robson kiria
Member
- Apr 11, 2014
- 73
- 105
. . L...Habari JamiiForums.
Leo 08/11/2021 kilichotokea eneo la Mbezi Louis ni kichocheo cha vurugu. Hii inatokana na maamuzi yaliyotolewa na mkuu wa wilaya na viongozi wengine ambao waliongozana kwenye msafara.
Watu (Machinga) tulikuwa na vipande vyetu tuliweka mabanda na wengine meza na biashara zilikuwa zinaendelea. Kufuatia agizo la kutolewa kwenye hifadhi ya barabara na maeneo mengine ambayo sio rafiki tulikubali na kutoa mabanda yetu na maeneo yalibaki wazi.
Cha kushangaza mkuu wa wilaya na wenzako leo mmetoa amri ya watu kurudi kujigawia maeneo na kuendelea na biashara. Hadi muda huu ni mpambano watu wanagombania nafasi na kurudisha mabanda.
Kilichoniuma ni waliokuwa na maeneo wanafika eneo la tukio na kuona mtu ambaye hajawahi kuwa na biashara pale Mbezi Louis amewahi nafasi, hata wapita njia nao wanagombania maeneo.
Mkuu wa wilaya ungetumia japo akili kidogo na kutoa tamko la kueleweka kuwa watu warudi kwenye maeneo yao ya awali sio kusema kila mtu apambanie nafasi(kugombania).
Kutokana na taarifa yako watu hawajawahi kuwa na maeneo wala kuhitaji au kuwa na biashara lakini wanapigania maeneo ili wamiliki.
Maoni yangu: Tusirudishwe tena kufanya biashara barabarani na maeneo mengine ya wazi.
Mimi ni Machinga kutoka Mbezi Louis.
Kiwango cha Elimu: Master of Laws in Procedural Law and International Legal Practice.
Mawasiliano yangu ni PM.