Mbingu saba, siri na nguvu ya namba saba

Ikiwa katika mfuatano wa namba msingi yani 0-9/1-9, namba saba inaonekana ni namba ya kawaida kabisa, lakini kwa taarifa yako hii ndio namba ya ukamilifu inayoendesha dunia na ndio namba yenye tafsiri zinazoshabihiana kwenye imani zote
Nina hakika ulianza kuitambua hii namba upekee wake kwenye habari za uumbaji, kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa siku sita na siku ya SABA akapumzika..... Lakini wengine watakuambia kuhusu mnyama paka Kuwa na roho saba ama lile joka lenye vichwa saba

View attachment 503310Kibiblia namba saba! Imetajwa kwenye mambo mengi sana sana nitataja machache kwasasa
-ukamilifu wa kiroho
-utimilifu wa jambo
-mnyama wa sadaka asiwe chini ya siku saba
-pair saba za wanyama walioingia kwenye safina ya Nuhu
-Alama ya uungu na Mungu mwenyewe huku namba sita ikiitwa namba ya mwanadamu (refer uumbaji na Freemasons)
-msamaha samehe saba mara 70
Namba saba imetajwa kwenye Bible mara 490 ...hapa utapata majibu mengi

View attachment 503309Kwa Wahindu na wabuddhist wanaamini katika mbingu saba kama ifuatavyo
1.dunia
2.ulimwengu hai
3.mbingu
4.ulimwengu wa kati, mpaka kati ya ulimwengu wa juu na chini, ulimwengu wa kiza na nuru
5.ulimwengu wa rebirth na reincarnation
6.hekalu la baraka mduara wa ukweli
7.mbingu ya saba, hatua ya mwisho kufikia ukamilifu

Nitakuja na tafsiri ya namba saba kwa imani ya Kiislam pia....lakini namba saba ni namba yenye nguvu mamlaka na ndio pointer ya ulimwengu unaoonekana toka katika ulimwengu wa roho

Nitarudi kuendelea sehemu ya pili.... Usisahau pia kinywaji baridi cha SABA JUUView attachment 503308
9 is the best
 
Tuliozaliwa mwezi wa saba tucomment wapi mshana ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
.
slide_3.jpeg
 
Ikiwa katika mfuatano wa namba msingi yani 0-9/1-9, namba saba inaonekana ni namba ya kawaida kabisa, lakini kwa taarifa yako hii ndio namba ya ukamilifu inayoendesha dunia na ndio namba yenye tafsiri zinazoshabihiana kwenye imani zote
Kwa sisi wakristo hakuna mahali kwenye vitabu vyetu vya dini Yaani Biblia kuna sehemu pameandikwa kuna Mbingu saba,halafu Mungu hakuumba ulimwengu na vitu vyoote kwa siku 6 halafu ya saba akapumzika,nikwamba kazi yake ya uumbaji ilianza siku ya kwanza hadi ya saba halafu ndio akapumzika yaani Mungu alimaliza kazi ya uumbaji hadi ile siku ya saba halafu siku hiyo hiyo ya saba alipomalizia uumbaji akapumzika inamaana hadi siku ya saba Mungu alifanya kazi ya kumalizia uumbaji wake halafu akapumzika MWANZO 2:2
Kwa imani ya Kikristo namba saba na namba zingine zoote hazina maana yoyote sijui kwa imani za wenzetu uliowataja
 
Kwa imani ya Kikristo namba saba na namba zingine zoote hazina maana yoyote sijui kwa imani za wenzetu uliowataja.... Okay
 
Namba 7 kiimani ni namba ya Ukamilisho.

Jamarat mawe 7
Surat fatiha ina aya 7
Shahada herufu 7
Watoto wa mtume walizaliwa 7
Mtoto aanze kujifunza dini akiwa na miaka 7
Takbar ya Idd huwa ni 7
Malaika wakuu wapo 4(Jibril, Mikael, Israafil na Malakul Maut)

Mitume waliyopewa vitabu 4( Daud, Musa, Issa na Muhammad)

Vitabu navyo 4 ( Zabur, Taurat, Injil na Furqan)

Maswahaba wa Mtume wakubwa wapo 4 ( Abuu Bakr, Umar, Uthman na Ally)

Maimam wakubwa wapo 4 ( Imam Malik, Imam Shafii, Imam Muhammad ibn Hambal na Imam Abuu Hanifa)

Malaika waliyobeba Arshi ya Mungu ni 4 ( Siku ya Qiyama wataongezwa watakuwa 8)
_---------------------------------------------------

Swala zipo 5

Nguzo za Uislam ni 5

Uulil Azmi ni 5( Nabii Ibrahim, Nabii Musa,
Nabii Issa, Mtume Muhammad mwengine nimemsahau)

Maswali atakayoulizwa mja siku ya Qiyama ni ma5
 
Nimeongeza maarifa mapya hapa.... Elimu haina mwisho na ubongo haukatai kupokea maarifa mapya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom