Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Kwa muda mrefu sasa barabara za Mbezi Beach, tena eneo lote halipati matunzo yanayostahili eneo hili.
Barabara karibu zote ni mbovu kupundukia.
Ukiacha barabara mbili tu zilizojengwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, hakuna chochote kinachofanyika, na barabara hizo ni Ally Sykes na ile ya Kawe-Africana.
Kuna barabara nyingi tu ambazo kuzitumia ni kero kubwa, na barabara hizo ni:
-Mbezi Garden hadi Baraza la mitihani
-Barabara ya kuelekea NSSF flats(inaungana na barabara ya Kawe/Africana)
-River rd kwenda shule ya St Marys
-Barabara ya kuunganisha Kunduchi na eneo la Kilongawima
-barabara ya Mbezi Jogoo
Pamoja na barabara hizo kuna ile barabara ambayo ni mfupa uliowashinda wengi, barabara ya Mbezi Samaki Wabichi hadi Goba.
Inabidi tuandike kwa masikitiko juu ya barabara hizi maana katika wilaya nyingine kama Ilala na Temeke kazi kubwa inafanyika, na mimi mwenyewe nimepita Temeke kwa kweli juhudi za wilaya hiyo kujenga hadi vichochoroni inatiamoyo-hongera Mbunge wa eneo hilo.
Kule Oysterbay lami inatandikwa hadi barabara ndogo kabisa zenye kuhudumia watu si zaidi ya kumi!
Na hapo ndio nawageukia wawakilishi wetu, mnatuteteaje kwenye vikao vyenu?
Mbona wala hatusikii kuwa barabara nillizotaja ziko kwenye mpango wa kujengwa?
Msituangushe wawakilishi wetu