Mbinu hizi za wapinzani zimeshashindwa tayari

gwamaka aswile

Senior Member
Mar 26, 2015
186
106
MBINU HIZI ZA WAPINZANI ZIMESHASHINDWA TAYARI!

Siku chache zilizopita kumetokea tabia ya kushambuliwa kwa maneno kwa baadhi ya wakuu wa wilaya kupitia vyombo vya habari ikiwemo magazeti yakionesha picha mbalimbali za wakuu wa wilaya na kuwakejeli, lakini pia baadhi ya wabunge na mameya na viongozi wengine wamekuwa wakionekana kuwakshfu na kuwadhalilisha wakuu wa wilaya. Hali hii ilishika kasi baada ya Rais kuonesha dalili za kuteuwa wakuu wa wilaya hivi karibuni. Wakuu wa wilaya kikatiba ni wawakilishi wa rais kwa ngazi ya wilaya na ndio wenyeviti wa usalama wa wilaya, kifupi ndio viongozi wakuu ngazi ya wilaya.

Katika uchunguzi uliofanyika wakuu wa wilaya wanaoandamwa sana ni Mh. Paul Makonda (Kinondoni) na Mh. Peter Kasesela (Iringa). Wiki zilizopita viongozi hawa wamekashfiwa sana kwa maamuzi yao ya kiutendaji bila sababu za msingi.

Swali la kujiuliza;

Kwanini wanaowakashfu wakuu wa wilaya wawe viongozi wapinzani tu? Na pia kwanini waje na sababu moja tu ya kuingiliwa majukumu yao? Je hapo mwanzo walikuwa hawaingiliwi majukumu yao? Pia kwanini wale wakuu wa wilaya wanaoonekana wanawajibika sana na kuendana na kasi ya Rais ndio wanaoandamwa? Je hakuna agenda ya siri hapa kwa UKAWA juu ya serikari ya awamu ya Tano? Je, hii sio hasira ya uchaguzi baada ya CCM kushinda na UKAWA kushindwa? Katika uchunguzi wa kina wa wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa wameonesha kuwa hali hii inatokana na upinzani kukosa mbinu mbadala ya kukubalika tena kisiasa na hii imetokana na Rais Magufuli kukubalika sana kwa jamii kuliko mwanasiasa yeyote katika kipindi hichi, hali inayowatisha Upinzani kuwa wanaweza poteza ushawishi wa kisiasa na kushindwa vibaya uchaguzi ujao 2020. Lakini pia imegundulika kuwa Upinzani wamekutana katika vikao vya siri na kukubalina kutumia mbinu hii ya kuwashughulikia wakuu wa wilaya ili kudhoofisha serikali ya awamu ya tano, hali hii imethibitika pale viongozi wa Upinzani wakianza ziara za kimya kimya mikoani kuanzia wiki iliyopita ili kuwachafua viongozi ngazi za wilaya. Huu ndio mkakati walionao sasa Upinzani juu ya serikali ya awamu ya Tano.

Rai yangu;

Upinzani utafute mbinu nyingine kwani mbinu hii imeshajulikana na itawapotezea kabisa nguvu ya kisiasa kwa viongozi wao waliobahatika kupata nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na umeya. Pia watambue kuwa siasa ya kusubiri makosa ya mwingine upate umaarufu imepitwa na wakati.

Pia, wakuu wa wilaya wasikatishwe tamaa na maneno ya wakosoaji, kwani ukiona watu wanakusema sana ujue wanatambua mchango wako, kwa hiyo wanachotakiwa kukifanya ni kusimamia ilani waliyopewa ya CCM ambayo ndio anayoisimamia Rais Magufuli na lazima wajue wanatakiwa waendane na kasi ya Rais ili wasije kuwa mizigo kwa serikali hii.
 
Back
Top Bottom