Mbinguni sio salama! Ni Propaganda tuu

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,722
2,000
USALAMA WA MBINGUNI BADO NI MDOGO

Na, Robert Heriel

Wakati Mungu anaumba Mradi wake wa Dunia aliumba kila kitu kikiwa chema kabisa. Hakuna ambacho kilikuwa na kasoro, kila kitu kilikuwa kimekamilika. Hivyo yeyote unayemuona hapa duniani ujue amekamilika yaani yuko full completely. Hii Propaganda ya kusema mwanadamu hajakamilika ni hila, njama, ulaghai wa viumbe wasio na asili ya binadamu.

Kabla sijaenda mbali, nieleze kwa kifupi namna Mradi huu wa Dunia ilivyoumbwa na Mungu. Mungu aliiumba dunia kwa mfumo wa kutegemeana (Ecosytem) yaani viumbe vinategemeana. Kutegemeana huku ndio kunakamilisha mradi mzima wa dunia. Katika Mradi huu kuna aina nyingi za viumbe kulingana na asili yao walivyoumbwa. Mathaalani; Wapo viumbe walioumbwa kwa Hewa, wapo walioumbwa kwa maji, wapo walioumbwa kwa moto, wapo walioumbwa kwa Mwanga/ nuru wapo walioumbwa kwa udongo, wapo walioumbwa kwa mchanganyiko wa mada zaidi ya moja yaani labada maji na udongo, au hewa na mwanga.

Hivyo naweza kusema viumbe wapo aina zifuatazo kulingana na malighafi zilizotumiwa kuwaumba;
1. Viumbe wa umaji
2. Viumbe wa Umoto
3. Viumbe wa Uhewa
4. Viumbe wa Udongo/umadini
5. Viumbe wa Unuru/umwanga
6. Viumbe waliochanganya malighafi kama mwanadamu ambaye amechanganya umaji(ikiwemo damu), udongo na uhewa(Roho) chochote kikipungua katika mchanganyiko huo basi maisha ya mwanadamu aypo mashakani.

Kila kiumbe kimepewa Miliki au ufalme wake na watakaokitumikia. Mwanadamu amepewa dunia, na vyote vilivyopo duniani ni mali yake na vinamtumiikia.

Nikirejea kwenye Mada.

Adamu aliumbwa Duniani ambapo kiasili ndio kwake. Baadaye Mungu Akamchukua huyo Mtu akampeleka (Edeni) ambapo kiasili sio Duniani. Kumbuka Adamu akitolewa Duniani kupelekwa Edeni alikuwa pekeake kwa mujibu wa maandiko.

Baadaye Mungu akamuumba Hawa/Eva kupitia ubavu wa Adamu. Hii ni kumaanisha Eva/Hawa aliumbiwa Edeni. Najaribu kufikiri na kugundua kuwa Eva ni matokeo ya mchangiko wa malighafi za dunia na Edeni. Kupitia Ubavu wa Adamu, Eva alijipatia malighafi za dunia(udongo) na kupitia malighafi zingine zilitoka pale pale Edeni. Nadhani mpaka sasa unaweza anza kupata picha ya kuelewa tofauti baina ya mwanaume na mwanamke kiasili.

Lakini lazima tujiulize, wakati Mungu akiumba mradi wake mara zote alikuwa akikiri kuwa kila alichokifanya ni chema na hakika ilikuwa chema, lakini baada ya kumhamisha Adamu na kumpeleka Bustani ya Edeni ni kwa nini mawazo yake yalibadilika na kusema "Si vyema" "huyu mtu awe pekeake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na hapo ndipo akamuumba Hawa/Eva kupitia ubavu wake. Hii ni kumaanisha Kwa duniani Adamu ilikuwa vyema kuwa pekeake wakati Edeni haikuwa Vyema.

Lakini hapa panaweza kuleta hitilafu kwenye kufikiri, je ni Mungu huyo huyo aliyesema kila kitu ni chema na sasa amebalisha mawazo? Mbona Mungu sio kigeugeu?

Akili yangu inaenda nisikokujua inafikiri hivi, huenda Aliyemuumba Adamu siye aliyemuumba Hawa. Kwa nini ninafikiri hivi? Pengine niseme sijui. Embu tuone.

Nafikiri Hawa aliumbwa kwa njama, hila, za Kumuangusha Adamu. Kumbuka Adamu kwake ni duniani, wala sio Edeni. Edeni ilikuwa inamwenyewe, je ni nani huyo?

Embu ona, Adamu analetwa tuu Edeni hapo hapo anapewa sheria ya kutokula Tunda la Mti wa Kati wa ujuzi wa mema na mabaya. Fikiria hapo! Punde anaumbwa Hawa/Eva kisha aliyeumbwa muda huo huo anakuwa wakwanza kula tunda. Bado hujashtuka. Akili yako inakuambia nini kuhusu aliyemwambia Adamu asile matunda ya mti wa kati wa ujuzi wa Mema na Mabaya kwani atakufa? Kisha aliyeumbwa Edeni anakula hilo tunda na anaenda kwa adamu akiwa hajafa, huoni adamu angeona aliyesema ukila utakufa angekuwa muongo? Kumbuka Mlengwa wa lile tunda kula hakuwa Hawa/Eva bali alikuwa adamu. Kama Adamu asingekula lile tunda ni wazi Eva asingepata madhara. Lakini hila za aliyemuumba Eva, na ndiye huyo huyo aliyemwambia ale ili ampe adamu amuaminishe kuwa hatakufa ili ale ndio zilimuingiza Adamu Mkenge, kula tunda la sumu, lenye kuua taratibu kizazi cha Adamu mpaka hivi leo. Bado hujaona kifo ni mradi wa viumbe fulani?

Baadaye tunapata habari za Nyoka akimdanganya Hawa/Eva ili akampe lile tunda Adamu. Lile Tunda lisingekuwa na madhara yoyote kwa Eva/Hawa kama Adamu asingelila. Mtihani ule ulikuwa unamhusu Eva/ Hawa. Hata hivyo Hawa/Eva hakudanganywa bali alifanya makusudi kwani tayari alikuwa anapewa oda na aliyemuumba(huyo aliyemwambia ampe mumewe lile tunda)

Nyoka(ambaye sio huyu atambaaye) ndiye alikuwa mmiliki wa ile Edeni. Kama Adamu alivyoambiwa atawale dunia.

Ili ujue Hawa/Eva alifanya kusudi kumuangamizA Adamu, angalia alivyoenda kumpa lile tunda Adamu ili alile, wala hakumpa maelezo yoyote kuhusu huko alikotoka zaidi ya kumwambia nimelila na lafaa kwa kula. Hakumwambia amekutana na nani. Habari hizo Adamu anakuja kuzifahamu baada ya Mungu kuja ambapo Eva/Hawa anasema kuwa amedanganywa na Nyoka, (Namuona Adamu akijiona mjinga akitumbua macho yake kama mtu asiyeamini kuwa kaangushwa bila kujua) Mungu akamwambia umeisikiliza sauti ya mke wako. Kumaanisha hakupaswa kumsikiliza bali yeye ndio asikilizwe.

Baadaye Adamu na Hawa wanatimuliwa Edeni, na kurudishwa Duniani tayari akiwa amekula tunda lenye sumu iuayo pole pole. Na Mmiliki wa Edeni anabaki kuwa mshindi.

Kilichokusudiwa kifanyike Edeni kimekamilika, Adamu hahitajiki tena Edeni hivyo kufukuzwa ndio suluhu.
Alifukuzwa, na hapo ndipo rasmi mwanadamu akaanza kukengeushwa na viumbe wa Mbinguni kwa kutumia mawakala zao waliopo huku duniani. Mara Mbinguni, mara peponi mara sijui Akhera.

Ati tutaishi na Mungu. Sirius!!! Kabla ya kuanguka hatukuishi na Mungu, hata sasa hatuishi na Mungu, na kamwe hatuishi na Mungu. Hata hao viumbe wengine hawajawahi kuishi na Mungu. Bali ni propaganda zao za kurubuni kizazi cha mwanadamu kzidi kuwa watumwa.

Nataka kusema Nini?

Dunia haijawahi kuwa mbaya, ubaya unatokea nje. Bila Edeni pasingekuwa na mabaya yote yanayoendelea duniani. Edeni ndio kulikuwa na tatizo wala sio dunani.

Mbinguni wanaishi malaika, Mungu haishi Mbinguni wala haishi duniani.Mungu hana Anuani, popote yupo kwa wakati wote. Mungu hana Kiti cha Enzi. Mungu hana Ulinzi. Malaika ni viumbe walioumbwa kwa Mwanga mkali, wenye mfano wa mwanadamu lakini hawana miili kama yetu. Malaika wapo wa aina nyingi kulingana na kazi, maumbile, na Sifa. Wapo malaika wenye mbawa kuanzia mbili, tatu, nne, sita, kumi na mbili na kuendelea.

Huko Mbinguni ndipo matatizo yalipoanzia, Falme za Malaika zimegawanyika. Kuihubiri mbinguni ni kuidhalilisha dunia. Kuwatukuza Malaika ni kuwatukana wanadamu.

Ipo tabia baadhi ya wanadamu wanawaabudu viumbe waishio mbinguni kwani viumbe hao wamewaahidi mambo mazuri, wengine wakiahidiwa kupewa uzima wa milele, wengine kwenda mbinguni, wengine wanaabudu kwa majina wakina Mikael, sijui Gabriel, na Yesu ambao kimsingi hao sio Mungu.

Bali wao wamekuja kuwafanya wanadamu kama mateka, kama vile huku duniani nchi moja inavyoenda kutawala nchi zingine, tunaita Ukoloni na sasa Ukoloni mamboleo. Ndivyo na viumbe wa Mbinguni walivyofanikiwa kuwatalawa viumbe wa duniani yaani sisi wanadamu.

Wanadamu wanawaona malaika ni bora kuliko binadamu. Wanapaona Mbinguni ni bora kuliko duniani.

Ninachotaka kusema ni kuwa, mwanadamu alikuwa mkamilifu kabisa kabla hajakutana na hila za viumbe wa mbinguni, si ajabu hata Edeni ilikuwa hila za hao viumbe kwani wamejaliwa nguvu, uweza, akili na mamlaka ya kusema kitu kikawa.

Matatizo ya duniani hayataisha leo lakini atakayeyamaliza ni mwanadamu mwenyewe. Pale Mwanadamu atakapoacha kuwatumikia Viumbe wa mbinguni iwe ni malaika au mashetani ndio siku hiyo hiyo dunia hii itakombolewa.

Naamini, miaka ya hivi karibuni mwanadamu ataweza kukikabili kifo. Watu hawatakufa tena kutokana na matokeo ya kisayansi na tekonolojia. Kifo kitadhibitiwa.

Nafahamu kuwa Kifo ilikuwa ni Mradi wa viumbe wa Mbinguni kumtawala mwanadamu. Lakini baada ya kifo kukidhibiti mamlaka ya mwanadamu itarejea kama ilivyomwanzo.

Kifo hakitadhibitiwa kwa kutamani kwenda Mbinguni. Watu wanachoshindwa kuelewa ni kuwa Kifo kimeletwa na viumbe hao hao wa mbinguni.

Sijajua Mungu yupo wapi kwa sasa, licha kuwa mahali popote yupo. Lakini hawezi ingilia mambo haya, mpaka siku ya hukumu.

Siku ya hukumu itafika pale ambapo Mwanadamu ataweza kukidhibiti Kifo.

Mbinguni sio salama kama watu wanavyofikiri.

Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Unguja
 
900 itapendeza

Senior Member
Nov 17, 2017
113
225

Duuuuuuuuh ngumu kumeza
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,225
2,000
huwa najiuliza hivi..
1.ilichukua muda gani tokea Adam aumbwe ndio akaumbwa Hawa ?
2.Ndani ya muda huo Adam alikuwa akifanya mapenzi na nani? Alikuwa hana sha hawa, had* ndi ama vipi?
3. kama viumbe wengine walianza kuumbwa *jike na dúme* iweje Mungu Amuumbe Adam peke yake bila jike?
Naendelea Kufikiri
Nalog off
Umewaza kitulivu, lakini kuna maswali rahisi umeyafanya kuwa magumu kwa makusudi.

Mfano q#2! 'Ndani ya muda huo Adamu.....etc etc!

Jibu lake mbona ni rahisi tu, kwamba alikuwa hajabaleke, kwani binadamu kabla ya balekhe huwa ana uwezo wa kuyafanya hayo uliyouliza?

Maelezo yako ya hoja kuhusu uumbaji wa Mungu kuumba mwanadamu dume bila jike, wakati alikuwa na 'exposure' ya uumbaji huko nyuma kuumba viumbe kwa mfumo wa pair ya dume na jike ili vizaliane, ninayaunga mkono.

Katika maelezo ya vitabu vitakatifu kuna mkanganyiko, ni kama vile M/Mungu viumbe alioanza kuwaumba walikuwa ni binadamu, kumbe binadamu ndiye kiumbe wa mwisho kuumbwa na kuwekwa hapa duniani.

Binadamu kaletwa duniani kakuta viumbe wanaishi na wengine hakuwakuta, tayari walikuwa wametoweka (mf: dinosours), lakini viumbe wote hao walikuwa madume na majike.

Iweje kwa binadamu kuwe na mkwamo na kusua sua kwa uumbaji kiasi hicho?

Huwa inafika mahali maandishi yanajichanganya menyewe halafu waumini tunafokewa na kutishwa ili tusitafakari kiuyakinifu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
20,673
2,000
Wakati Mungu anaumba Mradi wake wa Dunia aliumba kila kitu kikiwa chema kabisa. Hakuna ambacho kilikuwa na kasoro, kila kitu kilikuwa kimekamilika. Hivyo yeyote unayemuona hapa duniani ujue amekamilika yaani yuko full completely. Hii Propaganda ya kusema mwanadamu hajakamilika ni hila, njama, ulaghai wa viumbe wasio na asili ya binadamu.
Kwanini umeamua kuandika uongo, uongo ambao hata ukitafakari tu kwa akiki yako ndogo unauona ?

Kama wewe ni mkamilifu, inakuwaje una sahau ? Au kusahau ni ukamilifu ?

Kama umekamilika kwanini huwezi kusikia mazungumzo baina ya sisimizi ? Au kwanini huwezi kumuona sisimizi umbali wa mita tano kutoka wewe ulipo ?

Kabla sijaenda mbali, nieleze kwa kifupi namna Mradi huu wa Dunia ilivyoumbwa na Mungu. Mungu aliiumba dunia kwa mfumo wa kutegemeana (Ecosytem) yaani viumbe vinategemeana. Kutegemeana huku ndio kunakamilisha mradi mzima wa dunia. Katika Mradi huu kuna aina nyingi za viumbe kulingana na asili yao walivyoumbwa. Mathaalani; Wapo viumbe walioumbwa kwa Hewa, wapo walioumbwa kwa maji, wapo walioumbwa kwa moto, wapo walioumbwa kwa Mwanga/ nuru wapo walioumbwa kwa udongo, wapo walioumbwa kwa mchanganyiko wa mada zaidi ya moja yaani labada maji na udongo, au hewa na mwanga.
Sasa hapa mbona unathibitisha kutokuamilika na muda huo huo unadai sisi tulimbwa tukiwa kamili ?
 
Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
20,673
2,000
Adamu aliumbwa Duniani ambapo kiasili ndio kwake. Baadaye Mungu Akamchukua huyo Mtu akampeleka (Edeni) ambapo kiasili sio Duniani. Kumbuka Adamu akitolewa Duniani kupelekwa Edeni alikuwa pekeake kwa mujibu wa maandiko.
Haya umeyapata wapi ? Naomba ushahidi wa haya na utupe na jina la kitabu na jina la muandishi wa haya uliyo yaandika.
Lakini hapa panaweza kuleta hitilafu kwenye kufikiri, je ni Mungu huyo huyo aliyesema kila kitu ni chema na sasa amebalisha mawazo? Mbona Mungu sio kigeugeu?
Haya uliyo uaandika Mungu ameyasema wapi ?
 
Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
13,017
2,000
Umewaza kitulivu, lakini kuna maswali rahisi umeyafanya kuwa magumu kwa makusudi.

Mfano q#2! 'Ndani ya muda huo Adamu.....etc etc!

Jibu lake mbona ni rahisi tu, kwamba alikuwa hajabaleke, kwani binadamu kabla ya balekhe huwa ana uwezo wa kuyafanya hayo uliyouliza?

Maelezo yako ya hoja kuhusu uumbaji wa Mungu kuumba mwanadamu dume bila jike, wakati alikuwa na 'exposure' ya uumbaji huko nyuma kuumba viumbe kwa mfumo wa pair ya dume na jike ili vizaliane, ninayaunga mkono.

Katika maelezo ya vitabu vitakatifu kuna mkanganyiko, ni kama vile M/Mungu viumbe alioanza kuwaumba walikuwa ni binadamu, kumbe binadamu ndiye kiumbe wa mwisho kuumbwa na kuwekwa hapa duniani.

Binadamu kaletwa duniani kakuta viumbe wanaishi na wengine hakuwakuta, tayari walikuwa wametoweka (mf: dinosours), lakini viumbe wote hao walikuwa madume na majike.

Iweje kwa binadamu kuwe na mkwamo na kusua sua kwa uumbaji kiasi hicho?

Huwa inafika mahali maandishi yanajichanganya menyewe halafu waumini tunafokewa na kutishwa ili tusitafakari kiuyakinifu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru kwa hili jibu pamoja na maelezo mengine kuhusu huu mkanganyiko
Nalog off
 
Ramadhan James

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
2,188
2,000
Kwanini umeamua kuandika uongo, uongo ambao hata ukitafakari tu kwa akiki yako ndogo unauona ?
Kama wewe ni mkamilifu, inakuwaje una sahau ? Au kusahau ni ukamilifu ?

Kama umekamilika kwanini huwezi kusikia mazungumzo baina ya sisimizi ? Au kwanini huwezi kumuona sisimizi umbali wa mita tano kutoka wewe ulipo ?

Sasa hapa mbona unathibitisha kutokuamilika na muda huo huo unadai sisi tulimbwa tukiwa kamili ?

Penda kushambulia mada sio kumshambulia mleta Mada pia kumbuka Utafiti hupingwakwa Utafiti sio kupopoma ni " uongo" leta huo ukweli unaoamini ili nasi wengine tufahamu kisha tuamue jambo sahihi sio kutaka kutukaririsha tu " ni uongo"

Kusahau ni Nature kama ambavyo unalala bila hata kuomba ulale!

Ulienda Shule ili hukusoma na ukaelimika, Daima huwezi kumsikia Mdudu wala Mnyama maana hutambui wala huelewi lugha za Wadudu au Wanyama ndio maana unaishi na Mbwa, paka, mende, kunguni, Kondoo, Farasi, mijusi na Nguruwe lakini huwezi kuelewa wanachozungumza. Ebu kaa kujiepushe na aibu ndogondogo!

Nadhani hata wewe ukirudia kusoma hiyo Sentensi hautaelewa ulichoandika, amesema " tumeumbwa tumekamilika" elewa na usiulize tashititi.
 
Kwanza nakuomba unithibitishie tu kitu kimoja, umejuaje kama hiki alichokiandika ni Utafiti ? Isiwe unapenda kuandika ujinga.

Pili, nimeshambulia vyote viwili na ndiyo maana nimeweka na mifano. Sasa kama nimeandika ujinga jibuni maswali niliyo uliza hapo juu. Acha kukurupuka na kuandika ujinga.

Tatu, ulivyokuwa zwa zwa unauita huo ni utafiti.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom