MBINU:Jinsi ya kujiunga na jeshi la JWTZ na JKT

Utaweza push up kwenye kokoto

Utaweza kulala polini week6

Utaweza kutembea na viporo vya ugali kwenye mfuko wa kombati

Utaweza kuoga mtoni bila sabuni

Utaweza kutembelea kiwiko cha mikono Mita200

Utaweza kuitunza silaha siku zote za mafunzo

Utaweza kwata LA jasho na damu

Anyway njoooo

strugo ,
Mkuu pokea like.

Nimefurahi sana ulivyo hitimisha " any way njoooo "
 
Kwa ambao tulishafungua moyo tukiwa JKT mujibu wa sheria na sasa tumemaliza chuo, utaratibu wa kujiunga tena na jeshi ukoje?
 
k

Kwa JWTZ
  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
  • Awe hajaoa/hajaolewa
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
  • Awe na tabia na mwenendo mzuri
  • Awe na akili timamu na afya nzuri

Masharti ya Utumishi
  • Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
  • Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

Maafisa
  • Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
    huwafanyia usaili askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za askari wapya (Recruitment Schools).
  • Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
Naomba kuuliza aisee!!

Kuna vijana walioenda JKT kwa mujibu wa sheria,
Na sasa wanamalizia chuo/degree,

Mtu akitaka kurudi jeshini (jwtz) afuate utaratibu gani?
 
Naomba kujua kuhusu wale walioenda kama mujibu wa sheria miaka ya nyuma wanaweza kuomba tena kujitolea maana katika tangazo linasema asiwe amepitia mafunzo ya jkt na pia kupita jkt miaka ya nyuma ni kupoteza sifa ya kujiunga na jkt .....nawasilisha
 
Hili swali hata wale wajuaji wa kila kitu wanaogopa kulijibu.

Nenda wilayani katika office za mshauri wa jeshi la akiba (mgambo) ukaulize then Ukipata majibu Utujuze na sisi.
 
Naomba kujua kuhusu wale walioenda kama mujibu wa sheria miaka ya nyuma wanaweza kuomba tena kujitolea maana katika tangazo linasema asiwe amepitia mafunzo ya jkt na pia kupita jkt miaka ya nyuma ni kupoteza sifa ya kujiunga na jkt .....nawasilisha
Unaomba kama kawaida
 
Utaweza push up kwenye kokoto

Utaweza kulala polini week6

Utaweza kutembea na viporo vya ugali kwenye mfuko wa kombati

Utaweza kuoga mtoni bila sabuni

Utaweza kutembelea kiwiko cha mikono Mita200

Utaweza kuitunza silaha siku zote za mafunzo

Utaweza kwata LA jasho na damu

Anyway njoooo
Kitu akiweza demu cwezi shindwa.
Hayo mazoez simple sana.. Labda wangesema nisilale mwaka zima ningeogopa.
 
Kwa ambao tulishafungua moyo tukiwa JKT mujibu wa sheria na sasa tumemaliza chuo, utaratibu wa kujiunga tena na jeshi ukoje?
JKT hauruhusiwi kupita mara mbili regardless ulipitia kwa mujibu au kujitolea... ila km hauamini nenda wilayani kwako onana na mshauri wa mgambo muulize.
 
Kwa kifupi wanaotakiwa kwa degree yaani miaka 23_25 ni wale walioahirisha JKT mujibu wa sheria na wale ambao hawakwenda mujibu wa sheria either kwa kutochaguliwa au utoro. Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa form six miaka 20_22 nao ni kwa wale wasiopitia mujibu wa sheria tu. Kitu cha tofauti ni kwamba hao form six & degree niliowazungumzia hapo wamepewa chance ya kujitolea ili kuepusha mkanganyiko kwa sababu wengine bado wapo masomoni, wengine wapo kazini.
 
vp kwa mwenye miaka 21 na ana astashahada astashahada anaweza kuapply? au ndo mpaka awe na miaka kuanzia hiyo 23
 
vp kwa mwenye miaka 21 na ana astashahada astashahada anaweza kuapply? au ndo mpaka awe na miaka kuanzia hiyo 23
ndio maana nimesema hao jamaa wana sababu zao maalum kupanga vigezo ivyo. Hapo kwa huyo uliemsema ni kwamba katoka form 4 na kujiunga na diploma program moja kwa moja. Sasa hao jamaa kusema diploma mtu awe na miaka 23_25 wanawalenga wale vijana waliomaliza form four na kufaulu wakaingia A-level ila wakashindwa kujinga na vyuo vikuu (na hawakujiunga na JKT mujibu wa sheria) ivyo wakaamua kutumia vyeti vya form four kusomea diploma ivyo hadi kumaliza diploma wengi wao watakua around 23 to 25 yrs.
 
kwa kifupi asilimia kubwa ya wanaohitajika JKT intake hii ni wale wasioenda mujibu wa sheria na wanapenda kwenda ila kwa mabadiriko kidogo ambapo inabid wajitolee.
 
Naomba kujua kuhusu wale walioenda kama mujibu wa sheria miaka ya nyuma wanaweza kuomba tena kujitolea maana katika tangazo linasema asiwe amepitia mafunzo ya jkt na pia kupita jkt miaka ya nyuma ni kupoteza sifa ya kujiunga na jkt .....nawasilisha
Actually mujibu wa sheria hatakiwi kurudia kozi ya jkt kujitolea wakikugundua watakutoa kabla ya kusajiliwa ila pia wanaweza kukujua na kukuacha
 
Actually mujibu wa sheria hatakiwi kurudia kozi ya jkt kujitolea wakikugundua watakutoa kabla ya kusajiliwa ila pia wanaweza kukujua na kukuacha
kuna jamaa alishapitia JKT kwa mujibu wa sheria alienda mlale wazee wakamtambua kupitia records za makao makuu ya JKT wakamrudisha hata kabla mafunzo hayajaanza.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom