Mbilinyi: CCM na Serikali yake ni vurugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbilinyi: CCM na Serikali yake ni vurugu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Feb 16, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mbilinyi: CCM na Serikali yake ni vurugu

  • Asema zipo CCM mbili, serikalini uwenzetu upo
  • Afikiria Unguja ingekuwa mkoa na Pemba wilaya
  • Aonya kujiunga OIC ni mawazo finyu na uvivu

  Na Sarah Mossi

  WAZIRI wa zamani wa fedha anayeendelea kushika nyadhifa mbalimbali kitaifa kwa sasa, Profesa Simon Mbilinyi, amesema kuna tatizo serikalini na katika chama tawala.

  Akizungumza na Rai katika mahojiano maalumu wiki iliyopita nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam, Profesa Mbilinyi alisema inavyoelekea kuna CCM (Chama Cha Mapinduzi) mbili; ile ya zamani na ya sasa ya wanamtandao ambayo itaharibu nchi.

  “Wamejitahidi (Serikali ya Rais Jakaya Kikwete) kufanya waliyoahidi katika kampeni, ila bado kuna problem ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali, hawako pamoja na personality zimeanza kutawala. Siasa hizi zitatupeleka pabaya.

  “
  Serikali ifikirie hili kwa kina zaidi na iwe na watu strong (wenye nguvu), isiwe na ideas (mawazo) za zamani za huyu ni mwenzetu, tuseme huyu anaweza. Tukisema huyu ni mwenzetu tutaumia. Hata muundo wa Serikali ni mkubwa kuliko kazi zilizopo, tuna watu wengi wa kufanya kazi lakini kazi hazipo. Central Government (Serikali Kuu) zina matrilioni ya bajeti lakini hazina kazi, kazi zote ziko kwenye district (wilaya).

  “Kwenye siasa…kwa uzoefu wangu CCM ina two shadows (vivuli viwili). Kuna chama in tradition (jadi) na chama mtandao. Hizi mbili ziwe pamoja kama ilivyokuwa zamani na chama kifanyiwe ukarabati kifanye kazi kama kilivyokuwa zamani. Sisi wazee tunaona chama hakipo sawa,” alisema Profesa Mbilinyi kwa masikitiko.

  Alisema changamoto kubwa iliyonayo Serikali sasa ni suala la ukosefu wa ajira, akaonya kwamba yalikuwa makosa makubwa kubinafsisha na kuuza mashirika mengi ya umma, badala ya kukodisha.

  “Changamoto kubwa ambayo ni ya hatari ni unemployment (ukosefu wa ajira), vijana wengi utawaona ni smart (werevu) lakini hawana ajira. Ajira yenyewe iambatane na structure (mfumo) ya uchumi. Tumefanya makosa makubwa ya kubinafsisha kila sekta lakini bado hazikufanya vizuri. Badala ya kutaifisha tungeajiri wakubwa wenye nafasi waje watuendeshee viwanda vyetu. Tungealika watu waje watusaidie kujiendesha. “Kwenye mambo ya simu na posta leo hii tungekuwa na Tigo yetu, Zantel na Vodacom za kwetu. Hawa sasa wana fedha nyingi wanaweka matangazo yao katika kila sekta, hata kwenye michezo wanajitangaza. Tunachotakiwa hivi sasa kuwa na approach (mwelekeo) mpya si ile ya miaka ya 1970. Kilimo kiambatane na viwanda vyake. Tumeuza NBC (Benki ya Taifa ya Biashara) sasa tunaumia, na tuliharibu whole industry (viwanda vyote) tukaviuza badala ya kuleta watu kutusaidia kujiendesha. Tunahitaji viwanda ku absorb young population (kukidhi vijana),” alisema. Kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mivutano ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Mbilinyi alisema Zanzibar wangeachwa wenyewe bila kuunganishwa na Tanganyika, wangeuana. Kwamba angekuwa yeye enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekifanya Kisiwa cha Pemba kuwa ni moja ya wilaya katika Mkoa wa Tanga na Unguja kuufanya kuwa mkoa mmojawapo wa Tanzania.

  Alisema kwamba kuifanya Zanzibar kuwa mkoa ni suluhu ya kuwaepusha wasiuane kama ilivyokuwa katika miaka ya 1950, wananchi walipouana kwa sababu za kisiasa.

  Alionya kuwa migogoro ya kisiasa iliyopo Zanzibar inatokana na kauli potofu za wanasiasa wa visiwa hivyo, ikiwamo kauli inayodaiwa kuwa Zanzibar inanyonywa na Tanzania Bara. Ameshauri kuwapo mjadala mkubwa wa kisiasa Visiwani wa kumaliza mitafaruku, ikiwa ni pamoja na kuwaachia Wazanzibari waamue wanataka nini.

  "Tumejitolea (Tanganyika) sana bila kupata kinachotakiwa, lakini sasa wanasema (Wazanzibari) tunawanyonya," alisema Profesa Mbilinyi.

  Kuhusu baadhi ya watu na taasisi kutaka Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC), Profesa Mbilinyi alionya kuwa hayo ni mawazo finyu.

  Alisema madai kuwa nchi itafaidika kiuchumi ni kubweteka na ni uvivu, hivyo wananchi wanatakiwa wajengewe mazingira ya kufanya kazi na kuzalisha si kukimbilia kwenye mashirika kuombaomba.

  "Chama kinaweza kusaidia katika hili hasa wale wa zamani, lakini hawa wapya si rahisi na kwa sisi wengine hatuna dini, dini zote ni zetu. Ndio, wote wanaoingia huko ni kwa sababu za kiuchumi lakini sisi tufanye kazi, sisi hatuna dini," alishauri Profesa Mbilinyi na kuonya kwamba kuiingiza kwa nguvu Tanzania katika umoja huo hakutasaidia na si vyema kuifanya dini moja kuwa juu ya dini nyingine.

  Mjadala wa Tanzania kujiunga na OIC umeibuka tena baada ya miaka mingi kupita pale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kutaka kujiunga na jumuiya hiyo katika miaka ya 1980 na kupingwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikidaiwa kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  Hoja ya Zanzibar kujiunga na OIC ilikuwa ikitaka kupata ahueni ya kiuchumi kwa maana ya kupata misaada ya kifedha inayotolewa kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Wakati huo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, hayati Ahmed Hassan Diria alidaiwa kufanya mipango ya kuiingiza Zanzibar kwa siri katika jumuiya hiyo na kuzua mtafaruku.

  Hoja kubwa iliyopigiwa kelele na wananchi ni msimamo wa nchi kwamba Serikali ya Tanzania haina dini isipokuwa watu wake ndio waumini wa dini wanazozipenda. Lakini kikubwa zaidi kilichoafikiwa baadaye ni kwamba iwapo nchi ingetaka kujiunga na jumuiya hiyo, basi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo ina jukumu la kuomba uanachama huo wala si Zanzibar, maana Zanzibar si dola.

  Hoja hiyo imeibuka tena hivi karibuni, wakati huu ikianzia kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania karibuni, ambapo viongozi mbalimbali, akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri, Seif Idd kusema walikuwa kwenye mchakato wa kujiunga.

  Hata hivyo, wabunge waligawanyika, huku waumini wa dini ya Kikristo wakijitokeza waziwazi na kupinga uamuzi huo wa Serikali. Zanzibar nayo imesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiunga na jumuiya hiyo bado upo pale pale iwapo Tanzania itasuasua.  © New Habari

  Kama Rangi zitawaumiza tuelezane ili nizitoe au Invisible afanye hivyo.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Du ila hili la Pemba kuwa Wilaya ya Mkoa wa Tanga limeniacha hou!!!!!

  Yaani kama Mafia ilivyo Wilaya Mkoa wa Pwani?
   
 3. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mzee Mbilinyi!! (tena Profesa) alikuwa wapi wakati wote huo wa kupangwa mpaka kufikia kuuzwa kwa MASHIRIKA na MALI ASILI atupe mawazo na lawama hizi leo????? Kama ni tatizo la SEREKALI au la CCM yeye alikuwa na bado ni PART and PARCEL wa vyombo vyote viwili hivyo sasa mzee wetu anachotueleza ni nini mimi nashindwa kumelewa kabisa. Kuhusu CCM na mgawanyiko wao ofcos ni kujitafutia maslahi binafsi kila Mwamba ngoma huvutia kwake hilo halitupi wasiwasi Wananchi tumeshang'amua janja yao. Swala la ZANZIBAR hakuna haja ya kuendelea na uzito na kulaumiana kila kukicha LETS SPLIT THE SOONER THE BETTER. Juu ya OIC sioni hasaa umuhimu wa kujiunga kwa sababu za kiuchumi au za kidini.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli, pamoja na shutuma yoyte tuliyo nayo, mi namsifu Prof Mbilinyi, ameamua aseme things the way they are, siyo kuoneana haya. Sasa hivi utasikia ameandamwa oh, hivi vile, lakini mi nasema afadhali ameamua kuongea kuliko kuwa observer on the side! Wacha wazidi kujitokeza wengine wengi within CCM wajikosoe! That is a good sign!
  Hiyo ya Zenji, I like it! Yaani kaamua atupe changamoto ni kama throwing a bomb in the midst of a strife, but atleast he gets what he wants - ATTENTION! Kwkwikwiii.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo ni mfu mwingine ambae anatumia wakati wake wa majeruhi au extra time ya uhai wake kujiungisha ,yaani ukisoma kwa kina utaona anamshambulia Kikwete waziwazi maana ya mtandao ni ya Kikwete na ndio CCM iliyoshika bendera kusema itaharibu Nchi hakukosea maana dalili zinaonekana zimeanza kuwa za vitisho ila kama kuanza kuharibika kulianzia tokea wao wapo madarakani palipobaki ni kuendelea kuoza tu hakuna jipya ,ndio tunaposema samaki mmoja akioza wameoza wote ,hivyo iwe iwavyo CCM yote haifai kuwepo madarakani kuwepo kwao madarakani ni kuioharibu nchi na hakuna lingine watakaloweza kulifanya zaidi ya hilo.Suala la OIC si suala la kuumiza watu vichwa

  WaZenji wameshaona upande wa Bara wamekuwa wazito kama itakuwepo ajabu na mawazo finyu aliyoyaona huyu mzee wa kufa ndio waliyonayo wabara hakuna jingine ni nchi kibao tu zimo kwenye umoja huo tatizo lipo kwa Tanzania tu ,ni ufinyu wa mawazo na zaidi kulazia kwenye dini na kujifanya wengine ni watu au waumini wa kweli wa dini lakini ni waongo wakubwa wezi kama wao hakuna.maana fedha inayoletwa na kanisa kama itaanza kufuatiliwa utaona watu wanavyoadhirika kushinda mafisadi ndani ya CCM ,so far kuliunganisha suala la OIC ni kukosa muelekeo wa mawazo.


  Kuhusu Zanzibar (Unguja na Pemba) kuwa wilaya hilo kashindwa Baba yake Nyerere kulitekeleza na asidhani kuna atakaeweza ni kutafuta la kutafuta lakini hilo asitegee CCM yeyote yule kuwa ataweza kulitekeleza.Ni kutaka kuwadanganya watu na kuwaibia fedha hakuna jingine.

  Sasa huyu mzee kama alikuwa haelewi basi ajue kuwa unyonyaji upo na mnainyonya Zanzibar kwa hali na mali yaani hata kaburini ataenda kuambiwa suala hilo kuwa alikuwemo katika watu wanaoinyonya Zanzibar ,akikataa rungu, ndio maana yake,huko hakuna Sefu sharifu kama mtasuguana kwenye viriri vya majukwaa ya siasa, ni rungu tu.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh! Yote kazungumza vizuri sana lakini swala la Zanzibar kachemsha big time!...Lugha yote aliyotumia ni lugha ya chama na sio elimu yake, ktk swala la kitaifa ambalo halina suluhu toka CCM chama kimoja...
  Inaonyesha wazi kabisa kuwa Ujamaa na Ubepari ni vitu ambavyo vimewashinda hata wasomi wetu kutofautisha SIASA na UCHUMI pamoja na kwamba vinaenda pamoja kama vile Waislaam wanavyoshindwa kutofautisha DINI na MAISHA..
  Transition yetu itachukua muda zaidi ya vile nilivyofikiria!
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wacha hizo za kuchomekea na ni vipi utaweza kutofautisha dini na Maisha ? maana kama wewe unaleta udiniudini hapa basi ujue patakuwa hapana au hapatoshi kuandika, hivi wewe unaweza kuleta maana ya Ukiristo hapa ? Na nadhani huelewi hata maana ya neno Dini ndio ukakurupuka tu.

  Au wewe na huyo Mbirimbi nyote ni wamoja hamna dini anaesema serikali ya Tanzania haina dini ni muongo tena mwizi mkubwa ,iweje hakuna dini mtake watu watumie kukamata vitabu vya dini wanapokula kiapo ?

  Tanzania haina dini ,sasa basi iwe hakuna kula kiapo mtu atumie Katiba tu na avuruge kivyakevyake ndio maana mafisadi wakaiba.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Mkuu acha jazba.. soma (Ikrah) kisha jaribu kuelewa..
  Nilichoandika pamoja na kwamba hukupenda ndio ukweli wenyewe kuwa DINI ndio MAISHA.. Na hakuna UCHUMI bila SIASA pamoja na kwamba hivi ni vitu viwili tofauti..
  Muislaam sio Muislaam kama huishi (Maisha) kulingana na MWONGOZO wa dini yako..wakristu vile vile isipokuwa tatizo linakuja unavyoweza kutafsiri mwongozo huo kwa ajili ya watu wengine wasiokuwa na imani hiyo.
  Hivyo, mwongozo ambao naweza kusema ni siasa ktk uchumi au dini ktk maisha ni issue inayo deal na muumini sio kila mtu..
  In this case Ujamaa kama siasa, muumini wake ataendesha uchumi wake kutokana na imani hiyo ya Kijamaa hivyo haitakiwi kumgharimu mtu mwingine... Muislaam muumini ataishi yeyey kwa kufuata dini yake na sio kumgharimu mtu mwingine ktk imani yake..
  Mawazo ya Porf. mbilinyi yameshindwa kutofautisha vitu hivyo..ni sawa na mkristu au Muislaam anayejaribu kuwahukumu waumini wa dini nyingine kwa jinsi anavyofikiria yeye..In this case Mbilinyi katumia UCCM ktk kufikiria hatma ya taifa zima on Zanzibar..
  Sijui kama umenielewa!
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa umeeleweka japo umevuruga maana unapoelezea maisha ya kidini naamini katika dini imeelezwa vipi unaishi na watu wa dini zingine,ila pale mwanzo mjomba ulirusha dongo.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Sikurusha dongo mkuu isipokuwa wewe ndiye hukufahamu.. kwanza ungeelewa alichosema Mbilinyi kisha ukaunganisha na mfano wangu.. hatuzungumzii dini na waumini wake isipokuwa UCCM na muumini wake kutoa hukumu ya Muungano hasa alkilenga upande mmoja usiokuwa wake..
  Hii haina maana maneno ya Mbilinyi yanatokana ktk msahafu wa CCM au elimu yake bali katumia unazi wa chama ktk swala la taifa..
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tanzania bara kwanza nchi kubwa lazima igawanywe ziwe nchi mbilia au tatu hili kuleta maendeleo.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Naungana na mawazo ya Prof. Mbilinyi kwa kiasi fulani hasa pale anaposema kuwa ccm inatupeleka kubaya!! Ni dhahili kuwa ccm sasa imefika mahali ambapo ili iwe relevant to the current situation in Tanzania ni lazima ichague aidha IBADILIKE katika VISION yake kama bado inayo!! au ibakie hivyo ilivyo na kufa kifo cha pole pole kama vilivyokufa UNIP huko Zambia na KANU kule Kenya. CCm hawawezi kuleta maisha bora kwa kila mtanzania kama wataendeleza kubagua wananachi kuwa huyu mwana mtandao na huyu sio; watu watapata maendeleo pale kazi zitapewa watu kwa uwezo wao na sio upendeleo!! Maendeleo yatakuja pale tu watu watafanya kazi na si kutegemea kutembeza bakuli iwe kwa watu binafsi hata nchi yenyewe!!. Maendeleo yatakuja pale tu viongozi watakapopiga vita rushwa kwa dhati na si kwa usanii; na ili watu wamuamini JK kuwa halifanyii mzaha swala la RUSHWA, Lowassa , Karamagi na Msabaha wafikishswe mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao juu ya mkataba wa Richmond. Muungwana akifanya hivyo atakuwaamepeleka salamu kwa mafisadi wote nchini kuwa hana masihara na mambo ya rushwa na wengine wote wataogopa vinginevyo wataona nimzaha tu.Kiomgozi imara humtoa rafikiye mpenzi kafara kuonesha seriousness ya maamuzi yake!!
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bulesi,
  Kila kitu ni mahesabu kwa CCM...
  Rostam, Lowassa , Karamagi na Msabaha ni bao la mwisho (kufikishwa mahakamani) kabla ya uchaguzi..
  Hapo JK na CCM watajizolea kura asilimia 90%...
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kura za wizi CCM imekwisha ,na haina pa kukimbilia ispokuwa kutumia nguvu za Jeshi kama walivyotumia kule Zanzibar ,ndio maana yake kwa CCM kubaki madarakani ni lazima wauwe tu hawana njia mbadala ,nani asiejua kwamba CCM walikwiba kura hapa Tanganyika na kule Zanzibar.

  WaZanzibari walikwisha aamka na kuzuia wizi huo ndipo majeshi yalipotumika kupindua matokeo ,upande wa bara walikuwa bado wamelala ila kwa siku zinavyozidi kukaribia na msisimko wa watu wanavyoamka basi hakuna la ziada linaloweza kufanywa na CCM ila kutumia nguvu maana pande zote mbili za Muungano zimeshaamka.
   
 15. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ....na kuombaomba mkuu!!
   
 16. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zakumi, mkuu hii ingefaa iwe Thread mpya kwani tunaafikiana kimaoni TANGANYIKA as a state/nchi is too big to rule from one centre.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa ukubwa gani lakini jamani?..
  Mbona Angola na nchi nyingine kibao zinaweza kwenda mbele kwa utawala kama wetu?... Lini sisi Watanzania tutakuja kubali kwamba matatizo ni sisi wenyewe Binadamu sio ardhi wala viwanda..If Angola na vita yote ile leo hii wametupita kama tumesimama iweje sisi tatizo liwe ukubwa wa nchi.

  A company goes down, tunatafuta sababu ndani ya shirika lenyewe kulibomoa sio viongozi wake..Leo tuna matatizo ya nchi tunatafuta kubomoa bomoa nchi tukitumia viongozi wale wale walioshindwa..can't get it!
  Ikiwa rais ameshindwa kuiendeleza nchi ndogo kama Zanzibar yenye raia wasiozidi millioni 2 tutaweza vipi kuongoza nchi yenye majimbo manne, matano na hata manane tofauti...
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ningeanzisha lakini sio unaona Mkandara alivyokuja juu. Kuna nchi Afrika, ni mateso tu kuendelea kujitawala. Nchi kama DRC, Tanzania, Sudani n.k ni kubwa mno. Na watu wenyewe hawana sophistication ya kujitawala. Huo ndio ukweli wa mambo.

  Matokeo yake tunapoteza muda na resources kutafuta amani na umoja. The size ya DRC ni sawa na nchi za Western Europe. Sudan vilevile. Matokeo yake vurugu tupu.

  Angalia nchi ndogo kama Rwanda. Wanaingia kwenye matatizo na wakimaliza wana-perform better kuliko sisi.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Mwiba, myonge, mnyongeni, haki yake mpeni. Ni kweli CCM iliiba kura Tz Visiwani na sio Bara. Visiwani angalau mna chaguo la wazi Ama CCM Ama CUF lakini bara ni utitiri, japo sio wote wanaipenda CCM lakini bado waliipa kura kwa sababu hakuna jinsi.
  Kwa upande wa Zanzibar, CCM haina jinsi ni lazima waibe kura ili Zanzibar isirudi kwa waliwapokonya tonge mdomoni baada ya uhuru wa Dec,'63. CUF ni lazima walie kwa vile ndio walionyang'anywa.
  Historia ya Zanzibar iatawaliwa na siasa za chuki, jazba na vitisho, ubabe na tishio la visasi. Ndo maana JK keshatangaza matokeo ya 2010 hata kabla ya uchaguzi, ni yaleyale ya Jan.'64, '95, '00 na '05 labda kama CUF nayo itamtafuta John Okelo wake.
  Suluhisho la kudumu ni utekezaji wa muafaka kwa serikali ya mseto.
  Huku bara pia mambo ni yale yale, CCM hawaibi kura bali wanajiokotea tuu kutokana na uhamasishaji duni na udhaifu wa upinzani utokanao na utengano ndio unaopelekea CCM kuendelea kutesa na mustakabali wa taifa letu lote kuendelea kuwa mikononi mwa CCM milele.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Mkuu wangu haya maswala ya kubishana bila kutumia fact na kuzichambua hayana mpango.. najua wewe msomi mzuri sana na umeelewa vizuri nilichoandika..
  Tatizo ni sisi binadamu na uongozi wake sio ukubwa wa nchi..U know it isipokuwa sasa labda unatumia siasa..
  Swala la Rwanda na maendeleo yake huwezi kuliweka ktk mjadala huu kwa sababu kuna nchi ndogo nyingi sana Afrika kama Burundi jirani yao tu hazifanyi vizuri kama wao wakati vita yao ilikuwa ndogo na ya muda mfupi sana. Ukitazama upande wa West Afrika kuna lundo la nchi ndogo ndogo mara tano ya Tanzania (i.e Guinea Bissau) lakini zote maskini kuliko zote duniani ukijumlisha na visiwa vya Haiti huko Carribean...Zote tumeona matatizo ya uongozi wa nchi hizo ktk utawala bora..
  Nakuomba itazame tena ramani ya Afrika kisha nambie kwa nini nchi hizo maskini..
  Ukizungumzia Ulaya, hapo tayario mwenyewe umeisha toa jibu ULAYA! maendeleo yao yametokana na Uongozi pamoja na watu wake, sio ukubwa wa nchi kwani zipo nchi maskini pia zenye majimbo wakati Canada ambayo ni kubwa kwa kila jimbo kuliko Tanzania na nchi hizo za Ulaya imeendelea zaidi..
  Unaposema Angola wamebarikiwa resources nyingi una maana gani mkuu wangu!..ikiwa swala ni baraka za resources iweje Kongo wamebakia nyuma! Hivi baraka zote tulizopewa sisi mnashindwa kuzitambua wakati tuna kila madini nchini, gas, maji masafi (Lakes) na ardhi yenye rutuba naweza sema kuliko nchi ZOTE za Afrika..Jamani kuitumia Rwanda na udogo wake huwezi kuona kuwa ni aibu kubwa sana kwetu kusingizia udogo wa nchi hali ambayo imewaingiza wao ktk vita vya wenbyewe kwa wenyewe.. na bado haitakwisha iko siku litaibuka tena maanake hoja ya mgao waardhi ndogo bado kabisa haijapatiwa ufumbuzi..

  Anyway, sasa mkuu, kwa maneno yako hayo nadhani hapa ndipo pa kuanzia.. yaani inaonyesha wazi kwamba Watanzania hatufahamu baraka tuliyokuwa nayo...Tukifahamu hilo kwanza kisha tukajiuliza kwa nini hatupigi hatua mbele kimaendeleo zaidi ya kuwa gurudumu la nyuma linalofuata tutaweza jenga hoja maana kujiuliza sisi wenyewe badala ya kusingizia ardhi iliyokuwepo toka dunia iumbwe..
  Miaka ya 70 na 80 tulikuwa chini ya Ujamaa siasa mbovu kiuchumi yet tulikuwa ranked 120's leo hii ndani ya Ubepari na opportunities zote zilizopo tumesimama 150's, mkuu kama sisi sio tairi la nyuma ni kitu gani!
  Bado unafikiria kweli ni ukubwa wa nchi!...
   
  Last edited: Feb 17, 2009
Loading...