Mbinu mpya wanawake wanayoitumia kumsaliti mpenzi/mume wake

ngajone

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
531
299
Habari za kutwa wana JF.

Leo nawapa mbinu za hawa wake zetu/wapenzi wetu wanazozitumia hasa wanao fanya kazi mbali.

Ilikuwa Jumamosi moja hivi nilikuwa kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja hivi badaa ya kuserebuka vya kutosha mara hee kucheki muda ni saa 6 na ushee nikaona home mbali ikanibidi nitafute logde ya karibu nilale hapo kesho yake nirudi home.

Basi nikaangusha gari hadi alfajiri kama saa 10:50 nikaona huu ni muda wa kutoka kuwahi home ile natoka tu getini nakutana uso kwa uso na shemeji yangu mke wa rafiki yangu amemshika jamaa kimahaba wanaingia mule mule lodge hiyo alfajiri.

Me nikawasalimia akaitikia yule jamaa tu shem kala ngumu sasa nikawa nawaza shemu kila siku anatoka alfajiri kwenda job na kumuacha mumewe ndani kumbe ndio hiki kinacho mfanya atoke kila siku alfajiri kujifanya anakwepa foleni ya magari kumbe sio kweli. Coz rafiki yangu huwa anachelewa kwenda kazini kwake, kumbe shemu anawahi kutoka kuelekea job anapitia sehemu na mchepuko wake wanafanya yao alafu ndio anaelekea kazini.

Yaani hapa natamani kumwambia jamaa lakini naogopa kuvunja mahusiano yao na ukicheki rafiki yangu anampenda sana mke wake. Nawaza; je, nimwambie ukweli best yangu au nikaushe tu?

Nawasilisha. Maoni yenu wadau..
 
Hapo Kausha tuu. Tena jitahidi kila unapokutana na shem mchangamkie kama hukuona chochote vile. Wakati huohuo kaa ukimsoma jamaa ako na huyo shem kisaikolojia, Ikiwezekana hata na mkeo kama unae ili kubaini kama shem karopoka kwamba alikuona asubuhi unatoka lodge. Anaweza kawa kakuwahi ili kujilinda yeye.
Ukimwambia mshikaji wako utakosa yote. shem atakuchukia na ikitokea wameachana sidhani kama jamaa yako atakuwa karibu sana nawe tena. vilevile kama una mke shem lazima nae alipue -hata kama ulitoa taarifa unalala lodge yatawekwa maneno kukuharibia tu.
Cha kumsaidia jamaa yako hapo ni kumshauri aongeze upendo kwa mkewe. Kama wana kijiusafiri ampeleke waifu job kila asubuhi na kumchukua jioni.
 
Kiutu uzima nakushauri uongee na huyo shemeji yako kwanza usikie msimamo wake na kipi kilichomsibu mpaka akatumbukia kwenye uasherati.
Unaweza kumwambia rafiki yako,lakini kwa kuwa kapenda ukaishia kusutwa na shemeji yako na kuonekana mtu wa ajabu katika jamii. Kwa sababu rafiki yako lazima atakutaja atakapofikisha ujumbe.
Wanawake ni wajanja sana katika masuala haya,unaweza kugombana na mshikaji bila sababu ilhali ulikuwa na nia njema kabisa.
Kila la kheri mkuu.
 
Baadhi ya wanawake hawana hata mshipa wa aibu.. Bado wanayofanya humu maofisini ni balaa tupu.
 
Mleta mada nawe vipi. Changamkia hiyo papuchi. Mblackmail muambie huyo shem asipokupa utamsemea kwa mume wake.
 
Hio ni mbinu ya wanaume wengi waliooa. Ukiwa viwanja ukipata mwanamke unaenda nae hotel kwasababu ni usiku sana huwezi kukaa muda mrefu unamuacha alale hspo asubuhi kabla ya kwenda kazini unampitia unapasha then unasepa.
mimi siyo gesti nawatafuna changing room kwenye kubeba boksi. Na nimeapa sitawahi kuoa tena naogopa ishu ya KARMA
 
Habari za kutwa wana jf. Leo nawapa mbinu za hawa wake zetu/wapenzi wetu wanazozitumia hasa wanao fanya kazi mbali. Ilikuwa j,mosi moja hivi nilikuwa kwenye harusi ya jamaa yangu mmoja hivi badaa ya kuserebuka vya kutosha mara hee kucheki muda ni saa 6 na ushee nikaona home mbali ikanibidi nitafute logde ya karibu nilale hapo kesho yake nirudi home. Basi nikaangusha gari hadi alfajiri kama saa 10:50 nikaona huu ni muda wa kutoka kuwahi home ile natoka tu getini nakutana uso kwa uso na shemeji yangu mke wa rafiki yangu amemshika jamaa kimahaba wanaingia mule mule lodge hiyo alfajiri. Me nikawasalimia akaitikia yule jamaa tu shem kala ngumu sasa nikawa nawaza shemu kila siku anatoka alfajiri kwenda job na kumuacha mumewe ndani kumbe ndio hiki kinacho mfanya atoke kila siku alfajiri kujifanya anakwepa foleni ya magari kumbe sio kweli. Coz rafiki yangu huwa anachelewa kwenda kazini kwake Kumbe shemu anawahi kutoka kuelekea job anapitia sehemu na mchepuko wake wanafanya yao alafu ndio anaelekea kazini. Yani hapa natamani kumwambia jamaa lakini naogopa kuvunja mahusiano yao na ukicheki rafiki yangu anampenda sana mke wake. Nawaza je nimwambie ukweli best yangu au nikaushe tu Nawasilisha maoni yenu wadau
Hayakuhusu haya ya shemeji yako,umelala kwa mambo yako maana yawezekana Hata wewe ulilala na kimada tu na ndiyo maana hukwenda home.

Ungelijua alacho nyuki usingalionja asali.

Wanaume na wana wake walio wengi wote si waaminifu wala hakuna wa kulaumiwa upande mmoja tu
 
Mtafute Hugo shem wako. Mwambie ulimuona na aaache. Akikaidi mtafutie MTU mwingine. Akizidi kuwa kichwa ngumu mwambie mumewe. Mathayo 18
 
Hapo Kausha tuu. Tena jitahidi kila unapokutana na shem mchangamkie kama hukuona chochote vile. Wakati huohuo kaa ukimsoma jamaa ako na huyo shem kisaikolojia, Ikiwezekana hata na mkeo kama unae ili kubaini kama shem karopoka kwamba alikuona asubuhi unatoka lodge. Anaweza kawa kakuwahi ili kujilinda yeye.
Ukimwambia mshikaji wako utakosa yote. shem atakuchukia na ikitokea wameachana sidhani kama jamaa yako atakuwa karibu sana nawe tena. vilevile kama una mke shem lazima nae alipue -hata kama ulitoa taarifa unalala lodge yatawekwa maneno kukuharibia tu.
Cha kumsaidia jamaa yako hapo ni kumshauri aongeze upendo kwa mkewe. Kama wana kijiusafiri ampeleke waifu job kila asubuhi na kumchukua jioni.
Sawa mkuu ila kwa upande wangu nilimwambia my wife kwamba siwezi kurudi home kwa usalama wangu na alikubali kiroho safi
 
Back
Top Bottom