Mbinu chafu za serikali kuficha ukweli juu ya Dr. Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu chafu za serikali kuficha ukweli juu ya Dr. Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by de'levis, Jun 29, 2012.

 1. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna mbinu chafu zinapangwa katika kuficha ukweli wa kile kilichotokea kwa dr. Ulimboka. Mbinu hizi zinalenga kuficha maovu yaliyofanywa na serikali kwa dr ulimboka na hivyo kuisafisha serikali ili ionekane kuwa haihusiki na unyama huu.

  Mtu aliyekuwa anajitambulsha kwa dr. Ulimboka na kuwa na mawasilinao nae kwa mda mrefu akitumia jina la Abduel (si jina lake halisi na wengine humuita abedi) alikabidhiwa kazi ya kumfatilia dr ulimboka siku mbili baada ya waziri mkuu pinda kwenda kuonana na madaktari pale Muhimbili. Kitu cha kwanza alichofanya ni kujiweka karibu na ulimboka katika kuzungumzia matatizo yao lakini pia huyu jamaa alikuwa link kati ya ulimboka na serikali. Katika kipindi chote hicho mwanausalama huyu likuwa akimfatilia ulimboka ili kumjua kwa undani zaidi.

  Baada ya kuona msimamo wa dr ulimboka juu ya swala hili la madaktari hautetereki na habadiri msimamo wake maana walishataka kumpatia pesa ili anyamaze ; ndipo sasa maandalizi ya kumnyamazisha kwa kutumia formula ya ’’ maiti haisemi’’ yalianza. Lengo lilikuwa ni kumuua kabisa na hiyo juzi walidhani wamemuua.wazo la kumnyamazisha jumla ulimboka halikutoka kwa huyo mwana usalama bali nae alipokea maelezo toka juu kwa watawala. Mpango wa kutekwa ulimboka ulipangwa na kitengo anachofanyia kazi mwana usalama huyo na kutekelezwa na maafisa wapolisi waliokabidhiwa jukumu hilo.

  MBINU CHAFU
  Baada ya kufanikiwa kumteka na kumpiga vibaya dr ulimboka na hatimae kumtupa huko msitu wa pande huku wakidhani tayari adhma imetimia ya kumtoa uhai sasa serikali dhaifu imepanga mipango michafu ili kujisafisha ili isionekane kuwa imehusika na unyama huu.


  1. Abduel amesafirishwa na kuondolewa nchini Tanzania usiku wa tarehe 27 kwa kupita Nairobi na baadae ataelekea kwenye ubalozi wa afrika ya kusini atakapopangiwa majukumu mengine. Hii yote ni katika kuficha ukweli . hao maafisa wa polisi watano waliomteka ulimboka wapo nchini na mmoja amewekwa kwenye tume ya kuchunguza utekwaji nyara wake iliyoundwa na kova nahii imefanywa makusudi kwa malengo flani; wanne waliobaki wamesambazwa kwenda mikoan na hawapo dar.


  2. Kamanda wa polisi kova ameelekezwa KUHAKIKISHA anailinda serikali katika jambo hili na afanye awezalo kuonyesha umma wawatanzia kuwa serikali haihusiki na jambo hili.katika kuficha na kuilinda serikali kova, mwema na maafisa wa wajuu wa usalama wa taifa walishauliana ili kuilinda serikali na kadhia hii mahabusu 5 wenye makosa ya ujambazi wanahitajika kutoka katika magereza yaliyopo mwanza, songea, tabora, tanga na kigoma waletwe dar ili hao waweze kuonyeshwa kwenye vyombo ya habari kuwa ni majambazi yaliyomteka ulimboka na kumpiga. wakishapatikana wataonyeshwa kwenye vyombo vya habari na umma wa watanzania utaambiwa kuwa wale ndio walifanya unyama huo wako chini ya ulinzi na kuwa maohojiano yanaelendelea na uchunguzi ukikamilika watapelekwa mahakamani na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mchezo.
  3. mbinu nyingine ni kuwa mahabusu hao wasafirishwe hadi pwani na wauwawe wote na taarifa itoke kuwa ndio waliomteka dr ulimboka na wamekamatwa wakiwa mkoa wa pwani katika msako mkali wa jeshi la polisi. Na katika kujibizana risasi polis ilifanikiwa kuwaua majambazi hayo. Na hapo ndo itakuwa mwisho wa swala hili na serikali itakuwa imenawa mikono na kujisafisha

  Kwa sasa kinachofanyika ni kuwasiliana na magereza husika ili kila gereza litoe mtu mmoja (mahabusu) atakayesafirishwa hadi dar/pwani na wataunganishwa kisha kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari wakiwa hai au maiti ili kuuaminisha umma kuwa wao ndio walimvamia dr.ulimboka
  Upelelezi na uchunguzi unaofanyika sasa ni changa la macho kwa watanznai na hiyo tume aliyoiunda kova nayo ni changa la macho ,na kama ulimboka alifanikiwa kuwaona vizuri na kuzishika sura zao ,mmoja wao yupo katika kamati hiyo. hakuna uchunguzi wowote utakaofanyika wenye tija kwa taifa juu ya kilichotokea.Kamanda Kova anasimamia operation hii na ameambiwa HAKIKISHA serikali inasafishika.

  Mazingira yote yanayoihusisha serikali kwa watu wake kufanya ushenzi kuna jitihada kubwa inafanyika ili kufuta dhana hiyo. Si maraya kwanza kwa serikali kuua watu inaowaona ni mwiba kwake. Wapo wengi na wengi wamezikwa kwenye msitu huo wa pande, kuna msitu uko kibaha(kama uamzi wa kuwaua mahabusu utakubaliwa basi watauliwa kwenye msitu huo) na wengine hutupwa baharini .
  Kusamilika kwa ulimboka ni kuwa Mungu ana mpango nae na serikali inafanya kila linalowezekana kujinasua. si wote serikalini wamefurahishwa na kilichotokea wengine wamechukia tena sana
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  ndio unyama huu wanaupanga?!! asante de'levis kwa taarifa
   
 3. L

  Lorah JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kiruuuuuuuuuuuuuuuu.......
   
 4. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,041
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kumbee
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nakuaminia de'levis. Kupona kwa Dr Ulimboka ni mpango wa Mungu. hawa jamaa walifikiri wamemaliza kazi. Hii serikali ianafanya mambo yaliyofanywa na Amini miaka ya 70. Shame on them. Dr aueleze umma yaliyotokea.
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ee mungu mwema ingilia kati utuokoe.
  Inasikitisha sana.
   
 7. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  de'levis ,nakuamini sana kwa taarifa za ndani.

   
 8. K

  Konya JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mungu hamtupi mja wake na wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine mpaka kufanikisha hili tukio Mungu awaadhibu zaidi ya kile walichodhamiria kumfanyia huyu jamaa
   
 9. J

  John W. Mlacha Verified User

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  sasa hao mahabusu wamewakosea nini tena? Kweli serikali dhaifuu
   
 10. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  No comment
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kuna kitu kimoja hawa wahusika wa utekaji hawaelewi, au hawataki kuelewa... Hawataweza kupambana na Mungu... Mwenyezi ameshaamua kuwaumbua, na katika hili hakuna hata tone moja la haki litapotea. Mi nawashauri tu kitu kimoja.... They have to commit suicide... Wajiue...
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana kwa taarifa de'levis kwa moyo wako wa uzalendo Mungu atakusimamia ,Ili mradi waandishi nao ni wana JF watumie hii taarifa kuwaumbua serikali wawapigie simu wawaulize huo mpango wao wa kuuendelea kuua wananchi wasio na hatia
   
 13. j

  jigoku JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa,na kwa msingi huu umoja wa kitaifa unahitajika, mshikamano wa wananchi unahitajika hasa wale tunaopingana na unyama kama huu.

  Nguvu ya umma inahitajika,tushirikiane sote kwa kufichua mbinu chafu zinazopangwa za kufanya uonevu na hata za kuendelea kutaka kumdhulu Dr Ulimboka na wengine wote,lakini pia tutumie nguvu ya umma kukataa unyanyasaji wa wananchi.

  Tukatae kuonewa, tukatae kupewa huduma mbovu kutoka serikalini ambazo ni kwa kodi zetu na rasilimali zetu,tuungane pamoja kuikomboa nchi hii,tuing'oe serikali dhalimu ya CCM
   
 14. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inawezekana kabisa!...ngoja nami niendelee kufukua fukua kwa ma-sources,..baadae.
   
 15. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Hii thread imfikie mkuu wa Kaya, Mwema, Kova na waTZ woote wajue unyama huu.
   
 16. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi hawa watu wanaojiona kuwa wao ndio serikali sana wataendelea kuua watanzania mpaka lini? Hata kama ni majambazi (kwa kutuhumiwa au kuhukumiwa) serikali haina haki ya kuwaua. Hizo mbinu zao chafu na za kijinga hazitawasafisha hata kidogo zaidi ya kuendelea kuongeza hasira kwa wananchi. Kwa kweli hata kama haijathibitishwa, kwa hili la Dr. Ulimboka, nasema wazi ninaichukia hii serikali!

  Mkuu de'levis ukae ukijua kuwa kwa kuyaweka haya yote wazi, maharamia hao (maana tunajua wapo humu na wamekusoma) watabadilisha mbinu za namna ya kujisafisha. Endelea kufuatilia kwa karibu na utagundua hilo. Ila pia uzuri ni kwamba huwa hawatumii akili na hivyo wataumbuka tu kwa kila ushenzi wanaoufanya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ninasikia Mkuu leo amewa summon Baraza la usalama wa Taifa, anataka maelezo ya kina kwanini mpango wa kumuua Dr. Ulimboka uli fail?

  Hata wakitumia hiyo mbinu ya kuleta majambazi kutoka magereza sura ya Abeid Ofisa usalama wa IKULU inafahamika kwa madaktari wengi walioko kwenye timu ya majadiliano including Dr. Deo. Huyo Askari aliyewekwa na Kova kwenye tume tunamjua kwa jina na sura Hemedi Msangi.

  Ninakwambia kwa hili serikali imekula kwao. The last option walionayo serikali wataanza kuwauwa wote waliotumwa na kushindwa kuafanikisha operation hiyo akina Abeid, Hemedi Msangi na askari hao wengine wanne. Serikali imekuwa ya kigaidi.
   
 18. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr. Hamis Kigwangala amesema atawasomea dua wote waliofanya kitendo hicho hadi wafe, sasa kwa mazingira haya dua itasomwa kweli kama wauji wenyewe ni chama chake??
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mkuu uko sahihi kabisa tuungane lakini kuna watu kama zomba hawawezi kuelewa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Yarabi Mtume Muhamad na Yesu Kristo tunusuru na hili janga la kimafia
   
Loading...