Mbigiri-Kilosa: Bei ya nyanya yashuka hadi sh 700 kwa ndoo ya lita 20

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,107
1,782
Rais wetu mheshimiwa sana, wakati unashughulikia majipu, serikali kuhamia Dodoma, watumishi hewa, mikutano ya kisiasa, bil 20 za uniform za polisi, kupatiwa risiti kila tununuapo bidhaa na mengineyo, kumbuka kuna wakulima wanashindwa kuuza mazao yao.

Katika kijiji cha Mbigiri kilichopo Kilosa kata ya Mbigiri, wakulima wameitikia sana wito wako wa "HAPA KAZI TU" kwa kulima sana zao la nyanya lakini hawana soko la kuuzia mazao yao.

Kwa sasa bei ya plasitiki la ujazo wa lita 20 ni Tshs 700. Hii ni aibu sana kwenye serikali inayopiga kelele kila siku na kuwataka watanzania wafanye kazi kwa bidii.

Baada ya kupiga marufuku kucheza "pull table" mchana, vijana wameitikia wito kwa kujikita katika kilimo tasnia pekee isiyohitaji mtaji mkubwa sana ila nguvu binafsi.
Kwa kweli inasikitisha sana kuona vijana hao wamefanikiwa kupata zao la nyanya kwa wingi ila hawana soko la kuuzia hizo nyanya.

Nyanya ni nyingi sana mashambani na zinaoza kwa vile hakuna wateja wa kuzinunua...lakini nguvu nyingi zinaelekezwa kupiga vita mikutano ya kisiasa!
Nakutahadharisha mh Rais walio kupigia kura wewe ni hao wakulima...ukicheza nao ngoma isiyo na staili ya uchezaji utawapoteza wote.

Kilimo umekisahau sana mh.....watu wanasikitika sana kule kijijini kwa kukosa soko la mazao yao.

"TIME WILL TELL"
Mzalendo wa nchi.

upload_2016-8-4_13-40-1.png

Box la mbao likijaa ni Tshs 2000. Baadhi ya wakulima hawajakata tamaa wanauza hivyohivyo.

upload_2016-8-4_13-40-35.png

"HAPA KAZI TU".......but there is no stable markets.
 
Rais wetu mheshimiwa sana, wakati unashughulikia majipu, serikali kuhamia Dodoma, watumishi hewa, mikutano ya kisiasa, bil 20 za uniform za polisi,kupatiwa risiti kila tununuapo bidhaa na mengineyo, kumbuka kuna wakulima wanashindwa kuuza mazao yao.
Katika kijiji cha Mbigiri kilichopo KIlosa kata ya Mbigiri, wakulima wameitikia sana wito wako wa "HAPA KAZI TU" kwa kulima sana zao la nyanya lakini hawana soko la kuuzia mazao yao.

Kwa sasa bei ya plasitiki la ujazo wa lita 20 ni Tshs 700. Hii ni haibu sana kwenye serikali inayopiga kelele kila siku na kuwataka watanzania wafanye kazi kwa bidii.
Baada ya kupiga marufuku kucheza "pull table" mchana, vijana wameitikia wito kwa kujikita katika kilimo tasinia pekee hisiyoitaji mtaji mkubwa sana ila nguvu binafsi.
Kwa kweli inasikitisha sana kuona vijana hao wamefanikiwa kupata zao la nyanya kwa wingi ila hawana soko la kuuzia hizo nyanya.
Nyanya ni nyingi sana mashambani na zinaoza kwa vile hakuna wateja wa kuzinunua...lakini nguvu nyingi zinaelekezwa kupiga vita mikutano ya kisiasa!
Nakutahadharisha mh rais walio kupigia kura wewe ni hao wakulima...ukicheza nao ngoma hisiyo na staili ya uchezaji utawapoteza wote,.
Kilimo umekisahau sana mh.....watu wanasikitika sana kule kijijini kwa kukosa soko la mazao yao.
"TIME WILL TELL"
Mzalendo wa nchi.View attachment 375939
box la mmbao likijaa ni tshs 2000. Baadhi ya wakulima hawajakata tamaa wanauza hivyohivyo.


View attachment 375940
"HAPA KAZI TU".......but there is no stable markets.
Duh nilipata simu toka hom Mombo korogwe nikaambiwa debe moja la nyanya ni 2500 nikaona kwl soko limekua baya kumbe kuna wenzetu uko imeshuka hadi 700
 
Tanzania ya viwanda inakuja.Kama tunazalisha kwa wingi,kwa bei nafuu,kabla hazijaoza,na incentive ya Wenye Mitaji ya Kufanya processing Kuja.Tuendelee Kulima.Hata Ufugaji uko bei chini,hivyo Viwanda vya Kukamua Mafuta vipimo Njiani!!
 
Viwanda vya usindikaji wa mazao ndio tunahitaji kuanza navyo kwanza, sambamba na kuboresha kilimo...cha ajabu nawashangaa wanasema watapiga marufuku nguo za mitumba ili za ndani zipate soko wakati hata teknolojia ya kusindika nyanya inatusumbua...kwa sasa hivi au miaka 5 utaweza kuzalisha nguo quality zi replace nguo kutoka nje kwa bei ileile au pungufu? sidhani...inahitaji muda sana
 
Inatakiwa ifike mahala tuunde hoja zenye mantiki, Bei ya mazao mara nyingi inaamuliwa na Demand na Supply, Ukiona bei imeshuka sana ujue Supply imekuwa kubwa zaidi ya huitaji. Ndo kilichopo sasa, Supply ya Nyanya Imekuwa kubwa sana kwa sababu ya Mavuno ni mengi.
 
Hatari! Maisha ni magumu kwa kweli! Itakubidi uuze takribani ndo 30 ili uweze kununua suruali 1, ndoo tano kilo 1 ya sukari. Na hapo ukute hata wateja wanapatikana kwa shida. MUNGU atusaidie.
 
Inatakiwa ifike mahala tuunde hoja zenye mantiki, Bei ya mazao mara nyingi inaamuliwa na Demand na Supply, Ukiona bei imeshuka sana ujue Supply imekuwa kubwa zaidi ya huitaji. Ndo kilichopo sasa, Supply ya Nyanya Imekuwa kubwa sana kwa sababu ya Mavuno ni mengi.
Huwezi kukaa tu na kulia supply imekuwa kubwa! Supply ikiwa kubwa bado kuna njia za kufanya ili kuongeza demand. 1: Watanzania wengi bado tumelala. Hatuna ubunifu wa ujasiria mali bali tunaigana tu. Kwa mfano sasa ukienda Dar unakuta maelfu ya viduka vya nguo na Bar. Hakuna anayefikiri tofauti angalau atumie fursa kama hiyo kuhamishia hizo nyanya sehemu zenye demand kubwa! 2: Nyanya ni zao la msimu na sehemu nyingi hutatua tatizo la supply kubwa kwa kuwa na viwanda vya kusindika nyanya ambazo zitatumika sehemu nyingine zenye demand kubwa.
 
Mkuu hii ni fursa,unaweza ni PM kuja kuzibeba kuleta Dar?Najua Dar hata nikiuza kwa elfu 15 tu kwa box italipa.
Kabla ya kuleta dar Nenda kaulizie kwanza bei ya tenga la nyanya...
Ukiona huko kijijini wanalia jua mjini hali si shwari pia ktk bei...
 
Waje wachumi watufafanulie kuwa sasa shillingi imepanda thamani kwa maana ndoo ya 7,000/- sasa ni 700/-
 
Huwezi kukaa tu na kulia supply imekuwa kubwa! Supply ikiwa kubwa bado kuna njia za kufanya ili kuongeza demand. 1: Watanzania wengi bado tumelala. Hatuna ubunifu wa ujasiria mali bali tunaigana tu. Kwa mfano sasa ukienda Dar unakuta maelfu ya viduka vya nguo na Bar. Hakuna anayefikiri
tofauti angalau atumie fursa kama hiyo
kuhamishia hizo nyanya sehemu zenye demand kubwa! 2: Nyanya ni zao la msimu na sehem
u nyingi hutatua tatizo la supply kubwa kwa
kuwa na viwanda vya kusindika nyanya ambazo zitatumika sehemu nyingine zenye demand
kubwa.
Umesema kitu cha maana lakini tatizo nyanya hizo hazikai kwa muda mrefu huwa zinawahi kuoza....nyanya ambazo zinaweza kuvumilia ni za kutoka mangula...
Bado wakulima wanahitaji wawepo watu wanao sindika nyanya
 
Back
Top Bottom