Baba Adele
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 208
- 229
Wana JF,
Kuna habari ya kusikitisha imetokea maeneo ya Mbezi Luis kwa Robert.
Kijana wa kiume umri miaka 9 jina Raheem amesombwa na maji ya mto alipokua akijaribu kuvuka.
Jitihada za kumtafuta zinaendelea mpaka sasa bila mafanikio. Imeelezwa kua kijana huyo alitoka na wenzio baada ya kurudi msikitini swala ya Ijumaa akiwa na baba yake wakiwa kwenye bajaji lakini baada ya kurudishwa nyumbani alitoka na wenzie na kujaribu kuvuka mto ndipo maji yalimshinda na kumsomba.
Mpaka sasa haijafahamika kama yu hai au amefariki. Kwa kawaida mto hua unatumika kama njia ya kupita kwa miguu chini lakini mvua zinapozidi hujaa maji hivyo ni hatari si tu kwa watoto bali hata watu wazima hulazimika kuzunguka.
(Sisi sote ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)
Wana JF baada ya salam nichukue fursa hii kuwajulisha kama amnavyo nilitoa taarifa ya kuchukuliwa na maji kijana Raheem leo majira ya mchana baada ya sala ya Ijumaa.
Taarifa zinasema mtoto Raheem amepatikana akiwa ameshafariki maeneo ya Kawe Bondeni.
Kijana Raheem kabla ya kufikwa na umauti alitoka akiwa na baba yake na wenzake kwenda msikitini na baada ya swala baba yao aliwaaga akienda kwenye shughuli zake ndipo vijana hao walipo enda kupota njia ya mtoni amabako maji yalikua yamejaa kutokana na mvua.
Raheem aliteleza na hivyo ndugu yake alitaka kuingia kumuokoa ndipo alisikia sauti ya mtu mzima kimkataza na kuwaondoa eno hilo hatari, inasemekana watoto wa nyumba moja wote watatu walitaka kuingia kumfuata mwenzao bila ya kujua maskini hatari ambayo ingewakuta lakini yote ilikua kumnusuru mwenzao ambae Allah alimwita leo.
Vijana hao baada ya kufukuzwa eneo la mto na kutoa taarifa kua mwenzao ameondoka na maji ndipo jitihada za kumfuatilia zilipoanza bila mafanikio kwakua maji yalikua mengi sana.
Baadae mdau wa jf alitufahamisha kua mtoto huyo amepatikana akiwa amefariki maeneo ya Kawe.
Baada ya kutoa taatifa hii naomba nitoe wito kwa wana jamii.
Mazingira ya kifo cha Raheem Toba ni ahadi lakini wazazi hasa ambao mazingira yanayowazunguka kuna mito wanahitajika kua makini sana na wasiyegemee watoto wana uwezo wa kuyapima mambo kua ni ya hatari au laa.
Kutokana na mazingira nilivyoyaona. Ilimpasa Baba Raheem ahakikishe kua watoto wamefika nyumbani salama kisha yeye ndio aondoke kwakua jinsi yalivyo mazingira km mvua inanyesha basi hakuna njia nyingine mpaka wapite barabara ya lami ambako kuna daraja.
Siku za mvua kubwa watoto wasitoke majumbani hasa maeneo ya mito isipokua kwa usimamizi hata kama ni kwenda Shule, Madrasa, Kanisani au Msikitini.
Walimu wasiwaruhusu watoto kutoka mashuleni ikiwezekana wafuatwe na wazazi wao.
Leo nimeshuhudia mtoto wa jirani angu ambae anapenda kupita shortcut ya mtoni kwa bahati nzuru alijiongeza akapanda bajaji
Wazaz na walezi jitahidini kuwapa elimu watoto kuogopa maji, lakini pia liende sanjari na kuwafundisha watoto katika umri mdogo kujua kuogelea.
Nakumbuka niliwahi kusoma kitabu cha dini ya kiislam nikaona sehemu Prophet Muhammad amesema "wafundisheni watoto wenu vitu vitatu. 1. Adabu 2 Kulenga Shabaha na 3 Kuogelea"
Mwisho natoa pole kwa familia ya Shekh Toba Baba wa marehem Raheem.
Sisi sote ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea.

UPDATES
Innaa lilah wainnaa ilyhi raajiuuni.(Sisi sote ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)