Mbinu mbadala ni ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu mbadala ni ipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Infamous, Nov 19, 2010.

 1. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama sijaridhika na matokeo ya raisi mwaka huu, lakini nikayakubali, uchaguzi ujao wakachakachua tena sikuridhika lakni bado nikakubali, mwaka huu sijaridhika, na sitaki kuyakubali nifanye nini ili kufikisha ujumbe wangu kwa taifa, nipigane, nisimtambue raisi au niamue kukubali tena na nizidi kuburuzwa? Ukipata jibu then relate na uamuzi wa chadema..kisha assume wewe ungekuwa chadema ungefanyaje?
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mbinu waliyotumia CHADEMA ndiyo mbinu inayotumiwa na watu wastaarabu ambao hawataki machafuko au vurugu. Watanzania wengi hawajui siasa ndiyo maana hata kura ya maoni enzi za kukubali vyama vingi au kimoja wengi walipinga vyama vingi kwa kudhani kuwa ni haramu na havifai, ila kutokana na uongozi makini wa mwalimu Nyerere hakukubaliana mawazo ya wengi bali kuruhusu vyama vingi.

  Tukio la kutoka nje wakati Rais anahutubia bunge linamaana kubwa na pana kiasi ambacho kwa mtu mwenye mawazo finyu, atakimbilia kulaani na kulaumu bila kujua dhumuni, faida au lengo la tukio hilo. Hakuna faida ya kuwa na vyama vya upinzani kama vyama vilivyopo haviwezi kuikosoa serikali, au kuonyesha kutoridhishwa na mambo fulani fulani.

  Miaka kadhaa iliyopita waziri mkuu wa Uingereza alipigwa mayai viza wakati anahutubia kikao cha bunge la uingereza, kwa nchi kama yetu hilo likitokea litazungumziwaje?

  CHADEMA walichokifanya ni sahihi na ningewashangaa kama wangebaki kumsikiliza mtu ambaye wameshamkataa. Wanaopaswa kukaa bungeni ni CUF ambao wana ndoa ya mkeka na CCM baada ya kufanya matukio ya aibu fojo na maandamano kupinga ushindi wa karume mwaka 2000 kitu kilichopelekea upotevu wa maisha ya watanzania wasiokuwa na hatia. hayo kwa sasa yamesahaulika, mbaya ni CHADEMA anayeendesha siasa za kiungwana.
   
 3. Patrickn

  Patrickn JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 7,497
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Leaders of people of nations at a particular period of time represent the state of mind of the majority citizens. Kwa hiyo msiwashangae watanzania wanaolaani kitendo waliofanya wabunge wetu wa chadema maana wako gizani. Siku wakielewa watakuja mstari wa mbele tuendeleze mapambano

   
Loading...