Mbezi Louis: Polisi wamewagonga watembea kwa miguu waliokuwa wanavuka barabara.

Ni leo tu nilikuwa najitafakari namna askari wanavyovunja sheria za barabarani wakati mwingi bila hata sababu ya msingi. Overtaking za kijinga tena maeneo hatari kabisa, wao ni kama sheria za barabarani haziwahusu kabisa. Jeshi linapokosa kuongozwa na kutii sheria na kanuni hegeuka na kuwa genge la wahalifu. IGP achukue hatua kabla hatujachelewa sana
Polisi hawatii sheria, wanasisitiza wananchi watii sheria bila shuruti.
 
Sipati picha hapo ndio ingekua gari ya private imegonga hao watu. IGP lazima angeitisha press kuwatolea shombo na povu la kutosha maderava wa magari binafsi.

"Nyie maderava wa magari binafsi, hivi hamuoni alama za barabarani kweli? Mnaendesha kwa kuvunja sheria za barabarani hovyo, watu wanavuka kwenye zebra unakwenda kuwagonga, unaona kibao cha STOP unakwenda spidi. Ina maana hamuoni alama za barabarani? Au mnataka mpate sababu ya kuwasema vijana wangu wa polisi na ma trafic kwamba ni wakorofi kwa maderava" - HAIJIPII ZERO.

Nani tena vile hapo chini?
 
Back
Top Bottom