Mbezi Beach, Dar: Mwanamke achoma nyumba ya mpenziwe wa zamani

Mbezi kuna nini mbona matukio..sasa hivi itabidi kila asubuhi niwe 'nagoogle' mbezi Ili kupata matukio ya kibabe.
 
Mwanamke wa kikurya amechoma nyumba ya aliyekuwa mwanaume wake mkazi wa mbezi Beach kwa komba kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.

Tukio hili lilitekelezwa wakati mwanaume huyo alipokuwa ameenda kazini. Wananchi alofanikiwa kumkamata mtuhumiwa na hivi ninavyoandika mtuhumiwa huyu amefikishwa polisi.

Jamani mkiachwa achikeni, mkitemwa kubalini kutemeka.

-----

Msichana aliyejulikana kwa jina la Tina mkazi wa eneo la Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya anayedaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake aitwaye kwa jina moja la Kelvin mkazi wa Mbezi Bondeni.

Daaaahhhhh kweli siku zote kuingia ni rahic sana ila kutoka sasa ni mtihani mgumu kama huamini ingia kwenye kuvuta bangi afu utoke........
 
Ifikie hatua Serikali ifanyie kazi sheria zake kikamilifu bila kuangalia kama mtenda kosa ni mwamamke au mwanaume... La sivyo tunakoelekea ni kubaya!
Hapo zitaletwa sababu za kisaikoloji zitasomwa page saba mahakamani za hukumu zimajeaa neno 'saikoloji effect' and mental 'disfunction' ha ha ha
 
Yawezekana wote tukamshambulia huyo dada, lakini kwa upande mwingine wa shilling huwenda alikuwa na machungu na jasho lake kwa huyo mpz wake ambaye kaamua kuumwaga ili kimwana mwezake afaidi...hatujui wametoka naye wapi...na kachangia kiasi gani mafanikio ya jamaa.

Kupotezeana muda huwa ndiyo machungu makuu wanayopata wasichana wengi...unaishi na mpz miaka 5 hadi hata 8 afu unambwaga unatafuta kimwana mwingine unaoa..hii si haki kabisa, na mbaya zaidi sheria zetu hazitambui kipengele hiki cha kupotezeana muda.

Alichokosea huyu dada ambacho wengi wanamukukumu nacho ki kitendo cha kufanya kosa... kwa kweli hapa ndipo alipokosea.. nafikri baada ya kukosa room ya kusemea na kusikilizwa.

Ila sasa jamii ijifunze kwamba kuna kina dada wengi sana wanaumia rohoni kwa mambo haya...miaka 5 hadi 10 mnahangaikia maisha hamjaoana...afu mambo safi jamaa anakumwaga anaoa kidosho kingime unaanza kula naye bata huku ukishuhudia - hapana hii si haki sheria zetu zilimulike hili ili kuwe na fidia.

Wanaume kwa hili na sisi tunakosea...!!
Tuko sawa kabisa ndoa hailazmishwi,wanaume wangapi wamegharamia elimu za madem wako na kuachwa...wangeamua kulipiza ingekuaje
 
Kulikuwa na haja gani ya kuandika kabila la huyo mwanamke?

Alafu bila picha huu ni umbea tu!
Ili tujue tuweze kuassess!! Kufanya vituko vya ajabu na kikatili vinaendana sana na kabila la mtu aliyefanya tukio!!!
 
Mwanamke wa kikurya amechoma nyumba ya aliyekuwa mwanaume wake mkazi wa mbezi Beach kwa komba kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.

Tukio hili lilitekelezwa wakati mwanaume huyo alipokuwa ameenda kazini. Wananchi alofanikiwa kumkamata mtuhumiwa na hivi ninavyoandika mtuhumiwa huyu amefikishwa polisi.

Jamani mkiachwa achikeni, mkitemwa kubalini kutemeka.

-----

Msichana aliyejulikana kwa jina la Tina mkazi wa eneo la Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya anayedaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake aitwaye kwa jina moja la Kelvin mkazi wa Mbezi Bondeni.

Wakurya nao wameanza hizi visa za kuchoma nyumba
 
Back
Top Bottom