Mbinu ambazo wafanyakazi wanatumia kuibia waajiri wao

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,789
2,000
Nchi yetu inasifika kwa kuwa na waajiri wasiowaaminifu. Hili mimi mwenyewe nimejionea. Sasa basi, ili kusaidia kukomesha hili tupeane mbinu ambazo wafanyakazi wanatumia kuibia waajiri wao. Weka kazi yoyote, uhasibu, ualimu, mabaa medi, fundi ujenzi, udereva nk.

Wizi sio lazima pesa, weka wezi wa muda, vitu nk.

Mimi nilichokiona.

Kuna dada alifungua duka la dawa, dogo tu. Binti aliyemuweka akawa anajumua dawa zake na kuziuza. Siku kamkagua begi lake akakuta dawa kibao. Tupeane mbinu.
 

Oswald Daudi Mwakibete

JF-Expert Member
Apr 16, 2018
1,163
2,000
Kuna wafanyakazi wa makampuni mengine wakifanya promotion ya brand mpya mara nyingi wanawaambia wauzaji wao watoe nyongeza ya bidhaa zikinunuliwa kiwango flani.Wanunuzi wanafikia hivyo viwango,wauzaji vile vya bure hawawapi wanunuzi,wanatia kunako mifuko yao!
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,786
2,000
Mimi nawasifu sana wafanyabiashara Tanzania biashara zao zinaenda vizuri kwa kuajiri watu. Ni ngumu biashara kwasababu ya wizi.

Hulka ya mtanzania ni wizi we are not honest at all.

Wamiliki wa shoprite wanasimulia ulimwengu hawajawahi kuona wizi wa ajabu kwenye chain zao zilizotapakaa Africa kama Tanzania.

Yani wafanyakazi wa Shoprite walikuwa wanawaita ndugu zao na marafiki kuja kufanya shopping na kupita bila kulipa. Halafu wakicheleweshewa mshahara wanaandamana.

Bakhresa wanavyomuibia mafuta kwenye matrela yani mibongo halafu mijizi yenyewe mimaskini.
 

mbenda said

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
510
1,000
Africa ktk watu 10 utakaowaajili 6 watakuibia 2 watashindwa kuiba kutokana na mazingira ya ofic na 1 aliobaki hataiba kwa uwoga alionao na mwingine hataiba kwa hofu ya mungu, hii inatokana na imani ya kuwa bila wizi hutoboi lkn pia mishahara midogo na ugumu wa maisha huchangia, mm boss wangu alikuwa ananiambia najua huwezi kufanya kazi bila kuiba lkn ukiiba angalia na kampuni nafamilia yangu maaana tunaendesha maisha yetu kupitia hapa iba kwa tahadhali
 

mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,682
2,000
Uzi wa majungu ya kimataifa...
Usilolijua wiz ni dunia nzima.. watu wanafanya ku legalize kwa kutumia wenye mamlaka..
Kama kaz ni yako just build system acha kuwehuka na mbinu za wizi....
Dunia nzima niulize biashara yeyote nikwambie wanaibaje.. wizi =biashara
Cocacola= selling sugary water
Tvs= selling ads
Pharma= selling drugs(not treating)
Politicians= selling drama
Weww fanya kaz, ukiona unaibiwa mfukuze huyo unaedhani anaekuibia acha majungu na hisia...
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,789
2,000
Mimi nawasifu sana wafanyabiashara Tanzania biashara zao zinaenda vizuri kwa kuajiri watu. Ni ngumu biashara kwasababu ya wizi.

Hulka ya mtanzania ni wizi we are not honest at all.

Wamiliki wa shoprite wanasimulia ulimwengu hawajawahi kuona wizi wa ajabu kwenye chain zao zilizotapakaa Africa kama Tanzania.

Yani wafanyakazi wa Shoprite walikuwa wanawaita ndugu zao na marafiki kuja kufanya shopping na kupita bila kulipa. Halafu wakicheleweshewa mshahara wanaandamana.

Bakhresa wanavyomuibia mafuta kwenye matrela yani mibongo halafu mijizi yenyewe mimaskini.
Ukipita njia kuu utakuta kila kwenye kamji kuna watu wanapiga dili za mafuta. Zamani treni zilikuwa zinasafirisha mafuta, walikoma. Watu walizivizia porini na kupiga dili.

Nasikia kwenye Ranchi za taifa watu ilikuwa mnyama akijifungua wanafaulisha ndama.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,922
2,000
Umasikini/Ufukara ndio chanzo kikubwa cha maovu mengi yenye kuhusisha udokozi...
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,778
2,000
Madukani huku pia baadhi sio waaminifu.

akiuza bidhaa yako yeye haandiki kauza, anachofanya anaenda kujumua mzigo kwa bei ya jumla, akiuza bidhaa anarudishia bidhaa hio kwa mzigo alionunua kwa jumla.

Hapa unakuta bidhaa zako zipo vile vile kila siku kumbe yeye akiuza bidhaa zako kwa bei ua juu anarudishia bidhaa zake alizonunua kwa bei ya jumla.

anaweza kuuza hata katoni 10 za bidhaa flani ila katoni zako mbili unazikuta vile vile tu bila mabadiliko huku yeye akiwa anapiga faida, inakuwa kama kapata frem ya bure kuuzia bidhaa zake.

Ukihisi hivi wewe tuma mtu anunue bidhaa zako alafu jioni nenda kahakikishe, ukiona mzigo haujapungua ujue huyo mwizi tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom