Mbinu gani ya kutoa taarifa ya msiba kwa muhusika bila kusababisha maafa mengine?

Issuna

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,168
7,513
Nakumbuka nilienda mahali flani wakati wakupiga story alitokea kijana mmoja akaja kuleta taarifa ya msiba wa mama wa mtoto niliye kua nikiongea nae,pale pale yule mama alipata presha akadondoka nae Akafariki..

sasa najaribu kuwaza ni mbinu gani inafaa kwa mtu aliyefiwa na mume/mzazi/mtoto/ndugu halafu sisi majirani au ndugu tuweze kumfikishia taarifa kwa muhusika bila kusababisha Kifo kingine?

Msiba wa bibi yangu mzaa mama nakumbuka mleta Taarifa alinikuta nikiwa na mama..akamwambia mama kua BIBI kafariki Sitosahau kile kibao alichopokea yule kaka,hakugeuka nyuma aliondoka na hakurudi tena Ila ndio hivyo taarifa ikawa ishafika...sasa mama kama nae angekua na matatizo ya presha presha kwa jinsi mletaa taaarifa alivyoileta nadhani tungepata MSIBA mwingine.

NINI KIFANYIKE KATIKA KUFIKISHA TAARIFA KWA NJIA YA USALAMA??
 
Unafika na kumuomba samahani kwa taarifa utakazompa. Kisha unasema umepata taarifa za uhakika kuwa fulani hatunae duniani. Amepumzika kwa amani. Au safari yake imefika tamati.
 
Kama marehemu alikuwa mgonjwa ni rahisi maana wengi saikolojia yao huwa tayari kwa lolote

Tabu ipo kwa kifo cha ghafla hapo ndiyo taarifa inaweza kuleta mshtuko kwa mhusika kwa hiyo ni vyema kumuandaa kisaikolojia kwanza kabla ya kumjulisha juu ya taarifa hiyo mbaya zungumza naye kwa jinsi ya maswali kama mgonjwa wa operation anavyoulizwa wakati akipigwa sindano ya usingizi ukiona yupo vizuri unampa taarifa kuwa X hatunae tena jipe moyo
 
Busara zaidi taarifa za namna hii inatakiwa apewe na ndugu au mtu wake wa karibu sana ambae hata yeye huo msiba unamgusa.
Mfano taarifa ya kifo cha mzazi ukiipokea kutoka kwa ndugu yako mliozaliwa tumbo moja hua haina mshtuko sana kama ukipewa na jirani.
Njia nyingine kama msiba haupo mbali ni bora kumwambia anahitajika sehemu fulani akifika sehemu husika atakutana na mazingira ambayo yataanza kumuweka katika hali ya utayari wa kupokea taarifa tofauti na taarifa ya maneno ambayo hua inakuja na mshtuko zaidi.
 
Hapa duniani watu ufikiri ni pa milele ukifa umekufa mwambie muhusika fulani àmekufa direct hakuna kupindisha wala nini haya mambo sijui tutafute mbinu za kisaikolojia. ni kujisumbua bure
 
Mwambie mhusika xxxx kalala mazima. Hiyo haina madhara

Nakumbuka nilienda mahali flani wakati wakupiga story alitokea kijana mmoja akaja kuleta taarifa ya msiba wa mama wa mtoto niliye kua nikiongea nae,pale pale yule mama alipata presha akadondoka nae Akafariki..

sasa najaribu kuwaza ni mbinu gani inafaa kwa mtu aliyefiwa na mume/mzazi/mtoto/ndugu halafu sisi majirani au ndugu tuweze kumfikishia taarifa kwa muhusika bila kusababisha Kifo kingine?

Msiba wa bibi yangu mzaa mama nakumbuka mleta Taarifa alinikuta nikiwa na mama..akamwambia mama kua BIBI kafariki Sitosahau kile kibao alichopokea yule kaka,hakugeuka nyuma aliondoka na hakurudi tena Ila ndio hivyo taarifa ikawa ishafika...sasa mama kama nae angekua na matatizo ya presha presha kwa jinsi mletaa taaarifa alivyoileta nadhani tungepata MSIBA mwingine.

NINI KIFANYIKE KATIKA KUFIKISHA TAARIFA KWA NJIA YA USALAMA??
 
Hapa duniani watu ufikiri ni pa milele ukifa umekufa mwambie muhusika fulani àmekufa direct hakuna kupindisha wala nini haya mambo sijui tutafute mbinu za kisaikolojia. ni kujisumbua bure
ISHU SIO KUMPA TAARIFA,,,,ishu hapa ni kumpa taarifa vizuri asije ipokea na yeye AKAPOTEA kwa mshtuko.
 
Kama marehemu alikuwa mgonjwa ni rahisi maana wengi saikolojia yao huwa tayari kwa lolote
Tabu ipo kwa kifo cha ghafla hapo ndiyo taarifa inaweza kuleta mshtuko kwa mhusika kwa hiyo ni vyema kumuandaa kisaikolojia kwanza kabla ya kumjulisha juu ya taarifa hiyo mbaya zungumza naye kwa jinsi ya maswali kama mgonjwa wa operation anavyoulizwa wakati akipigwa sindano ya usingizi ukiona yupo vizuri unampa taarifa kuwa X hatunae tena jipe moyo
Nakubaliana na wewe mkuu labda cha kuongezea hapo kwenye msiba wa ghafla, inapendeza ukamuandaa mhusika kwa kuanzia mbali na kupeleka matukio fasta ie unamsogeza pembeni (kama uponae) then unaanza na samahani hivi umepata habari kuwa x kazidiwa ghafla au kakimbizwa hospitali baada ya abc na sikia hali yake bado haijakaa sawa then unamuomba muongozane kwenda eneo la tukio
Nb. Itapendeza zaidi mtoa taarifa akiwa mtu wa karibu kabisa na mhusika, pia hii itumie hatakama unahakika mhusika amefariki mbali na hospital, kidogo inatoa faraja mtu kusikia ndugu yake yupo hospitali hatakama anahali mbaya.
 
Busara zaidi taarifa za namna hii inatakiwa apewe na ndugu au mtu wake wa karibu sana ambae hata yeye huo msiba unamgusa.
Mfano taarifa ya kifo cha mzazi ukiipokea kutoka kwa ndugu yako mliozaliwa tumbo moja hua haina mshtuko sana kama ukipewa na jirani.
Njia nyingine kama msiba haupo mbali ni bora kumwambia anahitajika sehemu fulani akifika sehemu husika atakutana na mazingira ambayo yataanza kumuweka katika hali ya utayari wa kupokea taarifa tofauti na taarifa ya maneno ambayo hua inakuja na mshtuko zaidi.
mi naonaga bora wasiambiwe..waitwe tu LOCATION ila shda inakuja wengine wakiitwa huanza kuuliza kwani kuna nini?? mi nna kazi zangu huku....mkimlazimisha nae anajifanya haelewi..anasubiri mtu amtamkie LIVE
 
Nakubaliana na wewe mkuu labda cha kuongezea hapo kwenye msiba wa ghafla, inapendeza ukamuandaa mhusika kwa kuanzia mbali na kupeleka matukio fasta ie unamsogeza pembeni (kama uponae) then unaanza na samahani hivi umepata habari kuwa x kazidiwa ghafla au kakimbizwa hospitali baada ya abc na sikia hali yake bado haijakaa sawa then unamuomba muongozane kwenda eneo la tukio
Nb. Itapendeza zaidi mtoa taarifa akiwa mtu wa karibu kabisa na mhusika, pia hii itumie hatakama unahakika mhusika amefariki mbali na hospital, kidogo inatoa faraja mtu kusikia ndugu yake yupo hospitali hatakama anahali mbaya.
Mkuuu kuna mama mmoja alikua anaambiwa mwanae kagongwa na gari kaumia ila ni mzima..ile kupewa taarifa akawa anasema KWA SAUTI huku analia...Mnanidanganya mwanangu KAFA uwiiiii mwanangu mimi KAFARIKI (hapo mtu hata hajafariki) unafkiri inakuaje hiyo kama ingekua n kafariki kweli alafu ukaamua umzuge kwa kumuanzia mbali????
 
Nakumbuka nilienda mahali flani wakati wakupiga story alitokea kijana mmoja akaja kuleta taarifa ya msiba wa mama wa mtoto niliye kua nikiongea nae,pale pale yule mama alipata presha akadondoka nae Akafariki..

sasa najaribu kuwaza ni mbinu gani inafaa kwa mtu aliyefiwa na mume/mzazi/mtoto/ndugu halafu sisi majirani au ndugu tuweze kumfikishia taarifa kwa muhusika bila kusababisha Kifo kingine?

Msiba wa bibi yangu mzaa mama nakumbuka mleta Taarifa alinikuta nikiwa na mama..akamwambia mama kua BIBI kafariki Sitosahau kile kibao alichopokea yule kaka,hakugeuka nyuma aliondoka na hakurudi tena Ila ndio hivyo taarifa ikawa ishafika...sasa mama kama nae angekua na matatizo ya presha presha kwa jinsi mletaa taaarifa alivyoileta nadhani tungepata MSIBA mwingine.

NINI KIFANYIKE KATIKA KUFIKISHA TAARIFA KWA NJIA YA USALAMA??
Siku hiyo mkishapata habari kamili mnaenda mnamsaidia kila kazi anayofanya akitaka kwenda sehemu mzuieni mwambie asiende kuna wageni alafu andaeni mazingira ya hapo kwake kama kufagia kumwoshea vyombo kufua mpikieni wakati shughuli inaendelea yeye mwenyewe kuna kitu kama atashtuka hivi maana kadri mda unavyoenda atazidi kuwa na hofu kuna namna sii bure..wakati mkonhivyo hakikisheni yule anaekuja kama amewakuta nyie mwiteni pembeni mumkalishe kwanza maana anaweza kuropoka au kuanza kuoiga mayowe kabla..
 
Unamwambia fulani ameenda kuungana na malaika wanaimba na kusifu kwa furaha kwa Baba juu
 
Back
Top Bottom