Mbinu chafu 56 JK alitumia kushinda uchanguzi 2005

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Mbinu chafu JK alitumia kushinda uchanguzi 2005,
wananchi wangelipenda kujua mbinu zilizo tumia kwa CCM kushinda uchanguzi wa mwaka 2005 zikiwemo kile kilichoitwa ukatili kufa au kupona SALIM H. SALIM alihusishwa kumuuwa Rais wa zamani wa Zanzibar ABEID KARUME, ambayo ilitolewa kwenye magazeti likiwepo GAZETI MWANANCHI.

na aliye kuwa muhariri wa gazeti hilo BW.SAID NGUBA ndiye mwandishi wa waziri mkuu, fadhila hiyo..

mara mbili ukurasa wakwanza, MALECELA,BILALI kutolewa kimabavu, , kutumia BBC RADIO, na mengine mengi hiyo ni mifano tu ziko mbinu chafu zaidi 56 walitumia kushinda WanaJF zijazieni mpaka zifikie au na zaidi, ikiwepo kuiba kura, kuwamaliza upizanani, Ahadi na mikataba waliyo siini, ya mahoteli.kuwaujumu watu wasiyo waunga mkono,

jamani wanajambo mnayajua yawekeni hapa yote ili wasirudie 2010 iwe ni mwanzo na mwisho.

WEKENI HIZO MBINU ZOTE HAPA .
 
Mbinu chafu JK alitumia kushinda uchanguzi 2005,
jamani wanajambo mnayajua yawekeni hapa yote ili wasirudie 2010 iwe ni mwanzao na mwisho.

WEKENI HIZO MBINU ZOTE HAPA .

Ninayo ijua mimi ni kalamu kupitia vyombo vya habri.

Hii ikiongozwa na spinn master RA. aliwanunua wahariri na waandishi mbali mbali akiwemo Salva R. aliyetunukiwa cheo cha asante juziikulu, kuwapakazia kinoma washindani wake, hasa Sumaye kwa kumfanya aonekane ni mwizi mkubwa mbele ya macho ya Watanzania, kitu ambacho mpaka sasa hakija thibitika, na badala yake kumbe mwizi mkubwa alikuwa bosi wake chenkapa!
 
..aliyeongoza kitengo cha ujasusi wa propaganda na mbinu chafu...ni bernard cammillius membe..majeruhi wa kwanza akiwa bosi wake wa zamani usalama na ubalozini canada..dr kitine,akafuatia iddi simba,DR salim ahmed salim..sumaye alikabiliwa na lowassa mwenyewe akisaidiana na mkurugenzi wa sasa wa PCB, na ndio maana baraza la mawaziri lilipotajwa membe alipopewa unaibu waziri alizusha mgogoro mkubwa ndani ya mtandao akisisitiza kwa kazi kubwa aliyofanya hakustahili kugawiwa cheo kidogo.....cheo alichotegemea tangu mwanzo ni hiki cha waziri wa mambo ya nje.......
 
HABARI HII NI YA KUTOKA 'TANZANIA DAIMA'


Halahala Kikwete nchi inakuharibikia!


Na Absalom Kibanda

RAIS Jakaya Kikwete amerejea kutoka ziara ndefu ya kikazi katika nchi rafiki kihistoria, za Scandinavia, iliyomchukua siku kadhaa.

Bila shaka ni dhahiri kuwa kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kusafiri nje ya nchi sasa anaweza akasimama kifua mbele kuwaeleza Watanzania wenzake mafanikio ya kweli yaliyotokana na safari yake hiyo, tofauti na nyingine zilizotangulia.

Kikubwa katika ziara yake hiyo ni namna alivyoweza kuwashawishi viongozi wa Serikali ya Denmark ambayo miezi michache tu iliyopita walitangaza kusitisha asilimia 20 ya misaada yao kwa Tanzania kwa sababu ya kile walichokielezea kuwa ni kutoridhishwa kwao na kasi ya mapambano ya rushwa.

Akiwa katika nchi hiyo ambayo kihistoria kupitia katika Shirika lake la DANIDA imefanya kazi nyingi nyeti, kubwa kati ya hizo ikiwa ni ile ya miaka ya 1980 na 1990 ya kuzikarabati upya takriban shule zote za sekondari zinazomilikiwa na serikali ambazo zilianza kuonekana kuwa magofu.

Pengine akijua umuhimu wa Denmark kwa Tanzania na athari za uamuzi wa nchi hiyo kupunguza misaada yake kwetu, Kikwete aliifanya nchi hiyo kuwa ya mwisho katika ziara yake hiyo na siku ya mwisho akiwa huko akatoa tamko moja zito ambalo lengo lake lilikuwa rahisi; kuipotosha jumuiya ya kimataifa.

Akizungumza na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa, wa nchi hiyo, Ulla Termaes, Kikwete alijikuta akilazimika kutoa kauli ya utetezi pale alipotakiwa kueleza sababu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni mwenyekiti wake, kulaumiwa kwa kuua upinzani.

Mwandishi wake wa habari amemkariri akimweleza waziri huyo wa Denmark kuwa, CCM haina sababu ya kuua upinzani kwa kuwa inauhitaji sana.

Alikwenda mbali zaidi na kusema wapinzani wamekuwa wakishindwa wenyewe kwa sababu ya kukosa sera mbadala, na kwamba wamekuwa hawajiandai vya kutosha kukabiliana na CCM, chama chenye mizizi ya kihistoria.

Hakuishia hapo, bali aliamua kutumia mfano wake yeye mwenyewe akisema kuwa, alijiandaa kwa miaka 10 (tangu mwaka 1995) ili kujihakikishia ushindi katika kiti cha urais mwaka 2005.

Nilipoisoma habari hiyo, nilikubaliana na Kikwete katika hili la mwisho la maandalizi yake ya miaka 10 ya urais, japokuwa mara moja nilikumbuka kauli ya Baba wa Taifa ya mwaka 1995 aliyetuonya Watanzania kuwa makini na watu wanaofanya kila wanaloweza kukimbilia ikulu na akataka tuwaulize wanakimbilia huko kufanya biashara gani?

Kwa hakika maneno hayo ya Mwalimu yana maana sana leo hii, Kikwete anapokiri mwenyewe kuwa alianza kuitafuta ikulu miaka 10 iliyopita, ilhali zaidi ya mwaka mmoja na ushei tangu alipoingia ikulu ni shida kusema kwa hakika ni hazina gani ya mambo aliyokuwa ameyabeba kwa miaka hiyo 10 ya maandalizi.

Ingawa ni kweli dalili za maandalizi ya miaka 10 zilianza kuonekana mapema kabisa hata kabla ya joto la uchaguzi kupanda, kilichojidhihirisha wakati wote huo kilikuwa ni kile ambacho vijana wa mjini hivi sasa wanakiita ‘fitna’ dhidi ya wanasiasa ambao walionekana kuwa tishio dhidi ya kundi la mtandao na mgombea wao Kikwete.

Kwa maneno mengine, maandalizi ya miaka 10 ya Kikwete kuingia ikulu yalikwenda sambamba na azima ya kwelikweli ya kuua makali ya upinzani, kuanzia ndani ya CCM hata kabla hawajaanza kuuzika ule wa kutoka katika vyama vingine vya siasa.

Watanzania sasa wanapaswa kujua kwamba, maaandalizi hayo ya miaka 10 ndiyo yaliyowaondoa katika tanuru kuu la maamuzi ya kiserikali (Baraza la Mawaziri), wanasiasa wasomi waliokuwa na ushawishi mkubwa kwa Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wa wakati huo.

Maandalizi hayo ya miaka 10 ndiyo yaliyowaondoa kwa kashfa za kusukwasukwa za kweli na za kupikwa za kina, Dk. Hassy Kitine, Profesa Simon Mbilinyi na baadaye Iddi Simba.

Dhambi kubwa ya wanasiasa hao wasomi, ilikuwa ni ukaribu wao kikazi na namna walivyokuwa wakisikilizwa na Mkapa katika mambo mengi muhimu.

Kundi ambalo baadaye lilikuja kujulikana kwa jina la wanamtandao wakati huo likifanya kazi za chini chini, likiwatumia waandishi wa habari na wabunge machachari wa aina ya kina Chrisant Mzindakaya na wengineo, lilifanikiwa kuwang’oa katika uongozi wanasiasa hao ambao walijikuta wakianguka pasipo kujua ngumi iliyowapiga.

Hulka hii ya kuua upinzani haikuishia hapo; Augustine Mrema, ambaye bado alionekana kuwa tishio baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 naye alianza kushughulikiwa kwa namna ambayo ukitafakari leo hii unaweza ukaielewa vyema.

Pasipo kujua kuwa Dk. Masumbuko Lamwai alikuwa pandikizi la kisiasa la CCM ndani ya NCCR Mageuzi, Mrema ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa Temeke alijikuta akitegewa sakata la sh milioni 900, ambalo ghafla liligeuka kutoka kuwa kashfa ya vigogo ndani ya CCM na kuwa uongo wa aibu dhidi ya mwanasiasa huyo ambaye ushawishi wake ulimwezesha kupata asilimia 28 ya kura zote za urais mwaka 1995.

Huku wakijua kuwa mwanasiasa huyo angeweza kuiletea CCM matatizo makubwa siku za usoni, majemedari wa mtandao wakitumia makosa ya Mrema mwenyewe na mamluki kadhaa waliokuwa ndani ya NCCR Mageuzi na baadaye TLP, walifanya kila waliloweza kummaliza kabisa kisiasa.

Hoja kali dhidi ya Mrema zilizojengwa ndani ya Bunge na wanasiasa kama Edward Lowassa wakati wa kashfa yake ya sh milioni 900 ziliendelea kumtafuna Mrema taratibu kabla ya kummaliza hata kabla ya mwaka 2000.

Wakitumia kofia za CCM, genge hilo hilo, lilielekeza mashambulizi yao makali dhidi ya Chama cha Wananachi (CUF), kwanza kikavishwa kilemba cha udini na baadaye ugaidi kabla ya kubomolewa na kukifanya huko visiwani kionekane kuwa chama cha Wapemba na kitaifa kikachukua sura ya Kizanzibari.

CHADEMA wao wakavishwa taji la ukabila. Huku wakijua walifanyalo, wana CCM wakakiita chama cha Wachaga. NCCR ikauawa na baadaye TLP.

Vijogoo kadhaa wa upinzani wakarejeshwa CCM kwa bei ambayo siri yake bado haijafichuka. Kina Chifu Abdallah Fundikira, Daniel Nswanzugwanko na Lamwai (kwa kuwataja wachache) wakaongoza kundi hilo, kila mmoja akipewa ‘kishughuli’ cha kufanya.

Staili hiyo hiyo iliyotumiwa na kina Mkapa, Malecela na Philip Mangula kuua upinzani ndiyo ambayo leo hii imetumiwa na kina Kikwete, Lowassa na Yussuf Makamba kuwarubuni kina Tambwe Hizza, Amani Walid Kabourou na wengine wengi waliorejea CCM. Halafu rais huyo huyo anawaambia Wazungu eti sisi hatuui upinzani!

Turejee kwenye historia ya operesheni za siri za wanamtandao. Ajenda mahususi iliyofanywa na mashushushu wa mtandao waliosomeshwa na serikali kile kinachojulikana kama ‘strategic studies’ ndiyo ambayo katika kipindi cha miaka 10 ya maandalizi ya urais wa Kikwete imefanikisha kuharibu sehemu kubwa ya matishio ndani na nje ya CCM.

Historia inaonyesha kwamba, katika kipindi hicho cha mwaka 1995 na 2005, orodha ya matishio haikukoma. Kadiri muda ulivyozidi kusonga mbele ndivyo maadui wengine kadhaa walivyozidi kuibuka ndani ya CCM na nje.

Ndani ya CCM wakaibuka watu wa aina ya John Magufuli, Frederick Sumaye na Profesa Mark Mwandosya ambao nao kila mmoja kwa wakati wake akatafutiwa panga la kukatia ‘shingo’ lake kisiasa.

Kwa bahati mbaya, kila mmoja wa hao kwa kutojua vyema harakati za kundi hilo la mtandao wakajikuta wakijiingiza katika mtego. Magufuli akaponzwa na maamuzi yake ya zima moto, akajitwisha mzigo mzito wa lawama na akapoteza hali ya kutoaminiwa na wananchi, akijengewa hoja za kuonekana kuwa mtu wa kukurupuka.

Sumaye yeye akajikuta akilemewa na dhambi za kihistoria za wadhifa wake wa uwaziri mkuu. Kila alilolifanya likakosolewa, kila kauli yake ikawekwa katika kikaango, kila maamuzi yake yakapingwa na akapekuliwa kwelikweli kiasi cha kupoteza taswira ya kiongozi makini.

Frederick Sumaye ambaye wakati akiingia madarakani alipambwa kwa sifa nyingi za uchapaji kazi usiomithilika na vyombo kadhaa vya habari, akamaliza kazi akionekana mtu asiyefaa kabisa na asiye na uwezo wa kuongoza, na hoja za kumkashifu na kumchafua zikaongozwa na wale wale waliompamba wakati alipoteuliwa.

Kiboko kilichompiga Sumaye kikamchapa pia Mwandosya. Akahusishwa na uuzwaji mbaya kabisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), akatajwa kuhongwa na wawekezaji walionunua kampuni hiyo kwa kumpa kazi mwanawe na mwisho akadaiwa kuchangisha fedha za chama ilhali akiwa si mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) au uongozi mwingine wowote katika chama.

Orodha ya maadui wa mtandao ikawa ikiongezeka kila mara: Wakaingizwa pia kina John Malecela na Dk. Salim Ahmed Salim. Kila mmoja akapigwa na kombora lake, tena chini ya mkanda na walipojaribu kufurukuta wakakwama.

Kila mmoja wa hao alikufa kisiasa katika ngazi yake. Wale wa kundi la kwanza (kina Kitine, Simba na Mbilinyi) waliondoka mapema kabisa, wakabaki hao wa kundi la mwisho.

Wakijua hatari iliyokuwa mbele yao, wanamtandao wakapata fomula moja nzito na kubwa kweli kweli. Wakapenyeza ruba sehemu nyeti kabisa. Wakahakikisha wanawanasa watu walioshika turufu ya ushindi wao.

Harakati hizi walianza miaka takriban mitano au sita hivi kabla ya mwaka 2005. Kwanza wakamuunga mkono Mkapa kuhakikisha kuwa mgombea wake, Amani Abeid Karume, anashinda urais Zanzibar dhidi ya kundi gumu la aliyekuwa Rais wa Zanzibar hadi mwaka 2000, Dk. Salmin Amour Juma aliyekuwa akimuunga mkono, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Kikwete, Lowassa na Rostam Aziz, wanasiasa watatu vigogo wa mtandao wakaonekana wakiwa bega kwa bega na Karume. Hakuna siri kwamba wao ndio waliomfanyia kazi Mkapa ya kumshindisha Karume ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Tuliokuwapo Dodoma wakati huo tunajua. Kura za NEC zilipigwa mapema na wanamtandao wakajihakikishia ushindi mbele yetu, tena wakitaja idadi ya kura atakazopata Karume hata kabla mkutano (NEC) haujaanza. Baadhi yetu hawakujua kuwa hayo yalikuwa ni sehemu tu ya maandalizi ya miaka 10 ya Kikwete.

Huo ukawa msingi mkuu wa mahusiano ya kundi la Kikwete na Mkapa ambaye kwa hakika kwa mara ya kwanza akaona fahari kuwa na vijana wanaomtii. Sijui kama alijua kuwa hayo yalikuwa maandalizi yao ya urais miaka mitano ijayo na wala hawakumuunga mkono kwa sababu nyingine yoyote.

Ili kujihakikishia ukaribu na Mkapa, kundi hilo likafanya jambo moja kubwa. Wakawatafuta watu ambao Mkapa alikuwa akiwaamini sana. Wakawaingiza katika orodha ya maandalizi hayo.

Kundi hilo lilijumuisha watu wengi. Likamfikia Ferdinand Ruhinda, rafiki na mwenza wa kweli na wa siku nyingi wa Mkapa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970. wakafanya urafiki wa kuaminiana na mzee Kingunge Ngombale- Mwiru na baadaye wakaweza kuwa watoto wema wa mzee Rashid Kawawa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Walipoweza kuwapata wote hao wakawa na uhakika kwamba safari ya ushindi ilikuwa imeshakamilika. Kwa bahati mbaya wakati yote haya yakifanyika, kina Sumaye, Salim, Mwandosya, Malecela, Mangula na wengine walikuwa wamejisahau na waliposhtuka wakajikuta wameshachelewa.

Katika kipindi chote hicho cha miaka 10, kundi hilo likafanikiwa kupenya mioyo dhaifu ya sisi waandishi wa habari. Wengine wakatuajiri katika makampuni yao na wengine wakawafanya marafiki wa karibu na wenzi katika harakati, yaani makomredi.

Katika kipindi cha hiyo miaka 10, halikuwa jambo rahisi (japo ilitokea mara chache) kuwapo kwa habari mbaya zilizowahusu Kikwete na Lowassa, magazetini, hadi mwaka 2001 wakati mahasimu wao kwa mara ya kwanza walipounganisha nguvu na kujaribu kuwaangusha katika kura za kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Hilo ndilo lilikuwa tishio pekee kubwa dhidi ya mtandao katika kipindi chote hicho cha maandalizi ya miaka 10 ya Kikwete na wanamtandao wenzake.

Huku wakijua kuwa tukio hilo baya lilikuwa halina budi kusafishwa. Wakatafuta jawabu la tatizo hili. Wakajiimarisha kwelikweli na wakatumia vyombo vya habari kuonyesha kuwa matokeo ya ujumbe wa NEC ambayo aliyepata kura nyingi katika kundi lao alikuwa Sumaye, yalikuwa ya ‘kiitifaki.’

Makala zilizosheheni hoja nzito dhidi ya uchaguzi huo zikaanishwa, ikaonekana dhahiri kuwa, wingi wa kura za kina Sumaye, Shein na wengine zilipigwa kiitifaki na kwamba kulikuwa na mchezo mchafu uliochezwa. Kwa kweli wakapita kiunzi hiki pia.

Tangu wakati huo, kundi hili likatangaza rasmi vita dhidi ya wanaitifaki hao. Vijana wa CCM wakiongozwa na viongozi wao, wengi wao wakajikuta wakiwa sehemu ya mtandao na wachache waliobaki wakaonekana kuwa maadui wakubwa wa kundi hilo.

Sumaye, Mwandosya, Idd Simba, Malecela, Abdallah Kigoda na wengine wengi wakajikuta wakipigwa kwenye matanuri ya tuhuma zisizoisha.

Pengine kwa kutojua athari za tuhuma nzito zilizoelekezwa kwao na maandalizi makubwa ya kundi hilo la mtandao wanasiasa hao na wengine wakajiingiza kwa mbwembwe kujaribu kuupata urais kupitia CCM wakakwama. Hawakujua kuwa Kikwete alikuwa amejiandaa kwa miaka 10.

Maandalizi ya miaka 10 yalipofanikiwa ndani ya CCM yakageuka dhidi ya kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, Augustine Mrema na wengine na kila aliyejaribu kufurukuta akakutana na panga zito la maandalizi ya miaka 10 ya Kikwete.

Leo mwaka mmoja na ushei baada ya ushindi wa kishindo wa asilimia 80, Watanzania wanasubiri kwa hamu kuona matunda ya hayo maandalizi ya miaka 10 ya Kikwete. Wanasubiri kutimizwa kwa kaulimbiu yenye utata ya Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.

Kwa hakika kabisa hakuna anayeweza akasema serikali hii imekuja na jipya ambalo lilimshinda Mkapa. Hakuna anayeweza kusema kwamba, kaulimbiu ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’ imeshaanza kuonyesha dalili zozote za wazi.

Hakuna anayeweza akasema kwamba, maandalizi ya miaka 10 yalimwandaa vya kutosha Kikwete kiasi cha kuwa na dira mbadala kisera, kifalsafa na kimkakati kulinganisha na yale tuliyoyazoea.

Tofauti zinazoonekana sasa ni kuondolewa kwa wamachinga mitaani, huku umachinga wenyewe ukiendelea kuota mizizi. Ongezeko la maneno mengi ya viongozi yasiyo na vitendo vya wazi, kukithiri kwa semina elekezi kwa wakuu wa wilaya na mikoa ambazo aghalabu matunda yake huenda yameonekana katika vyumba vya madarasa pekee huku elimu ikibakia kuwa ni ile ile.

Kinachoonekena ni tishio kubwa la kuwa na walimu wa kutosha wa kuwafundisha hao watoto wanaojengewa madarasa mengi zaidi hata kusababisha serikali kuamua kuendesha ‘crash programs’ za miezi michache.

Ni jambo la ajabu kwamba wakati miaka 10 tu iliyopita wataalamu wa elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliamua kuifanya kozi ya ualimu kusomewa kwa miaka minne kutoka mitatu ya zamani, leo hii serikali ya CCM inawaandaa walimu wa sekondari kwa miezi isiyozidi mitatu tu.

Ingawa operesheni hii inaonekana kuwa chachu ya kuwapa ajira vijana wasio na kazi, lakini japo kwa hatua nyingine inayarejesha makosa tuliyofanya miaka ya 1970 wakati wa Elimu kwa Wote (UPE), mkakati uliowaajiri walimu wengi wa shule za msingi waliokuwa na elimu hiyo hiyo ya msingi. Hii ni Ari Mpya ya namna gani!

Wakati serikali ikiporomosha viwango vya elimu ya ualimu, serikali hiyo hiyo inaandaa Muswada wa Habari ambao unataka kuwawekea waandishi wa habari viwango vya kitaaluma. Hivi hii Kasi Mpya inaelekea wapi!

Kwa maneno rahisi kabisa, Kikwete anapaswa kutuonyesha Watanzania matunda ya maandalizi yake ya miaka 10 ya kujiandaa kuwa Rais wa Nne wa Tanzania, muda ambao hawajapata kuwa nao marais wote watatu waliomtangulia. Hakika Watanzania wanataka kuipima hiyo Nguvu Mpya.
 
me ninyo hisi iliyokuwa na nguvu zaidi ni ile ya nguvu ya giza..mapete yale na timu ya ufundi aliyokua akitembea nayo hata kule alipokua akito hotuba kidooogo azidiwe kete na yule jamaa lakini timu yake was strong..ika msave..
siku ile jangwania alipoanguka yasemekana hamna lolote ni tiba tuu ziliingiliana na kuzidiana kete wakamuwahisha bagamoyo kupewa first aid ya kijadi..kutoka kwenye ile ile timu yake ya ufundi ambayo kama ilivyo kwa Maximo nayo nasikia ilikua imported from west Africa as yasemekana huko ndo brazil ya nguvu hizo za giza..
pia tujiulize swali ni kwanini hatuoni lolote analofanya huyu bwamdogo na mtu unaweza mcriticise kufa lakini akitokea kwenye screen tuu mtu unaweza hata sema c.c.m oyeeee au kidumu chama cha mapinduzi.....je ni kwa nini????kama sio nguvu za ziada??au ndo tuseme jamaa ana kismati??no way
 
Kwa maneno rahisi kabisa, Kikwete anapaswa kutuonyesha Watanzania matunda ya maandalizi yake ya miaka 10 ya kujiandaa kuwa Rais wa Nne wa Tanzania, muda ambao hawajapata kuwa nao marais wote watatu waliomtangulia. Hakika Watanzania wanataka kuipima hiyo Nguvu Mpya.

Mtupori.... asante sana kwa hii.... this is deep....

Muda si mrefu watu watajua kuwa wanamtandao hawaitakii mema nchi yetu..... It is bad kuwa mkoloni na mwizi Rostam Aziz amejipenyeza vilivyo kwenye media so watu wengi hawapati habari kama hizi BUT... soon GOD's willing mtandao wataface justice yao
 
Kundi hilo lilijumuisha watu wengi. Likamfikia Ferdinand Ruhinda, rafiki na mwenza wa kweli na wa siku nyingi wa Mkapa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.
Hapa mkuu umemsahau Mushi pia mshikaji wa karibu wa Mkapa, ambaye huyo mkuu alikuwa akikutania sana nyumbani kwake na yule Hawara yake wa maisha, Mama Rweyemamu, halafu ni Mkulu Ruhinda, ambaye Mtandao walimpa lile "FAILI" walilomkaba nalo koo Mkapa,

Halafu kuna siri mpya ambayo walikuwa wameificha kwa muda mrefu sana sasa inaanza kutoka, pia walimrubuni mkuu wa idara aliyestaafu, lakini ilikuwa ni siri yao kubwa sana, ila duniani hakuna siri, finally it is out there!

Heshima mbele mkuu kwa article nzito, yaani ndio Kumkoma Nyani Kwenyewe Mchana Kweupe!
 
Kwi kwi kwi!!!!!!!!!!!!!

Muungwana kakabwa kweli kweli. Atafute fall guy wake wa kumtumia kama kinga kama ambavyo Nyerere alivyokuwa na Kawawa.
 
....tatizo lowassa naye yuko ambitious hawezi kukubali kuwa "fall guy " au dodoki la muungwana kama vile kawawa kwa mwalimu na sumaye kwa mkapa....ndio tatizo la kuteuwana kwa mikataba..anapolijutia..
 
....tatizo lowassa naye yuko ambitious hawezi kukubali kuwa "fall guy " au dodoki la muungwana kama vile kawawa kwa mwalimu na sumaye kwa mkapa....ndio tatizo la kuteuwana kwa mikataba..anapolijutia..

mwisho unakaribia pia wengi wanasubiri kichama na kiimani...
 
Turejee kwenye mbinu chafu.

Mwaka 2005 nilijiandikisha katika kituo kimoja kule Arusha. kura zangu zote nilinielekeza upinzani. sitataja nani nilimpa urais hiyo bado ni siri yangu. kwa kuwa matokeo yalikuwa yakibadikwa, nami nilienda kuangalia. kwa mshangao wangu yule niliyepigia ilionyeshwa amepata sifuri ktk kituo kile. lakini cha ajabu sikuwa peke yangu niliyetoa malalamiko kama hayo.

Nilijaribu kutafuta sababu iliyopelekea matokeo yale na niligundua sababu kuu moja. kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walishinda njaa siku nzima pale kituoni ili hali wale wa ccm waliletewa chakula na viongozi wao. kilichotokea ni kwamba mtu mmoja (sina hakika kama alihusiana na chama gani) alifika mida ya jioni na kujifanya msamalia mwema kwa kuwapa pesa ili waende maeneo ya jirani wakapate chakula na warudi waendelee na zoezi la kuhesabu kura. muda huo ndiyo bao likapigwa.

Ushauri wangu ni kwamba, ili kushinda, ni lazima pia mawakala wawezeshwe, tena wawezeshwe vya kutosha. huko ndiko shina la hizo 80% za JK
 
ma-engineer wa mbinu chafu ni Kingunge na Rostam na mwingine mmoja nimemsahau wako watatu alikuwa ni balozi anaye mjua atutajie hapaJF
 
pia nikubaliane na mwenzangu wa hapo juu,mtandao walijitahidi sana kujiingiza katika ofisi nyeti(usalama wa taifa) na wakachukua watu wao pale ili wawafanyie kazi,na mmoja wa watu waliokamatwa na mtego huu ni mkurugenzi mkuu mstaafu wa idara hiyo,
 
anayejiita dr. NCHIMBi,huyu ndiye mnafiki mkubwa,alikuwa anachukua mambo ya kambi ya sumaye na anayepeleka kwa kina EL na MUUNGWANA,
na ilifikia akakodiwa chumba pale landmark..sikushangaa alipohusishwa na suala la marehemu AC sababu jibaba hili ni limbeya na linafiki,zaidi ya hapo ni wanaolazimisha phd zao kama dk mathayo,
huwezi kutegemea maamuzi ya maana kama cabinet imejaa watu wenye upeomfinyu,nawasiwasi huwa wanadiscus hata mambo ya twanga
 
kwenye siasa hakuna aliye msafi, sio JK, sio Mbowe, sio Mrema, sio Lipumba, sio nani ! wote wachafu, kama njama 56 alizotumia JK, basi kumbuka na wengine wengi kwenye siasa wana zao pia ila mmemshikilia bango tu Kikwete !
 
kwenye siasa hakuna aliye msafi, sio JK, sio Mbowe, sio Mrema, sio Lipumba, sio nani ! wote wachafu, kama njama 56 alizotumia JK, basi kumbuka na wengine wengi kwenye siasa wana zao pia ila mmemshikilia bango tu Kikwete !


tunamjadili kikwete kwa kuwa ndiye aliyetumia mbinu chafu kushinda....hata kama wapinzani walikuwa na mbinu chafu hazikuwasaidia..na ni kwa kiasi kidogo ambacho kwa umuhimu imetupasa kumjadili jk..

zaidi ya yote wengi tunalaani mbinu chafu ya aina yoyote regardless nani anaitumia...
 
tunamjadili kikwete kwa kuwa ndiye aliyetumia mbinu chafu kushinda....hata kama wapinzani walikuwa na mbinu chafu hazikuwasaidia..na ni kwa kiasi kidogo ambacho kwa umuhimu imetupasa kumjadili jk..

zaidi ya yote wengi tunalaani mbinu chafu ya aina yoyote regardless nani anaitumia...

PM nimekupata mkuu ! unataka kuniambia alitumia mbinu chafu halafu akakaa miguu juu na kutamaki akashinda ? jamaa kapiga kampeni, watu wakamkubali ! lazima tukubali kwamba wengi wa watanzania walikuwa wanamzimia JK kupita kiasi, yaani kama yeye binafsi alifanyiwa mbinu chafu 95, what do you expeect ? Wengi wa watanzania lazima tukubali 2005 walimkubali JK, sijui kwa 2010 ! kama mie ningekuwa nagombea urais chama cha upinzani 2005, kwa jinsi watanzania walivyokuwa wanampenda bila ya kumjua JK alivyo kiutawala, ningejitoa mwenyewe ! angalau jamaa meli imemueremea lakini alipendwa ! suala la kusema mbinu chafu ni kwa wale wanaofanya kampeni mapema kwa ajili ya 2010.
 
kwenye siasa hakuna aliye msafi, sio JK, sio Mbowe, sio Mrema, sio Lipumba, sio nani ! wote wachafu, kama njama 56 alizotumia JK, basi kumbuka na wengine wengi kwenye siasa wana zao pia ila mmemshikilia bango tu Kikwete !

mtetezi wa mafisadi! MWK tufanyizie tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom