Mbilia Bell kwishine!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbilia Bell kwishine!!!

Discussion in 'Entertainment' started by Bob K, Jul 3, 2009.

 1. B

  Bob K Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tuache masihala mbilia beli amekwisha mpaka kuifikia kutumbuiza police mess mara Bukoba mwana mama ambaye alikuwa anatingisha barani afrika nakumbuka alipokuja hapa bongo na mzee Tabu rey sikuwa mdogo sana lakini balaa lake lilikuwa kubwa kama si daimon basi ilikuwa uwanja wa taifa mtu kibao lakini kosa lake ni kumtoroka mzee huyu na kwenda kwa kwenye bendi ya Mtoto wa Omar bongo kule gabon nakumbuka mzee Tabu rey iliripotiwa na vyombo vya habari kuwa alilazwa hospitali kwa mshituko!! kama ni duwa la kuku sasa limempata hebu fikiria toka katika makumbi mbalimbalitena makubwa huko paris france leo bukoba mara police mess bado kidogo tutasikia kimboka nighty pub buguruni jamani mi naomba mshaurini apumzike mziki atafute kazi nyingine iko siku atapelekwa mpanda halafu aachwe kama defao alivyopelekwa Rukwa halafu nauli ya kurudi ikawa shida hebu waige mfano wa wanamuziki wa amerika akichacha anachili home hii mipango ya kutumbuiza toka parisi mpaka Mtwara fedhea harafu kule unafikia Urimbo gest hausi bafu la jumuiya yaaaani jamani huruma akamwombe msamaa mzee Tabu rey wadau mnasemaje katika hili naomba maoni yenu!!
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kwani watu wa Bukoba na Mtwara ndiyo hawahitaji burudani ya watu maarufu kama Mbilia? Cha maana kama wanampa mshiko na anaridhika ndiyo jambo la maana. Jaman hata sisi huku vijijini tunahitaji burudani, eti!
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu, very well said. Kuna watu wanadhani burudani kama hizi ni haki ya kundi fulani la watu tu!

  Na kuna ubaya gani akitumbuiza Police Officers mess? si ukumbi tu? unadhani mashabiki wake hawataenda?
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi nilivyomwelewa mtoa mada ni kuwa huyu mwanadada/mwanamama kwa wakati huo alikuwa na soko kubwa kiasi kwamba kutumbuiza sehemu kama police mess yeyote kwa wakati huo isingetosheleza mahitaji ya wapenzi manake maeneo hayo huwa ni madogo na pia asingeweza kuingiza kipato kikubwa kutokana na idadi ya wahudhuriaji kuwa wachache kutokana na udogo wa kumbi hivyo ikawa inamlazimu kutumbuiza kwenye kumbi kubwa au kwenye viwanja kama ilivyotanabaishwa Uwanja wa Taifa hapo juu...
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  teh teh te het..Mimi chichemi..
   
 6. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #6
  Jul 4, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KUTOKANA NA ULIVYOMUELEWA na kama kweli alimaanisha HIVYO JE?

  Uwanja wa kaitaba - BUKOBA nao ni ukumbi mdogo kushindwa kubeba mashabiki LUKUKI?????

  Mtwara pia hakuna washabiki????????

  Haya mambo ya kuwa STAR ndivyo yalivyo watu upanda na huwa kuna mwisho wake hata Yvone Chaka Chaka wa zamani sio wa LEO, just learn to live with it.

  Besides mwanamziki anayejichanganya hata kwenye ukumbi MDOGO kama huo kuna kitu anafaidi kuliko aliyeFULIA na KUCHILL MAHOME au vipi bwana Mbilia KAnyaga twende na karibu KIMBOKA......
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyo mtoa mada ndio wale wanaopenda kuabudiwa pindi wakipata nyadhifa. Bora tumekujua. Anayetumbuizwa kempisk na bukoba ni wamoja, kaka
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  Thanks Babuyao, inaelekea mtoa mada "BOB K" ndio wale wa kufagilia venyu frani za ki "check_BOB". Tukianza hivyo basi wafuatao nao watakuwa wamefulia; Beernie Man, Big Punisher, Shaggy, Eve, 50 Cents, Sean Paul etc ambao wametoka states kwenye majukwaa mabwa kuja kutoa shoo bongo, la hasha... hata huku bash ziko mswano!!!

  Tusipoangalia hata JK kuhutubia kule umang'atini tutasema na yeye kweshnehi che!!

  Mlioenda shoo ya Jana police mess - mambo yalikuwaje?? maana wengine tulizidisha mvinyo bongo zikalala
   
 9. B

  Bob K Member

  #9
  Jul 6, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  labda sijaeleweka sina maana kuwa watu wa bukoba,mtwara hawastahili burudani tena kubwa kubwa ila huyu mwana mama mbilia bell namwonea huruma kwani ukweli sasa hivi kafulia!! sasa ningekuwa naye karibu ningemtaadhalisha kuwa kwa kuwa sasa hivi yuko tayari kwenda kupafomu hata bukene au kaliua mpanda cha muhimu pesa yake,akumbuke kuwa hata maprota atakaokutana nao sasa ni wa kiwango cha chini sasa isije kutokea kuwa akaenda sehemu halafu shoo ikabuma akaishia kukosa nauli hata ya kurudi dar kwani wengi hudhani kuwa kwa kuwa alikuwa na jina hata ukimpeleka huko tanganyika atawashitua watu tanzania ya leo sio ya mwaka tisini kwani leo news latest every where juzi watu wameangalia kombe la mabara kikijini ambako hata mimi sikutegemea hivyo watanzania wa leo wanajua kabisa kuwa mbila beli keshafulia long time yatamkuta siku moja namwona anakuwa mwepesi kuru di rudi nani akumbuki defao yaliyomkuta hata pesa ya gesti alivyotoka kule rukwa ilimshinda ni afadhali ukabaki na heshima yako kuliko kutaka kuonekan mbele za watu bado uko juu wakati umeshachoka jifiche watu waulize uko wapi.

  mifano si tunayo hapa jijini dar!! chaos mwenye macho na aone na mwenye sikio na asikie kama alishidwa kuwekeza wakati anazo kwa ajili ya baadaye atapiga shoo mapaka na mkongojo!!!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Huu ubrazameni/usista duu mwingine ni uchwara tu.........watu wa kuja utawafahamu tu...........
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jamani wale mlioenda show ya MBilia, How is she doing... was the show any good??
   
 12. Rabin

  Rabin Senior Member

  #12
  Jul 7, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  He! jamani mimi simuelewi mtoa mada ana maana gani, ina maana hata Madona alivyokwenda kule malawi na kusalimia wale watoto amefulia? na mmoja akaondoka naye, je kafulia? umaarufu haumzuii mtu kuwa karibu na wengine labda kama wewe tabia yako tu kila mtu ana haki ya kupata burudani, mbona record zao zinafika kila mahali bila kujali huyu ni tajiri au fukara?
   
 13. KwayuG

  KwayuG Member

  #13
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 14, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  The place to perform a show it doesn't matter, what matter is the audience, that are there to cheer you up.
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  huyu mbilia bel inaelekea akichacha wabunge watamweka nyumba ndogo wanampenda sana ukiangalia kwenye picha spika wetu alipokuwa anadance nae dah mme wa mtu pale alikuwa mbende mbende.halafu dah ashakuwa bibi tena makunyanzi kibao hapendezi kivile ah akapumzike tu sasa
   
 15. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwalimu wako wa KUANDIKA IMLA naomba namba yake, du paragraph nzima ina comma na nukta moja tu!!!!!! sijui kama unamsomea mtu unaisomaje, SAFI LAKINI.....
   
 16. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Sasa wee chek Bob tatizo lako nini hapa?? yaani mtu akiwaletea burudani hata kwa wale ambao walidhani ni ndoto ya alinacha kumuona laivu msanii kama huyu mama Bell unaanza kuponda lol!.

  kwani unakumbuka kipindi kile alipokuja na Mzee T.L pale DOM si alitumbuiza uwanja huu wa Jamhuri! sasa akienda kule kwakina Minziro na kutumbuiza pale kaitaba kutakuwa na utofauti gani? istoshe kiingilio ni kilekile na nina uhakaika onesho likitangazwa mapema atajaza mashabiki toka mikoa na nchi za jirani pale.

  Tafadhali jenga hoja yako kwa umakini na sio kwa chuki na kudharau wananchi wa sehemu zingine.

  Amani.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kijana,

  Ukweli ni kama walivyoandika wengine kuwa siku hizi hata miji midogo wanakunywa BIA na wanapesa kishenzi. Kumbuka hayo majimbo ya ziwa kuna madini sana na vijana siku hizi wana drive na kujenga majengo makali, itakuwa kwenda kumuona Mbilia BEL?

  Kuhusu kesi ya kwenda Gabon ni kuwa:-
  Tabu Ley alimuahidi kumjengea nyumba. Bibie kasubiri nyumba haoni na akaanza kutushia nyau na ndipo Tabu Ley akamchukua na kumpeleka kwenye nyumba moja safi sana na kumwambia hii hapa. Bibie akaanza kutamba kuwa kapata mzinga wa jumba. Habari zikaenda hadi zikamfikia mtoto wa Mabutu. Kumbe ile ilikuwa nyumba ya Mabutu Son na Tabu Ley alikuwa kapanga kutuliza mambo. Mabutu Son akaja na kumtimua Mbilia Bel na bibie kwa hasira ya kunyanyaswa na aibu ya kudanganywa akakimbia kabisa Congo, na nafikiri kipindi hicho ndipo Bongo akaja kumchukua na kumuanzishia bendi nyingine akiwa SOLO na hapo akatoa vibao kama Manzili na Phenomeno etc. Jamaa huyo alikuwa akiitwa RASHID BONGO na alikuwa ni mdogo wake Omary Bongo na si mtoto wake.
   
 18. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kuzeeka ni wajibu . HAiwezekani ukaendela kuwa na mvuto wakati unazeeka. Kinachomata ni hadhi tu. Wako wanamuziki wazee kweli kweli lakini respected with milions of funs. Unamfahamu BiBi KIDUDE? Think positively , and asbtain yourself from undirectional criticisms. Mbilia Bell bado ni mzuri kwenye muziki wake tu ukiacha hayo mambo mengine ya kibinadamu.
   
  Last edited: Jul 8, 2009
 19. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  teheeee majibu mazuri kabis
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Bob K,

  Una matatizo na Bukoba na Mtwara au umekulia kwenye familia masikini aka fukara na sasa mishahara imeanza kukutana? Au ndio umeingia mjini na kufahamu ma-Hotel na makumbi makubwa?

  Nina wasiwasi na upeo wako wa mambo!

  BTW: Tabu rey ni nani? daimoni ni nini? kimboka nighty pub buguruni ipo buguruni sehemu gani?
   
Loading...