondoka kwa mgonjwa na muda huo huo ndio mgonjwa alikuwa anakata roho.

Dogo ilibidi arudi kule hospital kwa mgonjwa baada ya mm kumpa taarifa zile alipofika akanipigia akanambia "ni vile tu hali yake sio nzuri ila ningekupa uongee nae" akarudia kuniuliza tena "kwani wewe nani alikupa taarifa hizo" nikamwambia ni jirani yake na Mama mkubwa hivyo taarifa imetoka kwa Mama mkubwa japokuwa mimi hajanambia yeye moja moja na kanisani wamembariki kwa nauli kuja kuzika huko Mtwara. Dogo alishangaa sana na hatimaye taarifa zilifika kwa ndugu wote ila wengi tulijua Mama mkubwa atakuwa kachanganyikiwa tu au alichanganya taarifa wakati anaulizia taarifa za mgonjwa....cha ajabu imekuja kugundulia kwamba huyu mama alikusudia kufanya hivi kwasababu

1: Jirani yake ambaye anasali naye kamziba mdomo, kamwambia asiongee chochote kanisani ila yeye atasafiri kwenda Mtwara, hivyo kanisani wabaki na taarifa za msiba kama zilivyotolewa mwanzo

2: Kawaida ya kanisani hapo inapotokea msiba ni lazima mfiwa asindikizwe na mtu hata mmoja ila huyu Mama unaambiwa hakutaka alimuomba Kiongozi wake aende mwenyewe....na kumbuka hiyo ilikuwa Ijumaa

Jana Jumapili sasa, unaambiwa baada ya ibada Pastor akatangaza taarifa ile ya msiba upya ili taarifa iwafikie wengi zaidi na rambirambi zikakusanywa, wakati huo huyu Mama kashasafiri kwenda Mtwara na anayeshuhudia yote haya ni jirani yake ambaye ndiye aliyenipa taarifa hizi za msiba ambazo hazikuwa za kweli, Jirani anasema alijisikia vibaya sana kuona Pastor anatangaza taarifa za msiba ambao haujatokea, alitamani kwenda kumwambia ukweli lakini ameshindwa, na ukweli huu unaujua yeye tu hapo Kanisani kwao, jambo hili limebaki kichwani kwake anawaza namna ya kufanya

Akae kimya au amwambie ukweli Pastor?
Screenshot_20201214-191730~2.jpg
 
Acha u snitch wew mttoo wa kiume...mbona hayo makanisa yanachkua hela za watu kila siku..zamu yao nao kupigwa....mkuki kwa nguruwe......

Naona kinakuuma saaana..
 
Kwa uzi huu tayari habari zimemfikia pastor na waumini wake...
 
Kumbe nabii wao ni mzungu.
Ok.
Uzi ufutwe.
Hapa umebomoa zaidi ndugu.
Huu uongo ni zao la Lucifer.

Hivyo basi maandiko yanasema alivyo baba ndivyo walivyo watoto wake. Hivyo basi yawezekana Nabii ndio muongo nambari 2, mama yako mkubwa namba 3 na Lucifer namba 1.

Nakumbuka story kama hii iliyokea jeshini , kuruti mmoja alidanganya baba yake kafa. Akapewa pesa arudi kwao kuzika akaishia kula vyuku Dar. Karudi kambini kakaa ikaja taarifa kuwa baba yake kafa. Basi ikajulikana kuwa aliongopa awali.

Alilimwa kichapo ambacho hatakisahau mpaka uzeeni
 
uKIFANIKIWA kusoma vitabu kama hivi hapa hata hiyo hela ya mchango aliyowapiga utaona ni haki yake maana makanisa yamejaa matapeli tu kuna UKAKASI MWINGI sana nahisi jinsi ninavyosoma hivi vitabu nazidi kuwa na exposure kubwa sana
Screen Shot 2020-12-14 at 7.36.30 PM.png
 
Kumbe nabii wao ni mzungu.
Ok.
Uzi ufutwe.
Hapa umebomoa zaidi ndugu.
Huu uongo ni zao la Lucifer.
Hivyo basi maandiko yanasema alivyo baba ndivyo walivyo watoto wake. Hivyo basi yawezekana Nabii ndio muongo nambari 2, mama yako mkubwa namba 3 na Lucifer namba 1.
Nakumbuka story kama hii iliyokea jeshini , kuruti mmoja alidanganya baba yake kafa. Akapewa pesa arudi kwao kuzika akaishia kula vyuku Dar. Karudi kambini kakaa ikaja taarifa kuwa baba yake kafa. Basi ikajulikana kuwa aliongopa awali. Alilimwa kichapo ambacho hatakisahau mpaka uzeeni
Naunga mkono hoja na ndiyo maana napinga Uislam na Ukristo.....Ya nini tuwe tuna waabudu wazungu na waarab ikiwa Mungu alituumba sie Waafrika (binaadam wa kwanza duniani) kwa mfano wake?
 
Back
Top Bottom