Mbinu mbadala ya kumtambua potential 'soul mate' kwa kutumia vidole!

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,365
3,022
Achana na nyota sijui nini mara nge mara ndoo sijui maji/moto etc!! , kule tena mbali sijui herufi za majina mara sijui jina la mama, kabila etc............ kuna njia rahisi sana ya tena inayogundulika mapema ya kumjua potential soulmate wako. Kabla sijaendelea naomba niweke wazi vile naichukulia hii concept ya soul mate;

Nachukulia kwamba kila mtu ako na ma-potential soul mates mamia kwa maelfu hapa duniani. Ni kama ni kama wali tu. Sio kama eti maharage pekee ndio soul mate wa wali, bali hata nyama ni soulmate wa wali, samaki pia etc. Na vingine pia vinaweza kujengewa mazingira vikawa soulmate wa wali pia kibishi. Mfano umaweza kudhani viazi vitamu sio soulmate wa wali, lakini ukiongezea chai ya maziwa ukapata wali kiasi, kipande cha kiazi na chai ya maziwa vikabalansiana vikawa soulmates! So yule mtu atakayemchagua anakuwa ni potential soul mate na maisha yao katika ndoa wanaishi kukamilishana ili kuwa soulmates kamili wakitia juhudi.

Turudi kwenye mada: Nimewahi kujiuliza na kustaajabu! kwamba inakuwaje na inawezekanaje watu wakamilishane mawazo, na sentensi au tu mtu ajue exactly kile mpenzi/mwenza wake atapenda hata kama ni jambo jipya kabisa!?

Mfano: Hawajawahi kununua dinner set, na wala mme hajui mkewe anapendelea maua gani kwenye sahani, lakini akinunua peke yake akiyafikisha nyumbani mke anayafurahia na kusema 'kama ulijua yaani, ungeleta yale ya kijani niliyoyaona yangekuwa sio mazuri kama haya' na mme nae anasema 'wee! kama ulikuwepo, na mi niliyaona hayo ya kijani ila nikahisi haya ndo mazuri zaidi kumbe na we umeona eeh'
Kinyume chake sasa ni wale ambao karibu kila kitu utakuta mwenzi A anaona kitu A ni kizuri halafu mwenzake anachagua B, Mmoja akisema tujenge nyumba mwingine anasema tununue gari kwanza na kila mmoja anakuwa yupo sahihi ila ndo hivyo hawawi sahihi kwa upande mmoja. Mmoja akisema tupumzike home mwingine anadai akafanye kazi, wakati masoul mates wana uwezekano wa kusyncronise hadi mood za vyakula - It takes time though.
Fingers crossed.jpg
Fingers crossed.jpg

Katika ufikiri wangu nikakumbuka mzee wetu aliwahi kutuonesha kwamba sisi ni ndugu na tunatofautiana kufikiri. Kwa hiyo unapokuwa sahihi usifikiri mwingine hawezi kuuona usahihi wa upande mwingine. Alituambia mfano tujaribu kukunja vidole vyetu kama hapo juu pichani. Tuviweke kwa kurelaax kabisa ile kinamna binafsi tunahisi ndio kawaida na comfortable kabisa na ndio sahihi.

Jaribuni kufanya hilo zoezi na marafiki, wenza na wanafamilia muone je kuna uhusiano kati ya kuelewana kirahisi baina ya watu wanaoweka vidole kinamna moja? Kuna watu wataweka;
1. Kidole gumba cha kushoto ndio kipo juu zaidi na kidole-kadogo ka kulia ndio ka mwisho chini - Hawa mzee alisema wanafikiria kutokea kushoto kwenda kulia?

2. Kuna wale ambao kidole gumba cha kulia ndio kipo juu kimewafunika wote halafu kadogo ka mwisho ni ka kushoto! Hawa wanafikiria kutoka kulia kwenda kushoto.

Inawezekana nimepishanisha hizo direction za ufikiri lakini generally tu tambua hao wawili wanafikiria kwa direction mbili tofauti. Wote wanaweza kufika pote au kuishia njiani kabla ya kufika kushoto au kulia.

*Wanaoweka vidole kwa namna moja ndio hawa ninawaita potential soulmates.

Mzee alituonesha hiyo fact kama mbinu ya kutuunganisha na sio kutufarakanisha, maana mara nyingi[kama sio zote] tunapoelewa kuwa wenzetu pia nao wanafikira zao ambazo zaweza kuwa tofauti na sisi inatusaidia kuchukuliana kindugu, kuelewana zaidi, kuaminiana zaidi na kupendana zaidi. So hata kama sio potential-soul mates kwa ufikiri, tunaweza kuwa soul mates kwa kuamua. I believe we [us] make things happen💪

Tena muda mwingine ni faida kubwa kuwa na namna tofautitofauti za ufikiri kuhusu jambo moja hasa kama mnaaminiana. Hii itatoa fursa ya kila mmoja kuiona dunia kwa upana zaidi akisaidiwa na uono wa mwenzi wake. However binafsi naona kupishana kunasaidia zaidi katika mahusiano ya kikazi/biashara/kampuni na sio katika mambo ya maisha ya kifamilia tu. Labda kama unachukulia familia kama bussiness entity na unataka watoto wapate diversity ya viewpoints za baba na mama- Kama ilivyokuwa kwetu mama ni namba 2 na baba ni namba 1. Na familia imedumu!

Imagine tu hicho kitu kidogo itokee labda mpenzi wako anakulazimisha kwamba namna ya kuweka vidole comfortably ni yake, eti kisa yeye akiweka anajihisi comfortable na haelewi wewe unayeweka vingine kuwa unaweza kuwa comfortable pia kwa upande wako........ Hilo ni jambo dogo imagine sasa ni katika maamuzi yanayowaathiri wote wawili, uchumi, malezi ya watoto au mahaba. Kwa kweli kama kuna uwezekano ukampata potential soul mate itapunguza vita nyingi zisizo za msingi. Kumbuka! sio kwamba akiwa potential soul mate ndio hamtapishana. La. Ila nakuambia kutatua matatizo baina yenu kutasaidiwa sana kama namna yenu ya ufikiri ikiwa sambamba.

Kwa hiyo bila kupoteza wakati hebu mdada unayeweka vidole kwa namna ya namba moja na uko na umri chini ya 28yrs embu tuonane PM chaap🤭. Nini unastuka? Labda ni swali tu nataka niulize cmooon! Bado ni nadharia kuna mambo nataka kuthibitisha zaidi. Hata kama nipo single kweli aah! and who knows?
 
Sali sana mkuu

Soul mate wa siku hizi ni pesa
Hahahahaaah eti soulmate ni pesa 😂.

Sawa nazitafuta kwa mambo mengine, lakini sijakata tamaa na bado naaminiamini soulmate ni zaidi ya pesa. Sasa ivi wanawake wanatafuta na kupata pesa kwa hiyo zile power dynamics za kizamani hazifanyi kazi mwanangu.

Imagine mke ana pesa, mme ana pesa unadhani nini kitawaunganisha? Pawa zikilingana ni upendo pekee ndo unaweza kuwaunganisha watu. Hamna namna kuna video iligusia hayo masuala icheki:
 
HAYANAGA FORMULA HAYA NI KAMA BAHATI NASIBU
Sawa bahati nasibu, kind of....

Lakini kumbuka hata bahati nasibu ina kanuni zinazoweza kukuwezesha kuongeza nafasi ya kushinda 🤨. Wanaozichezesha wanazitumia na ndo maana wanapiga faida kila
 
Update/Nyongeza: Kwa kuwa marafiki wengi hasa walioshibana wanafanana ufikiri [fanyeni test ya vidole] na rafki zako muone.

Ndiyo maana sio wazo zuri sana kumchukua rafiki wa X wako wala X wa rafiki yako, utakutana na yaleyale

Anyway hiyo statement hapo juu 👆sio sheria kivile lakini tunajaribu kujiuliza, what are the odds.?
 
Tabia njema ndo msingi wa mahusiano mema, hivyo vdole huko zimbabwe hawana washaviuza, je wao wanajuaje soulmet wao
 
IMG_0041.jpg







SIJAWAHI KUKUTANA NA M2 MWENYE FIKRA KAMA ZANGU.
Neither a man nor a woman.
NEVER.
I THINK AM A DIFFERENT HUMAN BEING.
 
Tabia njema ndo msingi wa mahusiano mema, hivyo vdole huko zimbabwe hawana washaviuza, je wao wanajuaje soulmet wao
Ndio nakubaliana na wewe na nasisitiza ili wawili wawezekanike kuwa mates ni lazima kazi/juhudi na muda vitumike na kila kitu kinachohitajika. Labda tu watasaidika kuoata urahisi kiasi - Bado ni nadharia.

Kweli mnaweza kutofautiana ila mkiaminiana ndio mtakamilishana vizuri zaidi........haya mambo hayana sheria kali, zinanyumbuka
 
View attachment 2250855






SIJAWAHI KUKUTANA NA M2 MWENYE FIKRA KAMA ZANGU.
Neither a man nor a woman.
NEVER.
I THINK AM A DIFFERENT HUMAN BEING.
Yas, inasemekana wanaofikiria kutokea kushoto kwenda kulia ni wachache zaidi [Kutokana na picha na we ni mmoja wao] kuliko wale wa kutoka kulia kwenda kushoto. Bado utafiti unaendelea.

Mi mwenyewe nafikiria namna hiyo na naona ugumu ulivyo kukutana na mtu anayefikiria namna hiyo. Lakini wapo wote wa kike na wa kiume.

Mfano leo nimefanya utafiti kwa watu wanne, wa kike wote nimekuta watatu wote kulia kwenda kushoto na mmoja tu ndio kushoto kwenda kulia.
 
Sali sana mkuu

Soul mate wa siku hizi ni pesa
Said na pesa zake bado aliendelea kusalitiwana swalha hazikumsaidia kulilinda penzi.

Kuna ndoa hazina hela means Wana kipato Cha kawaida na still zinadumu na wanaishi vizuri, Kuna matajiri mapenzi yanawagaragaza vibaya mno.

Mapenzi ni fumbo gumu sababu moto Moyo wa binadamu ni msitu mnene
 
Said na pesa zake bado aliendelea kusalitiwana swalha hazikumsaidia kulilinda penzi.

Kuna ndoa hazina hela means Wana kipato Cha kawaida na still zinadumu na wanaishi vizuri, Kuna matajiri mapenzi yanawagaragaza vibaya mno.

Mapenzi ni fumbo gumu sababu moto Moyo wa binadamu ni msitu mnene
Huwa nakubali hilo jambo la 'fumbo'

Lakini pia naamini kuwa kadri unavyojitahidi kupata 'data' za kulifumbua ndivyo unavyozidi kufanikiwa kulifumbua zaidi na zaidi.
 
Back
Top Bottom