Mbinu mpya ya kutongoza mwanamke

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,479
5,068
Sasa hivi ukitaka kupiga sound demu unatumia maneno haya yanayokwenda na wakati

  • Vita ya kutazama uzuri wako haijawahi kuziacha hisia zangu salama.
  • Nipe makinikia ya moyo wako.
  • Naahidi kulipa mirahaba yako na kodi zote za mapenzi.
  • Sitakudanganya kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga wa madini ya mapenzi kama acacia.
  • Please usizuie contena la mchanga wa madini ya penzi langu kwenye bandari ya moyo wako.
  • Usiniundie kamati za marafiki zako kufanya uchunguzi wa makanikia ya upendo wangu.
  • usinitangaze kuwa naiba utajiri wa mgodi wa moyo wako hadharini mbele ya vyombo vya habari.
  • Nitakufata hata kwa private jet kama rais wa Barick.
  • Nitakuomba ukae kwenye meza ya mazungumzo ili uniruhusu kuchimba sukari ya moyo wako.
  • Usiwahusishe viongozi wastaafu ma X wako katika katika ombi langu sababu wengine watakuwa walikusainisha mikataba mibovu ikakuumiza na wengine wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kulijenga taifa la moyo wako.

72cf54e83c9d56aa48ac7309447fef68.jpg
 
Back
Top Bottom