Mbinguni nako hakutakuwa salama

mtarimbo

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,529
3,919
Kuna dhana ya kwamba mbinguni ukifika basi full kiyoyozi,yaan bata lake usipime, kuimba na kucheza tuu na raha nyingi, wengine wakaenda mbali zaidi ukifika huko unapewa mademu wa kutosha, yaani tendo la sex litaboreshwa kileleni unachukua siku tatu ndio una.., mtanisamehe nimeenda direct bila misamiati

Ila ukisoma Ufunuo kuhusu mbingu mpya ndipo akili inaruka na kujua huwenda kule nako kuna changamoto au hamjui jibaba alitokea huko

Ni hivi yaani hiyo Jerusalem itakua na bonge la ukuta jiulize panapojengwa ukuta mkubwa maanake siyo salama, najua watakuja wazee wa kutafsiri mtadai huo ukuta ni wa kiroho unamaanisha kuzungushiwa baraka.

Pili kuna ulinzi wa kufa mtu kila geti lina ulinzi.

Tatu kuna miti shamba ya kuponya magonjwa mbalimbali.

Mwisho taa hazitazimwa milele ni full mwanga.

Huenda tunashindwa labda kuelewa maandiko maana kwa uelewa wangu mdogo mbiguni ni stages za kufanyika kuwa mwana wa Mungu.

Kila stage ina fahari yake na changamoto zake.

Huenda kuna matatizo makubwa ambayo hatujawahi kusikia wala kuyaona tutayaona huko n.b kwa wateule tu.

Mungu hakupata kuwa Mungu kirahisirahisi, anafanya kazi na anakabiliana na machangamoto ya kutisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom